Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 11 Desemba 2015

Rais Magufuli atangaza baraza la mawaziri Tanzania

Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake jipya la mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lenye wizara 18 lakini litakuwa na mawaziri 

Katika mtiririko huo kuna baadhi ya wizara zitakuwa na waziri pekee bila ya kuwa na naibu waziri ambapo lengo kuu ni kutimiza ahadi ya kuwa na baraza dogo lenye kasi ya ufanyaji kazi  na kupunguza gharama za matumizi ya serikali yasiyo ya lazima.
Rais magufuli alisema baraza lake la mawaziri halitakuwa na semina elekezi na fedha zilizotengwa shilingi bilioni mbili kwa shughuli hiyo zitaelekezwa katika ufanyaji kazi mwingine wa kuboresha maendeleo ya wananchi kama vile madawati au kwenye utoaji wa elimu bure.
Wizara ya mambo ya njena EAC/Kimataifa
- Augustino Mahiga, Naibu Waziri - Dk. Suzan Kolimba
Wazara wa Utamaduni, Sanaa na michezo
Waziri-Nape Nnauye
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri -Sospeter Muhongo na Naibu Waziri-Medard Kalemani
Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri -Jenista Mhagama
Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala
mawaziri wawili - Simbachawene na Kairuki
Ofisi ya Makamu wa Rais/Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba Naibu waziri Luhaga Mpina.
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri ni Charles Kitwanga
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi
Waziri wake ni Wiliam Lukuvi Naibu Angelina Mabula.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Husein Mwinyi
Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri - Harrison Mwakyembe
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi
Waziri- Mwigulu Nchemba Naibu Waziri- William Tate Ole Nashon
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Waziri - Charles Mwijage
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalimu Naibu - Dk Hamis kigwangalla
Wizara ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi
Waziri - bado hajapatikana - Naibu Waziri -Stela manyanya
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri - bado hajapatikana na Naibu Waziri - Injinia Ramo Makani
Waziri wa Fedha na Mipango
Waziri - bado hajapatikana, Naibu Waziri - Dk. Ashantu Kijachi
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri - bado hajapatikana, Naibu Waziri -Edwin Ngonyani

Hakuna maoni: