Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 28 Septemba 2015

Viongozi wa Burkina Faso walioshikiliwa wapo salama

Brigedia jenerali Gilbert Diendéré wa Burkina FasoMkuu wa baraza jipya la utawala Burkina Faso alisema Rais na Waziri Mkuu wapo salama chini ya ulinzi wa jeshi na karibuni wataachiwa.
Brigedia Jenerali, Gilbert Diendere alizungumza na Sauti ya Amerika hapo Alhamis, siku moja baada ya wanajeshi kuiangusha serikali ya muda kwenye taifa la Afrika magharibi na kuwakamata viongozi wake. Jenerali huyo alisema jeshi lilipanga mapinduzi kwa sababu utaratibu wa kisiasa nchini humo haukuwa wa haki.
Alisema ataanza mashauriano ya kisiasa yanayojumuisha pande zote. Burkina Faso ilipanga kufanya uchaguzi wa urais na bunge hapo Oktoba 11. Tarehe hiyo hivi sasa ipo njia panda.
Waandamanaji vijana wa Burkina faso
Waandamanaji vijana wa Burkina faso
Watu wasiopungua watatu waliripotiwa kuuwawa wakati waandamanaji vijana walipojaribu kukusanyika karibu na makazi ya rais huko Ouagadougou na ubalozi wa Marekani ulisema vizuizi vya barabarani vimewekwa kote mjini humo.
White House mjini Washington ililaani vikali kile ilichokiita jaribio ambalo ni kinyume cha katiba la kuchukua madaraka. Naibu msaidizi wa Umoja wa Afrika, Erastus Mwencha aliwataka Alhamis viongozi hao wa kijeshi haraka kukabidhi madaraka kwa serikali ya muda. “Serikali yeyote ambayo haifuati katiba inalaumiwa moja kwa moja kwa sababu tunaamini katika utawala wa sheria na mabadiliko yeyote ya madaraka lazima yafuate utaratibu wa katiba”, alisema Mwencha.
Pia aliwasihi watu kutoshirikiana na jeshi kuchukua madaraka.
Serikali ya muda ilichukua madaraka nchini Burkina Faso wakati ghasia maarufu zilizomuondoa Rais Blaise Compaore madarakani mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kuwepo mamlakani kwa miaka 27. Alipanga kubadili katiba ili aweze kuongeza utawala wake.

Jumapili, 27 Septemba 2015

Mkuu wa baraza jipya la utawala Burkina Faso alisema Rais na Waziri Mkuu wapo salama chini ya ulinzi wa jeshi na karibuni wataachiwa.

Mkuu wa baraza jipya la utawala Burkina Faso alisema Rais na Waziri Mkuu wapo salama chini ya ulinzi wa jeshi na karibuni wataachiwa.
Brigedia Jenerali, Gilbert Diendere alizungumza na Sauti ya Amerika hapo Alhamis, siku moja baada ya wanajeshi kuiangusha serikali ya muda kwenye taifa la Afrika magharibi na kuwakamata viongozi wake. Jenerali huyo alisema jeshi lilipanga mapinduzi kwa sababu utaratibu wa kisiasa nchini humo haukuwa wa haki.
Alisema ataanza mashauriano ya kisiasa yanayojumuisha pande zote. Burkina Faso ilipanga kufanya uchaguzi wa urais na bunge hapo Oktoba 11. Tarehe hiyo hivi sasa ipo njia panda.
Waandamanaji vijana wa Burkina faso
Waandamanaji vijana wa Burkina faso
Watu wasiopungua watatu waliripotiwa kuuwawa wakati waandamanaji vijana walipojaribu kukusanyika karibu na makazi ya rais huko Ouagadougou na ubalozi wa Marekani ulisema vizuizi vya barabarani vimewekwa kote mjini humo.
White House mjini Washington ililaani vikali kile ilichokiita jaribio ambalo ni kinyume cha katiba la kuchukua madaraka. Naibu msaidizi wa Umoja wa Afrika, Erastus Mwencha aliwataka Alhamis viongozi hao wa kijeshi haraka kukabidhi madaraka kwa serikali ya muda. “Serikali yeyote ambayo haifuati katiba inalaumiwa moja kwa moja kwa sababu tunaamini katika utawala wa sheria na mabadiliko yeyote ya madaraka lazima yafuate utaratibu wa katiba”, alisema Mwencha.
Pia aliwasihi watu kutoshirikiana na jeshi kuchukua madaraka.
Serikali ya muda ilichukua madaraka nchini Burkina Faso wakati ghasia maarufu zilizomuondoa Rais Blaise Compaore madarakani mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kuwepo mamlakani kwa miaka 27. Alipanga kubadili katiba ili aweze kuongeza utawala wake.

Jumatatu, 21 Septemba 2015

Kuzidi hofu ya madhara ya jinai za Saudia nchini Yemen

  Wasiwasi wa taasisi za kimataifa na za nchini Yemen kuhusu jinai za ukoo wa Aal Saud nchini humo umeongezeka mno hivi sasa huku Saudia na kundi lake la nchi zinazotenda jinai, zikizidisha ukatili wao dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Yemen. Jeremy Hopkins, mjumbe wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Yemen ametoa tamko kuhusu kuongezeka jinai na uvunjaji wa haki za wananchi wa Yemen na kuharibiwa miundombinu ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu, na kusema kuwa, ana wasiwasi mkubwa wa kutofika shehena ya misaada ya kibinadamu kwa watu 11 elfu waliokwama huko kusini mwa mji mkuu wa Sana’a, kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Saudia. Jeremy Hopkins ameongeza kuwa, kitendo cha wanajeshi wa Saudia cha kushambulia shehena za misaada ya kibinadamu na maeneo ya kusafishia maji nchini Yemen kinasikitisha sana na kimewasababishia matatizo makubwa wakazi wa eneo hilo. Wizara ya Afya ya Yemen jana Jumamosi ilitoa taarifa na kusema kuwa hospitali za mji mkuu Sana’a hazina uwezo tena wa kupokea majeruhi na zimekumbwa na uhaba mkubwa wa madawa, mafuta na mahitaji mengine ya lazima. Wizara ya Afya ya Yemen imezitaka taasisi za kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuwaokoa wagonjwa na majeruhi wa mashambulio ya anga ya Saudia. Muhammad al Masouri, Katibu Mkuu wa taasisi ya masuala ya kisheria ya “al Bayt al Qanuni” ya Yemen amesema kuwa, hivi sasa haiyumkiniki tena kuzalisha maji safi nchini humo kutokana na kukatika umeme na kuharibiwa mabomba ya mafuta. Ametahadharisha kuwa, wananchi milioni 27 wa Yemen wanakabiliwa na hatari kutoka kila upande. Wanajeshi wa utawala wa ukoo wa Aal Saud jana Jumamosi pia waliendelea kufanya jinai kwenye maeneo ya makazi ya raia katika mikoa ya Sana’a, Sa’ada, Taez, al Baydha na al Hudaydah nchini Yemen na kuua makumi ya wananchi wasio na hatia kujeruhi wengine 100. Vile vile ndege vamizi za Saudia na genge lake zimeshambulia mara 20 majengo ya Wizara ya Vijana, Wizara ya Mambo ya Ndani na kituo cha polisi huko Sana’a. Amma cha kusikitisha zaidi ni kuona kuwa jinai hizo za Saudi Arabia zinafanyika mbele ya macho ya jamii ya kimataifa na mashirika yanayojigamba kuwa ni watetezi wa haki za binadamu na utawala wa sheria, ulimwenguni. Kimya cha mashirika hayo kimezidi kuwa kikubwa katika hali ambayo, shirika la habari la al Ahd la nchini Yemen limeripoti kuwa, Saudi Arabia inatumia pia makombora yenye gesi ya sumu dhidi ya wananchi wa Yemen. Kwa mujibu wa shirika hilo, gesi hizo za sumu zilizoenea kwenye makazi ya raia na mashamba ya kilimo, zimepelekea kuzuka magonjwa ya ajabu nchini Yemen. Houthis 

Sudan yatoa wito dhidi ya Israel

Sudan yatoa wito wa kusimama kidete dhidi ya Israel
Serikali ya Sudan imeutaka ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kusimama kidete mkabala na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjidul Aqswa. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imetoa taarifa kuhusiana na uvamizi na hujuma za Israel na mashambulio ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Masjidul Aqswa na waumini wa Kipalestina wanaotekeleza ibada katika msikiti huo na kuonyesha kuchukizwa mno na hatua hizo za Wazayuni. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan  imeutaka ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kuitisha mkutano wa dharura kwa ajili ya kutafuta njia za lazima za kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika msikiti wa al-Aqswa na kusimama kidete mkabala na jinai hizo za kinyama. Taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Sudan imebainisha kwamba, kusimama kidete na kuweko umoja katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu ni jambo la lazima kwa ajili ya kuhitimisha uvamizi na hujuma za Israel na kuzuia kubomolewa msikiti huo mtakatifu. Masjidul Aqswa ni eneo la tatu kwa utukufu kwa Waislamu baada ya Masjidul Haram mjini Makka na Masjidun Nabawi mjini Madina huko Saudi Arabia. Katika miaka ya hivi karibuni, Israel imeshadidisha njama na hujuma zake dhidi ya eneo hilo takatifu.

Jumapili, 13 Septemba 2015

SHEIKH ZUBEIR BIN ALLY MUFTI MPYA TANZANIA



     
 
Sheikh mkuu,mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally
      Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limemchagua sheikh Abubakar Zubeir bin Ally kuwa mufti wa Tanzania, kwenye  mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma.
       Uchaguzi huo umefanyika baada ya kifo cha aliyekuwa mufti wa Tanzania. Sheikh Issa bin Shaaban Simba aliyefariki juni 15 mwaka huu kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam,kwa ugonjwa wa kisukari na presha.
       Sheikh Abubakar Zubeir alichaguliwa baada ya kuwashinda masheikh wengine watatu waliojitokeza kushindania nafasi hiyo.
       Mwanazuoni huyo ndiye aliyekaimu wadhifa huo kwa miezi mitatu baada ya kifo cha mufti Simba, alichaguliwa kwenye mkutano wa dharura uliojumuisha wadhamini wa baraza hilo, maulamaa, masheikh wenyeviti wa mikoa na wilaya waliojumuika katika ukumbi wa hotel ya African dreams uliopo area D mjini Dodoma.
     
  Sheikh Zubeir alishinda baada ya jina la sheikh Hassan Kiburwa kutoka Kigoma kukatwa kwa kutokidhi viwango sheikh Mtupa na sheikh Ally Muhidini Mkoyagane kujitoa kwa hiari yao katika mpambano huo hivyo sheikh Abubakar Zubeir kupita bila kupingwa katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wa Bakwata zaidi ya mia tatu,na kuendelea kuandika historia.
       Katika hotuba yake ya shukrani, Sheikh mkuu, mufti Abubakar alishukuru kamati ya  Bakwata pamoja na wajumbe wote wa mkutano huo, alisema atafanya kazi yake kwa uandilifu na kuwaunganisha waislamu ambao wanaonekana kukata tamaa katika nchi yao wenyewe.
       “Nawashukuru kwa ushirikiano mlioniomnyesha na nInaahidi kuyasimamia yote mliyoyasema wakati nilipokaimishwa nafazi hii kule Bagamoyo na kubwa kufanyakazi na taasisi zote za dini zilizopo hapa nchini na nje ya nchi kwa mslahi ya waislam.Lakini pia niliahidi huko nyuma juu ya kuifanyia marekebisho katiba yetu ya Bakwata namuomba Mwenyezi MUNGU aniwezeshe nianikishe hilo kwa faida ya waislam wote na yeyote mwenye mawazo mema kw ajili ya kuboresha hali ya waislam nchini,milango iko wazi  namkaribisha kwa ushauri mzuri” alisema mufti. Aliwaomba waislam wote nchini kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa octoba 25 mwaka huu na kumtaka kila mmoja kumchagua kiongozi atakayeona anamfaa kwa ajili ya maendeleo ya eneo lake na taifa kwa ujumla.
        
Sheikh mkuu huyo amekuwa ndani ya Bakwata,akiwa mjumbe wa baraza la ulamaa tangu wakati wa uongozi wa mufti Hemed hin Jumaa bin Hemed.
Alikuwa naibu mufti wa Tanzania katika kipindii cha uongozi wa sheikh mkuu isa bin Shabani Simba na baadaye kuwa naibu kadhi nkuu wa Tanzania baada ya cheo cha unaibu mifti kufutwa kwenye katiba ya bakwata.
         Sheikh Abubakar ni zao la masheikh wakubwa nchini kama akina sheikh Hassani hin Ameer aliyeupokea uhuru wa Tanganyika mwka 1961,uwanja wa taifa Dar es Salaam,sheikh Abdallah Farsy wa Mombasa, sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo sheikh Mohamed bin Ayoub wa Tanga, mufti sheikh mkuu Hemed bin Jumaa bin Hemed.


         Na kuahidini kuwa nitafanya wema, uadilifu na heshima ya nchi yetu ili wote tumwabudu Allah (S.W) kwa amani na usalama “alisema mufti wa  Jamuhuri ya muungano wa Tanzania sheikh abubakar zubeir bin ally.


Jumatano, 9 Septemba 2015

Polisi wazuia shambulizi la kigaidi-Kenya

           Polisi nchini Kenya Jumanne waliwakamata watu watatu waliogundulika wakiwa na bomu la kienyeji walipoingia kwenye eneo la maduka ya kifahari.Kwa mujibu wa idara ya polisi ya Kenya bomu hilo liliteguliwa kwa usalama  na kulidhibiti lisilipuke.
           Mkuu wa polisi, bwana Robinson Mboloi  ambaye anaongoza kituo cha polisi cha Kasarani katika mji mkuu Nairobi akisema kuwa wamewatia mbaroni wanaume watatu ambao waligundulika kuwa na bomu hilo la kienyeji na kitufe cha kulilipua.  Eneo la maduka ambalo wanaume hao walikamatwa ni la Garden City Mall.    
           Bwana Mboloi alisema maafisa wa kitengo kinachoshughulika na milipuko walitegua bomu hilo  na eneo hilo la maduka liko salama.
Eneo hilo la maduka ambalo liko mjini Nairobi lilifunguliwa mapema mwaka huu, na kuelezewa kuwa kituo kikubwa cha maduka ya kifahari katika Afrika mashariki.
Kenya imekumbwa na mlolongo wa mashambulizi yaliyofanywa na waasi wenye uhusiano na kundi la wanamgambo wa kisomali la Al-shabaab ambao miaka miwili iliyopita walishambulia eneo la maduka la kifahari la Westgate Mall.
         Katika shambulizi hilo wanamgambo hao wa kiislamu walivamia na kuua watu takriban 67 na wafanyakazi katika siku nne za ghasia  wakidai ni majibu kwa jeshi la Kenya kuwepo nchini Somalia.
Wanaume watatu waliokamatwa Jumanne wameripotiwa  kuwa wote ni wakenya na walisimamishwa wakiwa pamoja na maafisa usalama kwenye eneo la ukaguzi la kuingia  kwenye kituo cha maduka.
Mboloi alisema kitufe cha kutegua bomu kilionekana wakati wa ukaguzi na shukran kwa kazi nzuri ya wana usalama.  Na kuongezea watachunguzwa  ili kufahamu mahusiano yao na ugaidi wa kundi la Al-shabaab.
Tangu mashambulizi ya Westgate, kundi la Al-shabaab limeendelea kuishambulia Kenya ndani ya ardhi yake huku shambulizi kubwa zaidi likiwa ni lile la mwezi April  mwaka huu wakati washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walipowaua watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa kilichopo kaskazini mashariki mwa Kenya, wengi wao wakiwa wanafunzi.

PAPA KURAHISISHA SHERIA YA TALAKA

Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika kanisa hilo .
Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo .
Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama .
Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kupokea komunio.
 Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa wanandoa , lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo