Tafuta katika Blogu Hii
Jumatano, 2 Machi 2016
PONSIO PILATO
PONSIO PILATO
Kuzaliwa Haijulikani
Italian, Roman Empire
Kufariki C. 37 AD
Italian, Roman Empire
Nafasi yake – Gavan wa Roma Yudea
Alikuwa ni kiongozi wa utawala Roma katika Yudea kuanzia 26-36 AD. Alikuwa chini ya mfalme Tiberius Na anajulikana sana kutoka kwenye maandiko ya Biblia wakati wa kesi na kusurubiwa kwa Yesu.
Vyanzo vya habari ya maisha ya Pilato, ni jiwe linalojulikana kama Pilato Stone, inayoonyesha historia yake kama kiongozi (Prefect), maelezo mafupi yalioandikwa kwa Tacitus, Philo wa Alexandria, Josephus, Injiri nne, kitabu cha Nicodemus, Kitabu cha Marcion Na maandiko mengine ya wakati huo.
Kupitia kwa vyanzo hivyo Pilato alimfuatia Valerius Gratus kama kiongozi wa Yudea mwaka 26 AD. Philo anasema mwanzo alizuia taratibu na mambo yote yanayohusu maswala ya dini, hiyo ilipelekea matatizo kwa watu wa Yudea.
Na Josephus alindika yanayofanana na haya 93 AD. Pilato akaariwa arudi Roma baada ya kulipuka kwa maasi makubwa yaliyotokea baada ya kifo cha Tiberius kilichotekea 16 March 37 AD. Nafasi yake ikazibwa na Marcellus.
Katika injili zote nne, Pilato alijaribu kufanya ushawishi ili Yesu aachiwe na kushindikana pale umati ulipokataa kumwachia. Akaanza namna ya kuepuka binafsi kuhusika na kifo cha Yesu, kwenye injili ya Mathayo. Pilato alinawa mikono kuonyesha hausiki na hukumu iliyopelekea kifo cha Yesu.
Injili ya Marko inamtambulisha Yesu asiye na hatia dhidi ya utawala wa Warumi, inamwonyesha Pilato hakutaka kumuua Yesu. Injili ya Luka Pilato sio tu hakubali kuwa Yesu hakuvunja sheria yoyote juu ya matendo ya Yesu. Katika injili ya Yohana, Pilato anasema “Sioni kosa juu ya mtu huyu(Yesu) na akawauliza wayahudi kwenye baraza kama Yesu aachiwe.
Kwa miaka mingi wanazuoni walivutana kuhusu namna ya kumuelezea Pilato. Alama zilizopo kwenye jiwe la Pilato, uvumbuzi uliofanyika mwaka 1961 hayo majina Pontius Pilate ni sawa na yale yaliyokuwa yanazungumzwa na wanazuoni.
Limestone block. Jiwe lilifumbuliwa mwaka 1961. Maneno [………] TIVS PILATVS [……….] tanayoonekana vizuri mstari wa pili.
Ushahidi pekee wa kitu kilichotokana na utafiti wa mambo ya kale kinachodhitibisha kuwepo duniani kwa mtu aliyeitwa Pilato. Maelezo ya lilatini yalikutwa juu ya jiwe yakionyesha utii wa Pilato kwa Tiberius. Uvumbuzi huo wakati mwingine unajulikana kama jiwe la Pilato , uligunduliwa mwaka 1961 na timu ya watafiti wakiongozwa na Antonio Frova. Lilipatikana kama tofari lilolotumika (reused) katika ngazi zilizokuwa na umbo la nusu duara nyuma ya nyumba ya Roman Theater Kaisaria jiji lilotumika kama sehemu ya utawala wa Roma kwenye jimbo la Yudea. Magavana wa warumi walipendekea Kaisaria na walikwenda Jerusalemu pale tu walipokuwa na sababu maalum au nyakati za mapumziko.
Maelezo juu ya jiwe yanaonyesha la msingi yanaonyesha ni maelezo ya ujenzi wa jengo, huenda ni hekalu lililokuwa linajengwa, huenda heshima ya Mfalme Tiberius miaka ya 26-36 AD. Ujumbe unasomeka kuwa Pilato kiongozi wa Yudea Pracfectus Iudacae. Magavana wa mwanzo wa Yudea walikuwa na cheo cha Prefect baadaye wakaitwa Proculator, wakianzia na Caspius Fadus mwaka 44 AD. Jiwe hilo lilivumbuliwa limehifadhiwa katika jumba la makumbusho la Islael Museum Jerusalem.
CHEO NA KAZI
Kiasili Ponsio alikuwa na cheo cha Procutor, Hivyo ndivyo Tacitus anavyomuelezea. Ingawa maandishi juu ya jiwe (limestone block) yanayojulikana kama jiwe la Pilato. Kwa heshima ya Tiberius Caesar August- lililogunduliwa mwaka 1961 Kaisaria linamtambulisha kama Kiongozi (Prefect) wa Yudea.
Cheo cha Gavana wa wa jimbo kilikuwa kinatofautiana kwa majina kwa vipindi tofauti. Wakati Somaria yenyewe Yudea na Idumea zilipokuwa chini ya mmoja wa Roman jimbo la Yudea kuanzia mwaka 6 AD mpaka yalipolipuka maasi ya kwanza ya Wayahudi mwaka 66, kiofisi zilitumika amri za Equestrian (Order) (Equesrian cheo cha ngazi ya chini ya Gavana. Walitumia cheo cha kiongozi (Prefect) mpaka Herode Agrippa 1 alipoitwa Mfalme wa wa Wayahudi mwaka 41 AD na Ctaudius. Baada ya kifo cha Herode Agrippa 1 mwaka 44. Yudea ikawekwa chini ya utawala wa moja kwa moja tokea Roma, Magavana wakaanza kuitwa Procuter. Kilipoanza kutumika cheo cha gavana na neno procuter lilitumika kwa maofisa wa maswala ya kifedha, na hakikuwa na tofauti ya cheo wala wala kazi zake na cheo kilichoitwa kiongozi (prefect). Uvumbuzi wa utafiti wa mambo ya kale na baadhi ya nyaraka zilizopatikana kaisaria inaonyesha kuwa Gavana wa eneo la wakati huo aliitwa kwa cheo cha Prefect (Kiongozi) mpaka mwaka 41 AD.
Kwahiyo maandishi yanayomtambua Pilato kama Procutor yanaanzia wakati wa Tacitus au hayakuwa kabla ya mwaka 44 AD.
Kimsingi hawa maprocutor na viongozi (prefect) walikuwa wanajeshi, kwa kuwa waliwakilisha Himaya ya Roma walihusika pia na kukusanya Kodi na pia ilikuwa na mamlaka kubwa ya Kimahakama. Na shughuli nyingine za kiraia ziliachwa mikononi mwa Serikali za maeneo husika, Mfano katika wilaya ya Yudea na Jerusalemu- ziliachwa kwa Makuhani na kiongozi wao ni Kuhani mkuu. Lakini Kuhani mkuu alichaguliwa na Mamlaka za Roma zililzokuwepo Suria au akichaguliwa na Kiongozi (prefect) wa Yudea wakati wa Pilato mpaka mwaka 41 AD. Kwa mfano Kayafa alichaguliwa kwa Kuhani Mkuu wa Hekalu la Helode na Kiongozi Valerius Gratus na akaidhinishwa na Mamlaka za Suria zikiongozwa na Lucius Vitellius. Kwa kawaida Pilato alikaa kaisaria lakini alisafiri eneo lake lote la kazi , hususani Jerusalem kutimiza majukumu yake ya kazi. Wakati wa Pasaka alama kubwa ya kidini ya Wayahudi. Sherehe kubwa za Kitaifa zilifanyika. Pilato kama Gavana au Kiongozi alitarajiwa kuwa Jerusalem kuhakikisha hali ya usalama. Hakwenda kushiriki ibada wala hakujionyesha mbele ya waumini sababu Wayahudi walichukia sana kufanywa sehemu ya jimbo la Roma.
Kwa cheo chake alikuwa na mamlaka ya vikosi vidogo vya jeshi vilikuwa chini ya utawala wake. Na ilipohitajika nguvu kubwa ya jeshi alipaswa aombe kutoka mamlaka zilizokuwa Syria, ambayo ingeingizwa Palestina na maeneo yake kadiri iwezekanavyo. Kama Gavana wa Yurea Pilato alikuwa na askari wachache waliokuwa Kaisaria na Jerusalem. Jumla ya askari waliokwepo wanakadiriwa kuwa 3000 kwa idadi.
Nyakati za Karne ya nne zinaitwa Matendo ya Pilato zinajieleza katika utangulizi kuwa zilipokelewa Kiofisi katika Praetonium katika Jerusalem. Nyaraka hizo zimetambulika kama Injili ya Nikodemu.
Nyaraka hizo zinazungumzia kwa upana matukio ya kipindi cha miaka ya kati.
Imezingatia zaidi matukio yaliyozunguka tukio la kusulubiwa ambayo yamesanywa pamoja na kuitwa Karamu. Sasa imetafsiriwa kwa lugha nyingi ambazo zimehaririwa kwa lugha mbalimbali. Kigiriki, Kikoptik, America na matoleo ya Kilatini. Matoleo ya Kilatini yalichapishwa mara kadha katika karne ya 15 na 16.
Moja kati ya matoleo ya kilatini mwisho wa kitabu yanazungumzia maajabu ya Veronika.
Matendo ya Pilato imegawanyika katika sehemu tatu ambazo aina ya uandishi wake ambao unaoneshwa umeandikwa na waandishi watatu walioandika nyakati tatu tofauti.
Sehemu ya kwanza (1-11) inazungumzia mambo mengi yaliyotokea katika kesi ya Yesu, ikiegemea Luka 23.
Sehemu ya pili (12-16) inazungumzia ufufuko wa Yesu.
Appendix: Inaelezea maajabu ya “Harrowing of Hell” Hii imeelezwa kwa Kilatini na imetafsiriwa kwa lugha nyingi za Ulaya. Haipatikani katika matoleoya Kimashariki, Syria na Armerican, ambayo yanapatikana moja kwa moja kwa kigiriki.
Ndani yake Leucius na Charinus, walifufuka katika wafu baada ya kusulubiwa na kufa kwa makuhani tukio la Yesu lilifanana sana na tukio la Limbo (Kisa cha Leucius na Charinus).
Eusebius (325) pia anayazungumzia Matendo ya Pilato kama alivyonukuliwa na Justin na Tertullian na waandishi mbalimbali wa wakati huo. Maandiko ya katikati ya karne ya nne, Epiphanius anaelezea matendo ya Pilato naye alieleza hivyo mwanzoni mwa mwaka 376 AD lakini hakuna muonekano kuwa toleo la kwanza la Kigiriki, toleo la mwanzo ni marudio la toleo halisi Justin- Katika nyaraka.
Apology of Justin anasema “Mambo haya yanavyotokea unaweza kufananisha na Ponsio pilato”
Nyaraka ziliandikwa kwa Mfalme wa Roma Pius.
Gavana Urbicus watu wote hawa watatu waliishi mwaka 138-161.
Kuna maandiko yanayoripoti kuhusu kusulubiwa, yanaaminika yaliandikwa na Ponsio Pilato akimwandikia Mfalme (Ladius) juu ya kichwa cha habari Matendo ya Petro na Paul (Act of
Peter and Paul) ambayo yanatajwa kuwa Uandishi unaoeleweka na wa Kitume, ingawa haukutegemea, mfupi na umekamilika. Hakuna uhusiano kati ya hizi nyaraka mbili zilizoandikwa katika karne ya 4 na Matendo ya Pilato.
Ripoti ya Pilato inaingizwa katika kundi moja na waraka wa karamu ya Petro na Paul yote yanapatikana katika matoleo ya Kigiriki na Kilatini.
Kifo cha Pilato
Maajabu katika tamaduni za Kilatini, watawala walimuona kama mzimu na sio Mtakatifu, inaelezwa katika Kitabu Nikodemu toleo la Kigiriki. (Asili ya maandiko yake) Kifo cha Pilato kilitokea wakati Mfalme Tiberius anaumwa, akamtuma Volusanius kwenda Yudea kumtafuta Yesu kwaajili ya kumponya. Alipofka Yudea akakutana na Pilato ambaye alimficha ukweli kuwa Yesu alisulubiwa akakaa Yudea kwa siku kadhaa. Lakini Volusanius kwenda Yudea akakutana na Veronika ambaye alimweleza ukweli kuhusu kilichotokea na akampa kiytambaa chake chenye picha ya sura ya Yesu ambacho akarudi nacho Roma.
Tiberius akapona.
Tiberius akamwita Pilato arudi Roma. Inasemekana alipotokea alikuwa amevaa alama ya aMsalaba, ambayo ilionekana baada ya Pilato kuvua mavazi zake, Ikatolewa amri auawe ,akajiua mwenyewe. Mwili wake ukatupwa Tiber (Mto) ambapo ulisukumwa na maji mpaka Vienne (Via gehemae) Ufaransa hapo pia ulisukumwa mpaka Rhone, hapo bado ukaelekea upande wa mashariki mpaka “Losania” ambapo ulikwama karibu na Lucerne, karibu na Pilatus- asili yake ni Mons Pileaus au “Cloud- Capped”, Kama John Roskin anavyoonyesha kwenye mchoro ambacho kuna mahujaji wanaoenda kuhiji hapo kila ijumaa kuu na kunawa mikono yao.
Toleo lingine la kipekee kuhusiana na kifo cha Pilato ni waraka wa Antoine la sale alilipoti akiwa safarini katikati ya Halia ya kuwa baada ya kifo cha Pilato mwili wake ulisukumwa na maji mpaka kwenye ziwa dogo karibu na Vettone Peak (2478m) Katika milima ya Sibillini na ukakwama hapo. Siku hizi ziwa hilo linaitwa Lago di Pilato.
Veneration
Kanisa la Othodox lilimtangaza Pilato Mtakatifu karne ya sita. Ikizingatia zaidi Matendo ya Pilato na mkewe Claudia Procula ambaye aliota ndoto kuhusu na kujaribu kumshawishi Pilato (mumewe) asimsulubu Yesu. Kwahiyo limetenga tarehe 25 june kwaajili ya Mtakatifu Pilato na mkewe Claudia. Na kanisa la Kigiriki wameiteua tarehe 27 Octoba kuwa ni siku ya Mtakatifu Pilato.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni