Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 25 Agosti 2015

Beverly Kelso-The Wailer asili




Alizaliwa 1948
Kingston Jamaica
Mtindo ska
Miaka aliyofanya kazi 1963-1965
Lebo Studio one
Beverly Kelso

Akishirikiana na The wailers
          Jambo moja linalojulikana kimakosa na wengi wa mashabiki na wapenzi wa muziki wa reggae, kuna Wailer asili mmoja tu aliyehai (aliyebaki) lakini hiyo si kweli.Na wailer mwenyewe anatatubulika kama Neville O’riley Livingstone. Anajulikana vizurI kama Bunny Wailer lakini Beverly kelso ni msingi na jiwe kuu la pembeni la The Wailers bado  anaishi. Anaishi Brooklyn,New York.
          Alizaliwa Kingston Jamaica mnamo mwaka 1948 na alisoma shule ya Nembhard Pre na baadaye Denham Town Primary School, Kingston
          Ingawa hatajwitajwi sana lakini ana mchango mkubwa sana katika kujenga msingi imara uliowafanya Bob Marley na The Wailers kuwa maarufu duniani.Akihusika kwa namna nyingi katika Maendeleo ya kundi
          Uwezo wa kelso unaweza kuupata katika nyimbo alizoshiriki kuitikia (backing vocal ) na kusaidia kutia mvuto. Baadhi ya nyimbo alizoshiriki ni Simmer Down, It hurts to be alone na Lonesome feeling.
          Ilikuwa jumatatu angavu jioni mwishoni mwa mwaka 1963 ambapo vijana watano chini ya miaka ishirini (20) Robert Nesta Marley, Neville livingstone, Winstone Hubert Macintosh, Junior Brathwaite na msichana pekee katika kundi Beverly kelso waliingia katika mlango wa nyumba namba 13 Brentford road Kingston 5 (baadaye ilijulikana kama Studio One ) kwa
 matumaini ya kutengeneza historia katika muziki, walikuwa na nyimbo nne,Simmer Down, Idon’t need you love, How many times na Straight and narrow way, sauti ya Kelso ikisikika katika kila wimbo.Kwa msaada wa sauti za nyimbo waliupata kutoka bendi ya skatalites, The Wailers wakafanikiwa kutoa wimbo wa Simmer Down ambao ulipata umaarufu mwanzoni mwa mwaka 1964 na kushika chati namba moja kwa wiki kadhaa.
             Sauti nzuri ya juu ya Kelso ikitikia (Background Vocals) ikitoa mlingano mzuri kwenye kundi,ikaacha athali  chanya na kulifanya kundi liifanye alama ya sauti ya kundi.
  1.             Bob Marley,Bunny Wailer,Beverly Kelso na Peter Tossh
  Kuondoka kwa Brathwate ambaye sauti yake ilifanana na sauti ya Kelso na kuonatoka kwa mwanakundi mwingine wa muda mrefu Cherry Smith (huya hakuwa amezama sana kwenye kundi ) kulilifanya kundi lijikutelimebaki  na watu watatu.
              Sauti ya juu ya Kelso inasikika vizuri zaidi kwenye nyimbo za Simmer Down na Lonesome feeling baadaye alitoa mchango mkubwa katika kuingiza matumiziya kinanda cha upepo (Pumping Organ) msaada ukiupata katika bendi ya Viking, kinanda hicho unaweza kukisikia katika nyimbo nyingine kama Cyrus na there‘s A Reward za Joe Higgs na Roy Wilson.
             Akizungumza kutoka New York yaliko makazi yake, anasema alirekodi nyimbo ishrini na tano (25) na kundi kabla hajaondoka mwishoni mwa mwaka 1965 ukiwemo mmoja ulio na jina Let the lord be seen in you. Kuondoka  kwake kuliliacha kundi pweke. Walikwenda mbali zaidi na kumtungia wimbo ilioitwa Donna.
           
Robert Nesta Marley na Rita Anderson


Akizungumza katika Tribute to the Great mwaka 2012, alisema kulikuwa na mjadala mkubwa katika kundi kuhusu masuala yanayohusu mwelekeo wa kundi lililokuwa linakuwa kwa kasi pamoja na jitihada kubwa zilifanyika kujaribu kumshawishi abadili mawazo yake ya kuondoka.
            Kulingana na maelezo yake alibaki akiheshimiwa kukubaliwa na wengi kila kuthaminiwa na wengi kila kundi lilipohusika.
           Wakati Marley anamuoa Rita Anderson, February 10, 1966, Kelso ni mtu pekee katika kundi aliyekuwa najua. Aliyasema hayo wakati wa mahojiana na Colby Graham, mhariri wa jarida la Vintage Boss.
           Kelso alikuwa ufunguo muhimu tena katika kundi la The Wailers pale alipomtambulisha Rita Anderson kwa Clement “Coxson“Dodd. Ushirikiano huo sio tu ulimwingiza Rita katika biashara ya muziki bali pia ulifungua milango ya mahusiano na Bob Marley.Unaweza kusema,bila kujua alinzisha ujenzi wa himaya ya Marley . kwenye nahojiano ya mwaka 2004 mjini New York na jarida la Vintage Boss kelso alieleza.
          “Wakati tunaenda  Studio kutoka Trench Town mara kwa mara tulipita njia ya mkato kupitia Ninth Street na makaburi ya Calvary tukipita nyumbani kwa akina Rita. Mara nying alikuwa na mtoto mikononi, na mara nyingi akitupungia mkono. Wengine walimpuuza lakini kama mwanamke nilijisikia vibaya nikawasimamisha, hawakupenda, siku moja mchana akaniambia ana wimbo aliouita “Opportunity” anataka kurekodi, nilimweleza  bwana Dodd na akasema nimlete.nilimfuata lakini hakuwa amejiandaa.Mpaka awatafute waitikiaji wake (Backing Singers) mmoja tulimwita Dream na mwingine tulimwita Precious, wakipita Soulettes, walarekodi kesho yake” kelso alisema.
           Kelso anaishi Marekani tangu dec 27, 1979 na aliachana na muziki tangu enzi za Studio One. Ingawa akirudisha nyuma kumbukumbu nzuri za familia yake ya The Wailers.zinazoishi, anaona The Wailers ni taasisi bora ya muziki uliopendwa zaidi katika historia ya muziki wa Jamaica.
           Mwaka 2012 alisema anapanga kuandika kitabu kuhusu maisha yake na The Wailers.Kurudi kwake na kuandika kitabu huenda isiwe karata ya mwisho ya Kelso,upande wa muziki simmer down huenda ndiyo itakayomfanya akumbukwe kwayo.
           Labda sauti ya mwanzo ya vijana wadogo katika muziki maarufu ilisikika ikionya:
Chicken merry, hawk de dear
and when I’m de near you must be aware.
So simmer down, Control your temper
Cause the battle will be hotter
Nyimbo alizoshiriki
Simmer Down
The wailing wailers -1963
Ganja gun
I’m still waiting
The wailing waiters -1965
Rasta
Rude boy

The wailing wailers -1965
Ska jerk
The wailing wailers -1965

Hakuna maoni: