Ni kitabu
ambacho wakristo wengi hawajapata kukisikia au kukiona.
Ni kitabu
chenye sura 222, ambacho kilionekana kwa mara ya kwanza mwaka 1709 nchini
Uholanzi, na mwaka 1738, Kilipelekwa Vienna Austria kwenye maktaba kuu ambako
kimehifadhiwa mpaka leo.
Kimeandikwa
kwa lugha ya Kiitaliano sehemu za chini ya kurasa zake yameandikwa maneno kadha
wa kadha kwa kiarabu.
Mwaka 1907 ilitolewa tafsiri ya kitabu kizima kwa lugha ya
kiarabu kufuatia rai ya Seyyid Muhammad Rashid Ridha. Aliyetafsiri ni Dk Khalid
sa’adah.
Pia
kimetafsiriwa katika lugha nyingine tofauti tofauti ikiwa pamoja na kiingereza.
Upo utatanishi
mkubwa kuhusu mtu aliyekiandika kitabu
hicho, upande ukidai mwandishi ni Barnaba yule kutoka Kipro (Cyprus) ambayo
Luka aliandika habari zake akimwita Mtume, Nabii tena Mwalimu mtu mwema
aliyejaa Roho Mtakatifu na imani (Matendo 14:4,14, 13:1 na 11:24). Inadaiwa
kitabu hiki kiliibwa na mtawa mmoja aliyeitwa Fra Marino kutoka Vatican wakati
wa Papa Sixtus (1589-1590) na kwamba awali kilitambulika kama injili harisi na
kilitumika katika makanisa ya Alexandria hadi mwaka wa 325 baada ya Masihi. Kwa
upande mwingine imeelezwa kwamba kwa vile katika sehemu zote zilizonukuu Torati
katika kitabu hicho yametumiwa maneno yafananayo kabisa na yale yaliyotumika
katika Biblia tafsiri ya Vulgata iliyoandikwa mwaka 380 baada ya Masihi, ni
dhahiri mwandishi wake sio Barnaba. Pia umefanywa uchunguzi wa kisayansi juu ya
karatasi ya mwandiko wa kitabu hicho na imethibitishwa kwamba kiliandikwa baada
ya mwaka 1500. Inaaminika mwandishi wa kitabu hicho ni Mhispania mmoja
aliyeitwa Mustafa.
Tokea mwaka
1907 kilipotafsiriwa kitabu hicho katika lugha ya Kiarabu baadhi ya watu
wamekuwa wakizungumzia na kudai kuwa kitabu hicho ndiyo inili pekee yake iliyo
sahihi. Kukubaliwa na injili hiyo ya Barnaba bila shaka kunahusiana na kutajwa
kwa Ismail katika sura ya 44 kuwa ndiye aliyekaribia katika kutolewa sadaka na
babaye Ibrahimu, na siyo Isaka kama isemmavyo Biblia.
Kivutio
kingine katika kitabu hicho ni sura ya 212 inayoonesha Yesu akihofia
kubadilishwa kwa injili, na sura ya 222 inayozungumzia watu iwaitao waovu
walioeneza habari za kufa kwa Yesu Msalabani na kusema alikuwa mwana wa Mungu.
Katika sura hiyo anatajwa Paulo kuwa ndiye aliyepotosha ukweli.
Ubatili wa
injili ya Barnaba unaonekana ndani ya kitabu hicho hicho kimehitilafiana sana
na vitabu vilivyoandikwa na wanafunzi wa Yesu kama vile Mathayo, Yohana, Petro,
Yakobo na Yuda. Imeeleza kwa mfano katika sura katika sura ya kwanza ya kitabu
hicho kwamba Barnaba alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu. Lakini Barnaba ni mtu
aliyefahamika kwa undani kwamba alikuwa binamu wa Marko, na kwamba aliingia
katika ufuasi wa Yesu baada ya Pentecoste, ambayo ilikuwa ni siku ya hamsini
baada ya kufufuka kwa Yesu. Barnaba hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Hata jina la
Barnaba alipewa na Petro na wenzake likiwa na maana ya “Mwana wa faraja”
(Matendo 4:36, 37) Kabla ya hapo alifahamika kwa jina la Yusuph.
Kuhitilafiana
kwingine kwa injili ya Barnaba na vitabu vya Mathayo, Marko, Luka na Yohana ni
katika maelezo ya sura ya 92, yesemayo Barnaba akiwa pamoja na Yesu waliamriwa
na Malaika Mtakatifu waende kwenye mlima Sinai na kukaa huko siku arobaini.
Lakini inafahamika kwamba tokea alipowachagua wanafunzi wakae
hadi alipopaa Yesu alikuwa ndani ya nchi ya Parestina tu, sio nje ya hapo
(Mlima Sinai upo nchini Misri).
Kutokufahamika
huko kwa Jiografia ya Palestina na mwandishi wa kitabu cha injili ya Barnaba kunajidhihilisha zaidi katika sura
ya 20 inavyoeleza jinsi Barnaba alivyosafiri na Yesu katika mashua kwenye
bahari ya Galilaya hadi kwenye mji wa Nazareti. Hili ni jambo lisilowezekana,
Nazaleti iko Kilometa zaidi ya 60 kuyoka
bahari ya Galilaya. Pia katika sura ya 63 mji wa Ninawi ulioko Al Kishr kwenye
mto wa Tigris umeelezewa kuwa ukingoni mwa bahari ya kati ( Mediteranea).
Jambo linguine
linalochanganya ni kuhusu majira. Sura ya 92:10 inaonyesha Yesu aliishi wakati
mmoja na Muhammad, na kwamba Yesualifurahi alipomuona Muhammad akasema
“ijapokuwa mimi sistahili kufungua gidamu za viatu (vya Muhammad), lakini
nmepata rehema na rehema”. Pia ubatili wa injili ya Barnaba inajionysha sura ya
51:4-20 ambapo Mwenyezi Mungu ameelezewa
jinsi alivyofanya maelewano mazuri kabisa na ibilisi.
Ni wazi
kabisa yeyote asemaye injili ya Barnaba
ndiyo sahihi hajasoma kitabu hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni