Watu wanne wameuwawa Jumamosi (12.11.2016) katika mripuko uliotokea
ndani ya kambi kubwa kabisa ya kijeshi ya Marekani nchini Afghanistan na
kujeruhi wengine kumi na nne ambapo utaifa wao haukuweza kufahamika
mara moja.
Kundi la Taliban limedai kuhusika na mripuko huo uliotokea
ndani ya kambi ya kikosi cha anga ya Bagram kaskazini ya mji mji mkuu wa
Kabul yenye ulinzi mkali wakati waasi wa kundi hilo wakizidisha
mashambulizi yao nchini kote kabla ya kuanza kwa kipindi cha majira ya
baridi ambapo kwa kawaida mashambulizi yao hupunguwa.
Msemaji wa
gavana wa jimbo la Parwan Waheed Sediqi ambako ndiko ilipo kambi hiyo ya
Bagram amesema mripuko huo umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga
ambaye amejiripua karibu na eneo la huduma ya chakula ndani ya kambi
hiyo.
Sediqi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba bado
hawajui utambulisho wa wahanga lakini mshambuliaji ni mmojawapo wa
wafanyakazi wa hapo.
Marekani ina takriban wanajeshi 10,000
nchini Afghanistan ambapo kikosi kikubwa kiko katika kambi hiyo ya
Bagram. Shambulio hilo linaonyesha ikiukaji mkubwa wa taratibu za
usalama ndani ya mojawapo ya vituo vya kijeshi vyenye ulinzi mkubwa
kabisa nchini Afghanistan.
Taliban yadai kuhusika
Kamanda
mkuu wa Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO nchini Afghanistan John
Nicholson ametowa rambi rambi kwa familia na marafiki wa wahanga
waliopoteza maisha yao katika shambulio hilo na kuwahakikishia kwamba
jamaa zao waliojeruhiwa wanapatiwa huduma nzuri kabisa na wataendelea
kuzingatiwa mawazoni.
Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah
Mujahid amesema kundi hilo la waasi limehusika na shambulio hilo ndani
ya kambi ya Bagram na kudai kusababisha maafa makubwa kwa wanajeshi
wavamizi wa Marekani.Kambi hiyo ya Bagram imekuwa ikishambuliwa mara kwa
mara na waasi wa kundi hilo la Taliban.
Mwezi wa Disemba mwaka
jana mshambiliaji wa kujitowa muhanga wa kundi la Taliban aliyekuwa
akiendesha piki piki aliuwa wanaheshi sita wa Marekani karibu na kambi
hiyo hilo likiwa mojawapo ya shambulio lililosababisha maafa makubwa
dhidi ya vikosi vya kigeni nchini humo kwa mwaka 2015.
Kuongezeka mashambulizi
Shambulio
hili la Jumamosi linakuja baada ya lori lilosheheni mabomu kubamizwa na
ubalozi mdogo wa Ujerumani katika mji wa Mazar-i-Sharif kaskazini mwa
Afganistan hapo Alhamisi usiku na kuuwa takriban watu sita na kujeruhi
wengine zaidi ya 100.
Kuongezeka kwa mashambulizi hayo dhidi ya
vituo vya mataifa ya magharibi kunakuja siku chache tu baada ya
kumalizika kwa uchaguzi wa rais wa Marekani uliokuwa na ushindani mkali.
Suala
la Afghanistan lilikuwa halikupewa uzito wakati wa kampeni za uchaguzi
nchini Marekani juu ya kwamba hali nchini humo inaweza kuwa suala la
dharura kwa rais mpya wa Marekani.
Rais mteule wa Marekani
anatarajiwa kurithi vita vya Marekani vilivyochukuwa muda mrefu kabisa
na havina dalili ya kumalizika hivi karibuni.
Tafuta katika Blogu Hii
Jumamosi, 12 Novemba 2016
Utajiri wa mtoto wa rais wa Angola
Isabel Dos Santos ni binti wa kwanza wa Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola na anamiliki utajiri wa kiasi dola bilioni 3.2 za Kimarekani, unaomfanya kuwa ndiye mwanamke tajiri kabisa barani Afrika.
Binti huyo amejijengea himaya yake kwa mapana na marefu na hasa katika mji mkuu Luanda ambao ni miongoni mwa miji ya kifakhari na ghali kabisa duniani.Unapotembea katika mji mkuu wa Angola, Luanda, ni vigumu sana kushindwa kuitambua au kukumbana na alau kampuni moja ya Isabel Dos Santos. Binti huyo wa kwanza wa Rais Eduardo Dos Santos na ambaye ni mwanamke tajiri kabisa barani humo amejenga himaya yake ya utajiri katika moja ya miji ghali kabisa duniani -kutoka sekta ya mawasiliano, benki, televisheni ya setelaiti hadi kwenye spoti - kote huko anamiliki biashara kubwa zenye majina mjini Luanda.
Isabel anahodhi kampuni ya Unitel, ambayo ni kampuni kubwa kabisa ya simu za mkononi nchini Angola ikiwa na matawi 81 ndani ya mji huo mkuu pekee na zaidi ya wateja milioni 10 nchi nzima. Anamiliki msururu wa maduka makubwa, huku akiwa pia na hisa katika mabenki ya BIC na BFA sambamba na katika kampuni ya saruji ya Nova Cimangola.
Umiliki wa kampuni kubwa za mafuta
Na kama haitoshi, mwanamama huyo anasimamia kampuni kubwa ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Sonangol pamoja na klabu ya soka ya Petro de Luanda inayofadhiliwa na kampuni yake.
Almuradi, orodha ya utajiri wa Isabel Dos Santos ni ndefu ikijumuisha pia sekta ya afya na uhusiano wake na kliniki kubwa kubwa nchini humo bila ya kuiweka kando sekta ya biashara ya madini, anasema mwanachama wa upinzani, Nelito Ekuikui:
''Tunaweza kuzungumzia pia sekta ya afya na uhusiano wake na kliniki kubwa kubwa za humu nchini bila ya kusahau sekta ya madini. Kampuni hiyo hazina ushindani. Hilo ni tatizo kubwa kwa nchi kwa sababu ni vigumu sana kwa wafanyabiashara wengine. Endapo tungekuwa na wafanyabiashara wapya tungekuwa na nafasi nyingi za ajira.''
Taswira ya Isabel kwa Waafrika
Baadhi ya watu wanamuangalia Isabel Dos Santos kama mfano wa wafanyabiashara barani Afrika ambao wametoa nafasi za ajira zinazohitajika kwa kiasi kikubwa, katika taifa ambalo asilimia 24 ya watu hawana kazi, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014. Lakini Nelito Ekuikui haliangalii suala hilo kwa jicho sawa na hilo. Yeye anasema utajiri wa Isabel na biashara zake nchini Angola hazina mpinzani na hilo ni tatizo. Mwanaharakati wa Angola, Benmedoto Jeremias, anasema kwamba kuwa binti wa rais wa nchi kumemrahisishia mwanamama huyo shughuli zake zote ikilinganishwa na wawekezaji wengine, ''Kila kitu anachokimiliki Isabel Dos Santos kimetokana na upendeleo na fursa anazopata kutoka kwa baba yake. Sio mali alizopata kwa juhudi zake''
Kwa upande mwingine, mwandishi habari Rafael Marques ambaye amekuwa akifuatilia mzizi wa utajiri wa Isabel Dos Santos kwa kipindi cha miaka mingi, anasema kwamba baba yake, Jose Eduardo Dos Santos, amekuwa na dhima kubwa katika kumjengea utajiri huo.
Mwandishi huyo wa habari wa Angola aliiambia DW mapema mwaka huu kwamba kila alichokitaka Isabel, baba yake alihakikisha anakipata. Dos Santos alitumia hadi nafasi yake kama rais kumpa mwanamwe huyo majukumu ya kusimamia fedha katika mikataba mikubwa mikubwa ya serikali, ingawa mara nyingi Isabel amekuwa akizipinga tuhuma hizo za kupendelewa.
Na baada ya kuiongoza kampuni kubwa ya nishati ya mafuta ya Sonangol na kufikia hatua hadi ya kuwa mwekezaji mkubwa nchini Ureno, mkoloni wa zamani wa Angola, wapinzani wanahisi hana tena pa kwenda na sasa huenda akageukia kujaribu katika siasa. Mwanaharakati Benedito Jeremias anakubaliana na hilo akisema mrembo huyo wa miaka 43 huenda ikawa hata ana mipango ya kukirithi kiti kinachokaliwa na baba yake.
Tume ya uchaguzi DRC yahusishwa na kadhia ya rushwa
Gazeti moja la Ubelgiji limechapisha ripoti wiki iliyopita likisema
kuwa tume ya uchaguzi ya Congo imelipwa takriban dola milioni 2.4 kama
ada kwa benki zenye uhusiano na rais wa DRC, Joseph Kabila.
Gazeti hilo pia limesema tume hiyo ilitoa kiasi cha dola milioni 7.5 fedha taslimu kutoka benki ya BFGI, kwa sababu ambazo haziko bayana. Madai hayo yanahusishwa na mkopo wa dola bilioni 25 ambao benki uliuotoa kwa tume hiyo ya uchaguzi inayojulikana kama CENI.
Uchaguzi wa DRC ulitarajiwa kufanyika mwezi huu, lakini umeakhirishwa mpaka Aprili 2018. Serikali imedai kwamba ukosefu wa rasilimali za kifedha unaoikumba CENI ni moja ya sababu kuu kuhusiana na uchelewesho huo.
Rais wa shirika la kisheria la Congo, Georges Kapiamba ameiambia VOA kuwa ugunduzi huo unatia wasi wasi mkubwa hasa kutokana rasilimali ambazo wamepewa CENI na kwasababu tume ya uchaguzi ilijidai kuwa haitaweza kuandaa uchaguzi kulingana muda uliowekwa kikatiba kwa misingi kuwa haikuwa na fedha za kutosha.
Kapiamba amemuandikia mwanasheria mkuu wa Congo akimtaka kuchunguza suala hili. Lakini hatarajii kuwa ombi lake litashughulikiwa.
Kulinga na ujuzi wetu katika siku zilizopita, Kapiamba amesema, hawana imani kuwa mwanasheria mkuu anaweza kutekeleza hilo kwa uhuru kama ambavyo tungependa. Kapiambia anadai kuwa wale wenye rasilimali au wale ambao wako kwenye chama tawala wanaweza kulindwa kwa chochote kile ambacho wanakifanya au vitenda vyao.
Serikali ya Ubelgiji pia imetaka uchunguzi kamili ufanywe.
Kwa mujibu wa benki, ada hizi si za kawaida kupewa kiwango hiki cha mkopo, wakati rais wa CENI amedai kwamba kutoa fedha taslimu kutoka katika benki ilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mishahara, kukodi magari na kununua mafuta katika sehemu za ndani za nchi ambako hakuna huduma za benki.
Ugunduzi huo umevutia mtizamo wa ziada kwasababu kaka wa kambo wa Kabila ni mkuu wa BFGI na moja ya dada zake rais aliorodheshwa kuwa mmiliki wa asilimia 40 katika benki kuanzia Oktoba 2014.
Shutuma hizi, ni chanzo cha nyaraka ambazo zimepelekwa kwenye vyombo vya habari na mfanyakazi wa zamani wa BFGI, na pia zilimlenga Albert Yuma, rais wa Gecamines, kampuni ya taifa ya uchimbaji madini, na mshirika wa karibu wa Kabila.

Trump: Sitafuta mpango wa Obamacare
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
aliyefanya kampeini ya kupinga Bima ya afya inayofaahamika kama Obama
care, sasa amesema atafanyia marekebisho machache kipengee cha sheria
juu ya bima hiyo ya matibabu kwa gharama nafuu.
Katika mahojiano
ya kwanza tangu achaguliwe rais siku ya Jumanne, Trump ametangaza
mageuzi makubwa ya sera punde atakapochukua nafasi ya Barack Obama
katika Ikulu ya White House mwezi Januari mwaka ujao.Trump, aliyesisitiza vikali kuwa atafutilia mbali bima hiyo inayowapa fursa mamilioni ya Wamarekani maskini kupata huduma ya afya kwa bei nafuu punde tu atakapochaguliwa rais, yaonekana amebadilisha msimamo wake juu ya suala hilo.
Na Katika kile kinachoonekana kulegeza msimamo wake juu ya mpinzani wake Hillary Clinton, Rais huyo mteule amesema,Clinton ni mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa.
Alhamisi, 3 Novemba 2016
Uchunguzi waanza kutokana na kuchomwa kanisa la kihistoria Marekani
Maafisa wa usalama wa Marekani wameanzisha uchunguzi wa haki za
kiraia baada ya kanisa moja la watu weusi katika jimbo la kusini la
Mississipi baada ya kuchomwa moto na kuandikwa kwa rangi alama ya
“Mpigie kura Trump” .
Kanisa hilo la kihistoria lililojengwa miaka 111 iliyopita la Hopewell Missionary huko Greenville Mississipi liliharibika sana kutokana na maji mengi ya kuzima moto na moshi hapo Jumanne usiku.
Meya wa Greenville Errick Simmons alisema kwamba wanalichukulia tukio hilo kama uhalifu wa chuki kwasababu ya ujumbe wa kisiasa ambao wanaamini ulikuwa na lengo la kusababisha kitisho kwsa waumini wapiga kura.
Anasema kitendo hicho ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya haki ya wananchi kuabudu kwa uhuru.
Meya huyo alisema kwamba Idara ya upelelezi wa jinai , FBI na idara ya upelelezi ya jimbo la Mississipi wanasaidia katika uchunguzi huo.

Kiongozi wa IS asema hakuna kusalimu amri
Wakati vikosi vya Iraq vikizidi kuusogelea mji wa Mosul, kiongozi wa
wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS Abu Bakr al-Baghdadi
amewatumia ujumbe wa sauti wapiganaji wake akiwataka kutosalimu amri
dhidi ya majeshi ya serikali. Kiongozi huyo amesikika akisema "hakuna
kusalimu amri" na kuwaambia wapiganaji kwamba ni heshima kuilinda ardhi
hiyo kuliko kusalimu amri kwa aibu. Huo ni ujumbe wa kwanza kutolewa na
kiongozi katika kipindi cha mwaka mmoja na kumekuwa na tetesi juu ya
afya na harakati za kiongozi huyo lakini hajulikani alipo. Mwezi Juni
mwaka 2014, alijitokeza hadharani mjini Mosul na kutangaza Dola la
Kiislamu nchini Iraq na Syria. Muungano wa kijeshi unaoongozwa na
Marekani na unaovinga mkono vikosi vya Iraq, unakadiria kuwepo kiasi ya
wapiganaji 3000 hadi 5000 wa IS ndani ya mji wa Mosul.
Wikileaks yachapisha barua pepe mpya kuhusu Clinton
Mtandao wa Wikileaks umechapisha barua pepe mpya kutoka kwa mkuu wa timu
ya kampeni ya Hillary Clinton, John Podesta. Barua pepe hizo
zinaonyesha wizara ya mambo ya nje ikimueleza Clinton juu ya ripoti
inayohusu taarifa za matumizi ya barua pepe binafsi. Katika taarifa
zilizoko ndani ya barua pepe za Clinton, kunaonekana kuwepo na uratibu
wa karibu kati ya wizara na timu ya kampeni ya Hillary Clinton na
zinapendekeza kwamba huenda afisa wa serikali alimdokeza Bi. Clinton
kuwa taarifa zake za matumizi ya barua pepe binafsi ziko karibu
kujulikana. Timu ya kampeni ya Clinton inaishutumu Wikileaks kwa kutumia
taarifa zilizodukuliwa na Urusi katika jitihada za kuingilia uchaguzi
wa nchi hiyo. Wagombea wote wawili Donald Trump wa Republican na Hillary
Clinton wa Democrats wameendelea kutupiana vijembe katika kampeni za
lala salama kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)