Angalia mazoea yanayoambatana na krismasi nini mti wa kijani kibichi (mti krimas) siku hizi ya plastiki, ukumbi,mapambo, pamba, mzee mwenye ndevu nyeupe na kofia yenye kishungi na mstari mweupe na suti nyekundu,taa(disco lights) maua ya plastiki,kigogo cha mti kinachoonekana kiini chake,mnyama pori mwenye pembe kama mti na tololi yana maana yeyote na kuzaliwa kwa Yesu?
Yote haya hayana uhusiano naye lakini yana mambo
mengi ya kufanya kwenye matamasha ya kipangani. Lini hasa Yesu alizaliwa?
Alizaliwa siku ya tarehe 25 disemba?
Ukichunguza kwa umakini maandiko, kwa vyovyote, kwa uhakika inaonyesha kuwa tarehe 25 disemba haiwezi kuwa siku ya kuzaliwa Yesu. Hizi ni sababu.
Kwanza tunaona kuwa
wachungaji walikuwa kondeni wanachunga
mifugo yao wakati Yesu anazaliwa (Luka 2:7-8) wachungaji hawakwenda kondeni
wakati wa mwezi wa kumi na mbili (disemmba),Kulingana na sherehe katika kitabu cha"The complete book of American holydays "mwandishi anasema...
" kulingana na maelezo ya Luka inaonekana Yesu anaweza kuwa alizaliwa kiangazi au mwanzoni mwa kipindi cha mchipuko (falls) . Kwa kuwa disemba kuna baridi kali na mvua katika Yudea ni wazi wachungaji wangetafuta hifadhi ya mifugo yao wakati wa usiku. ( Uk. 309)
" kulingana na maelezo ya Luka inaonekana Yesu anaweza kuwa alizaliwa kiangazi au mwanzoni mwa kipindi cha mchipuko (falls) . Kwa kuwa disemba kuna baridi kali na mvua katika Yudea ni wazi wachungaji wangetafuta hifadhi ya mifugo yao wakati wa usiku. ( Uk. 309)
Pia the enterpreater’s One-volume commentary anasema
kuwa aya hiyo
inapinga kuzaliwa ( kwa Yesu) disemba 25 kuwa hali ya hewa haikuruhusu” wachungaji
kuchunga mifugo yao wakati wa usiku .
Pili wazazi wa Yesu walikwenda Bethlehem kujisajili
katika sensa ya Warumi (Luka 2:1-4)sensa kama hizo hazikufanyika wakati wa
baridi ambapo joto lilishuka chini ya kiwango cha kuganda na njia zilikuwa katika hali mbaya, sensa
kwenye hali ya hewa kama hiyo ilikuwa ni sawa na kujishambulia.
Ilikuwa vigumu kuwaingiza wapangani katika ukristu
ukweli muhimu unaotakiwa kuelea vizuri kichwani mwako ni kuwa kuifanya siku ya
tarehe 25 Disemba ilikuwa ni makubaliano na wapagani (William Warsh. The story
of Santa Klaus 1970 uk.62)
Kama
Yesu hakuzaliwa tarehe 25 Disemba, biblia inaonyesha lini?
Maandiko ya kibiblia yana onyesha wakati wa majira ya mchipuo (falls) ya
mwaka kuwa ndiyo uwezekano zaidi wa Yesu kuzaliwa kipindi hicho ukiegemea
kwenye hoja ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji.
Elizabeti (mama yake Yohana Mbatizaji. ) alikuwa na
ujauzito wa miezi sita wakati taarifa ya Yesu ilipotolewa (Luka 1:24-36)tunaweza
kukadiria wakati wa mwaka Yesu
aliozalilwa kama tunaweza kuja wakati aliozaliwa Yohana . baba yake Yohana, Zakaria
alikuwa kuhani akihudumu katika hekalu la Jerusalemu wakati wa abiya (Luka
1:5)Historia inaonyesha kuwa hii ilifanyika mwezi wa sita (juni 13 -19) kwa
mwaka huo.The campannion bible, 1974, appendix 179. Uk 200)
Wakati huu wa huduma ya hekalu ndipo Zakaria alipo
pata habari kuwa yeye na mkewe Elizabeti watapata mwana.
(Luka 1:8-13) baada ya kumaliza zamu yake akarudi
nyumbani Elizabeth akapata ujauzito (Luka 1:23-24)
Kadiria kuwa tukio la Yohana lilitokea karibu na
mwishoni mwa mwezi wa sita jumlisha miezi tisa inatupeleka mwishoni mwa mwezi
wa tatu ambapo ndipo uwezekano mkubwa ndipo alipozaliwa Yohana jumlisha miezi sita (tofauti ya umri wa kati
ya Yohana na Yesu (1:35-36)
Ingawa ni vigmu kuipata kwa mara ya kwanza yeyote
aliyesherehekea Disemba kama siku ya kuzaliwa Yesu wanahistoria
wanakubaliana kuwa hiyo ililkuwa wakati wa karne ya nne. Hii inashangaza ni
tarehe iliyo chelewa krismas hailusherehekewa Roma, mjimkuu wa himaya ya Warumi
mpaka miaka 300 baadaye, baada ya kifo cha Yesu. Haina asili katika mafundisho
wala matendo ya Wakristu wa mwanzo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni