![]() |
Alvin Patterson |
Alvin
“ Secco “ Patterson
Jina
kamili Fransisco Willie
Pia
anajulllukana kama
Alvin
“ Secco “ Patterson,Secco Pep ,Willie Pep
Alizaliwa
(1930-12-30)
Asili
– Kingston Jamaica
Mtindo
– Reggae
Mpigaji
wa percurssion
Vyombo
anavyopiga –percussion /bongo drum , conga, tambourine, cowbell, nk.
Mwaka
aliofanya kazi 1969 mpaka sasa
Alioshirikiana
nao
Bob
Marley & The Wailers,The Wailers
Alvin
“ Secco “ Patterson
Alizaliwa tarehe 30 Desemba 1930, Havana (Cuba) ni
mpiga percussion alikuwa mwanakundi wa The Wailers band
Alvin alikuwa
ni mpiga percussion katika Bob Marley and The Wailers na ni mmoja kati ya
marafiki wa karibu sana wa Bob Marley. Ingawa anajulikana kama “Secco”alizaliwa
akaitwa Fransisco Willie, Havana Cuba na baba mwenye asili ya Jamaica na mama Mpanama
akiitwa Cellestina Hardin. Alichagua jina la Alvin Patterson kama jina la
kisanaa na alipata jina la “Secco” kama kifupisho cha jina lake la Fransisco
alihamia Jamaica na wazazi wake waliishi Westmorland, ambako wazazi wake
walikuwa wanajishughulisha na kilimo baadaye akahamia Kingston na mama yake
baada ya wazazi wake kuachana, kama kijana Patterson alitafuta kazi katika
mgodi wa madini ya bauxite
Mwaka 1957 Patterson aliamua kuhamia Marekani
kutafuta kazi yenye kipato zaidi. Akiwa katika safari yake ajali mbaya ilitokea
ya treni ilitokea 1st September.
Mara moja Patterson alirudi kisiwani kuwatafuta ndugu zake aliohofia
wanaweza kuwemo kati ya watu 200 waliofariki au 700 waliojeruhiwa. Na wazo lake
la kuondoka likafutika ma akarudi jumla Kingston katika mgodi wa bauxite.
Ilikuwa kipindi hiki ndipo Patterson kwa mara ya
kwanza alipo kutana na Bob Marley akiwa
na miaka kumi na tano, mdogo kwa Patterson tofauti ya miaka kumi na tano na
waliishi wote eneo moja katika makazi duni ya
watu masikini Trech town. Marley alimwona Patterson sababu ya umaarufu
wake wa mchezo wa cricket, alikuwa na uwezo mkubwa wa kuucheza na akaanza
kumfuatilia Patterson mara kwa mara, akitafuta ujuzi wa criket na pia akivutiwa
na muonekano wa Alvin Patterson
Wakazama katika urafiki na Marley na wakabaki hivyo
mpaka mwisho wa maisha ya Marley. Patterson alimtia moyo Marley wakati anaanza kujaribu kuimba muziki,akiwa
Patterson mwenyewe alipata uzoefu katika muziki wa kupiga percussion kwa
mwanamuziki maarufu wa Calypso akiitwa Lord Flea na wapiaji wengine namna ya kupiga combo za kikalypso. Na alikuwa
ni Patterson kwanza aliyelichukua kundi la The Wailers. Likiwahusisha Marley,
pamoja na Peter Tosh na Bunny Wailer kulipeleka studio za Coxsson dodd kwa mara yao ya kwanza july 1963. Makubaliano yalifikiwa na The Wailers wakatoa muziki uliotikisa “simmer down” wimbo
uliomtambulisha Marley
Wakati wailers ikijitanua katika muziki Jamaica,Patterson
aliendelea kifanyakazi katika mgodi wa bauxite, mwaka 1966 wakati Marley akifanyakazi
Marekani, Patterson alijeruhiwa katika ajali iliyotokea katika mgodi, wakati
bomba la gasi iliyopita chini ya sakafu ya canteen ilipopasuka, ikasababisha
mlipuko ulioacha wafanyakazi wengi kujeruhiwa vibaya. Patterson alitupwa nje ya
jengo na akapoteza viatu katika tukio hilo wakati Marley aliporudi kisiwani wiki kadhaa baadaye
, alimshawishi Patterson kuachana na
kazi ya mgodini na aanze kujikita katika muziki matokeo yake Patterson akaanza
kuchangia percussion katika nyimbo zilizofuata za The Wailers mchango wake wa
kwanza unaojuikana ulikuwa juni 1967walipotoa “ lyrical satirycal” na this
train” ziliachiwa na the wailers zikihusisha wail n soul M label. Wakati
ushiriki wa Patterson katika Original Wailers (ikiwahusisha Tosh na Bunny)
ulikuwa mdogo, lakini mchango wake ulizidi kuongezrka. Wakati Original Wailers
walipokwenda ziara yao ya kwanza (pekee)uingereza
mwaka 1973. Patterson alishiriki kama mtu wa kipekee kwenye ubunifu wa kiasili(root)
Wakati ushirikiano wa Marley, Tosh na Bunny
ulipoisha Paterson akawa kiini cha kuihuisha bendi upya kwa maelezo ya Marley
na akashiriki kila rekodi na maonesho
yote ya jukwaani ambayo Marley alifanya kwa maisha yake yote, Patterson akazama
katika muziki na rekodi walizofanya
akibuni na kufanya muziki
uonekane wa kiasili.
Chupa ya maziwa katika “jamming” na muitikio wake
sauti ya percussion katika “crazy baldhead” ni miongoni mwa mifano bora kabisa
ya mitindo yake ya kufanya. Kitu rahisi kwa ubora wa juu. Ingawa hakutajwa
Patterson anaaminika aliandika baadhi ya nyimbo za marley ukijumlisha na
“work”.
Wakati wote wa maisha ya marlley Patterson alikuwa karibu yake. Mwaka 1976,Patterson alikuwa anafanya mazoezi na Marley akiwa barabara ya 56 Hope (road) ambapo mtu mwenye bunduki alimjeruhi Marley, pia walikuwepo mkewe Marley na meneja Don Taylor. Septemba 1980 Patterson alikuwa na Marley wakati alipopatwa shambulio la ugonjwa wakati anafanya mazoezi ya mbio (jigging) centra park na akabaki na Marley wakati wote wa matibabu yake ya kansa new York, marekani mpaka katika kliniki ya Dr Josef Issels.
Rottach-Egern, Ujerumani.
Kufuatia kifo cha Marley, Patterson aliendelea music
na The Wailers band . mwaka 1990 Patterson alipata shambulio la ubongo,
(haemorrhage) akiwa ziarani Brazil shambulio lililokaribia kupoteza maisha yake
alipopata nafuu akaachana na muziki wa jukwaani isipokuwa anaonekana tu katika
matamasha mbalimbali yanayomuhusisha Marley . Patterson sasa anaishi kingston.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni