Ethiopia inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka
50, huku shirika la Save the Children likitoa wito wa haraka wa
msaada wa chakula.
Shirika hilo limesema msaada huo utakuwa ni suluhisho la mda tu, na
viongozi wa dunia wanaokutana mjini Paris lazima wachukuea hatua juu ya
mabadiliko ya hali ya hewa.
Serikali ya Ethiopia inasema watu millioni 10 na laki moja
watakabiliwa na upungufu wa mkubwa wa chakula mwaka 2016, na zaidi ya
nusu ya hao ni watoto.
Kadhalika kuna watoto takriban laki 4 walio katika hatari ya kukumbwa
na utapia mlo mkubwa, hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa
ukuwaji na matatizo ya akili.
John Graham, mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini
Ethiopia, amesema mzozo wa mwaka huu ni matokeo ya mabadiliko ya hali ya
hewa.
Ukame mbaya unahusishwa na mfumo wa hali ya hewa ujulikanao kama El
Nino umeharibu misimu miwili mikuu ya mvua nchini humo mwaka huu na
kutokana na hilo mavuno yajayo hayatarajiwi kuja hadi mwezi Juni
mwakani.
Idara ya Umoja wa Mataifa ya Chakula na Kilimo (FAO) inakadiria kuwa
takriban aslimia 80 ya Waethiopia wanafanya kazi katika sekta ya
kilimo, na wengi wao ni wakulima wa wadogo wadogo ambao wanategemea mvua
kwa kilimo.
Hiyo ndio sababu taifa hilo linakumbwa na mizozo ya chakula mara kwa
mara na wakulima wanakosa njia na elimu ya kukabiliana na changamoto za
hali ya hewa.
Shirika la Save the Children linaomba msaada wa takriban dola
millioni 100 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa lakini limesema mwaka huu
majibu yamekuwa ya pole pole mno.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni