Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 18 Machi 2016

Korea Kaskazini yajaribu makombora

Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa ya kati, siku chache tu baada ya kiongozi wake Kim Jong-Un kuahidi kufanya majaribio kadhaa ya silaha za nyuklia na makombora, wakati ambapo mvutano wa kijeshi ukizidi. Msuguano kati ya Korea mbili zilizogawika umeongezeka tangu Korea Kaskazini ilipofanya jaribio lake la nne la nyuklia Januari 6, na kufuatiwa mwezi mmoja baadaye na ufyatuaji wa roketi ambao ulichukuliwa na wengi kama kificho cha jaribio la kombora la masafa marefu. Maafisa wa Marekani wamesema walifuatilia ufyatuaji wa makombora mawili ya Rodong -- yanayoaminika kuwa ya masafa ya kati kutokea kwenye magari. Kombora la Rodong lina uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 1,300.

Hakuna maoni: