Rider
Seventeeny
Jina
Peter Paschal Joseph
Kuzaliwa
Arusha
Mwanamziki
Mtindo
bongo flavor
Mwaka
alioanza 2004
Alizaliwa hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha na kuanza masomo
katika shule ya Msingi Kaloleni baada ya
mwaka mmoja wazaszi wake wakahamia Tanga ambako ni nyumba iliko mizizi
ya ukoo wake. Hapo akaanza tena darasa la kwanza katika shule ya msingi
St.Martin ambayo sasa inaitwa Magila wilayani Muheza mkoani Tanga huo ulikuwa mwaka 2000.
Hakukaa sana Tanga baba yake alipata uhamisho wa kazi na
kuelekea Dar es salaam hapo hakuwa na
hiari isipokuwa kukusanya virago vyake na kumfuata baba yake, kwa mara
nyingine tena akajikuta anaanza darasa
la kwanza katika shule ya msingi Vingunguti A iliyopo wilaya ya Ilala huo
ulikuwa mwaka 2001.
Kama kawaida ya vipaji vyote huanza kujitokeza umri mdogo akiwa shuleni akajikuta anapenda muziki na kutamani kuwa mwanamuziki mkubwa albam ya Dully sykes uluyokkwenda kwa jina la historia ya kweli ilikuwa na wimbo uliobeba jina la historia ya kweli. Kulikuwa na wimbo uliobeba jina la Salome huo ndio uliompagawisha Rider kwa kiwango cha kutosha kumfanya aukariri mashairi yake pamoja na nyimbo zingine ikiemo Monalisa.
Taratibu alijifunza kuimba na kufunga nyimbo pamoja na
kuigiza akishirikiana na baadhi ya wanafunzi wenzake waliokuwa na vipawa vinavyofanana.
Mwaka
2004 walianzisha kundi waliloliita Son cost, Rider akiwa kiongozi akishirikiana
na Yasco Taller pamoja na Bang'ala wa masoko.
Kundi liliendeshwa Kiugumu ugumu mpaka mwaka 2008 wlipofanikiwa kutoa wimbo ulioitwa Acha bifu
waliorekodiwa katika studio za Pamoja Records
kwa Nas B na kinanda kama solo artist. Studio zilikuwa kinondoni mkwajuni hapa
walitoa nyimba mbili.
Acha bifu ulionya wasanii wanajamii kuacha mivutano isiyo
na tija wala maana yoyote nyimbo hizo
hazikufanikiwa kuchezwa redioni. Mwaka 2009 ulikuwa mwaka mgumu kwa kila
manakundi. Wawili wliokuwa wana soma walijikita zaidi katika masomo na mmoja alikuwa anafanyakazi na
kukosa muda wa kufanya muziki kikamilifu. Hivyo kundi likafa kifo cha kawaida.
Akiwa anasoma Secondary ya Msongola hakuacha sanaa
imponyoke akageukia sanaa ya maigizo na kujikita katika uchezaji wa filam.
Akafanikiwa kupata nafasi katika kundi la Alwatani Theatre Group lililo kuwa na
maskani yake ilala likiongozwa na Haji Dilunga.
Akishiriki katika filamu ya Bunge la wachawi namba moja,
Bunge la wachawi namba mbili, Popobawa na Zindiko alipopata nafasi ya kuingiza
na Ahmed Ulotu (Mzee Chilo). Bada ya kumaliza kidato cha nne akarudi kwenye muziki.
Akaanzisha kundi linaloitwa La Ukoo Entertainment.
Kundi lilianza kama masihara, sasa limekuwa kubwa likIshirikisha
wasanii wa fani mbalimbali toka kona tofauti tofauti, wazo lilianzaia shuke
utekelezapo wake ulipoanza hakukuwa na kusimama hata baada ya kumaliza shule
wanebaki na La Ukoo Entertainment kundi likiwa na wachoraji, waigizaji Graphic
Designers, vinyozi, wacheza mpira wote pamja wanaitwa La Ukoo. Si kwa maana ya
watu wa asili ya sehemu moja la hasha isipokuwa Ukoo katika burudani ndipo wote
wanajumuika chini ya mwamvuli mmoja La Ukoo.
Kwa sapoti ya marafiki na La Ukoo akanza ktoa T-shirt
zenye nemo ya la ukoo Entertainment. Milango iko wazi na kundi linapokea yeyote
mwenye kipaji cha sanaa anayependa kujiunga 2012 alifanikiwa kutoa wimbo Nimedata
akiwa amemshirikisha jay maswagger kutoka kundi la republic. Millionare
lililokuwa chini ya marehemu Sharo
Millionere mwongozaji akiwa Dr. Babak na Big Josh imetengenezwa katika Studio
za Kany Records chini ya producer Man Lee”
hii pia haijapata kuchezwa redioni ila inapatikana youtube kwa jina rider
17 ft.Jay Maswagger
kama kawaida changamoto haikosekani popote hapa zinamkabili pia Rider
kwenye kazi yake ameonyesha kipaji akabuni wazo , na kulifanyIa kazi lakini
ukosefu wa pesa ni changamoto kubwa na
nzito kwake, kuikabili, pia msimamizi wa kazi zake pamoja na wadhamini bado
hajawapata hivyo kumuwia vigumu kurekodi na kuzifanyia promo kazi zake zichezwe
katika vituo vya radio na tv ziweze kuwafikia watu kwenda Studio kwa miguu ni changamoto
nyingine inayomkabili. Pia wapo watu wanaoshindwa kuthubutu kufanyia kazi
mawazo yao. Hawa wanatumia midomo na nguvu zao kumkatisha tamaa ya kutimiza
ndoto zake.Hivyo yeyote mwenye kutaka
kusukuma harakati hizi kwa michango ya hali na mali na mawazo mazuri milango
iko wazi na anakaribishwa.Yote kwa yote hachoki anakaza mkwiji na kusonga mbele
sasa anajiandaa kurekodi wimbo mpya na kutoa video yake wapenzi na mashabiki
wake watapata kazi zake kupitia mitandao ya kijamii kueni mkao wa kula.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni