Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 10 Oktoba 2015

IBADA YA HIJA




1.        Kuzuru msikiti  wa Mtume au kuweko Makka kufanya Umrah (kwa wanafanya Hajjut- Tamattu’u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul- Haraam.

               
Madina
      Kuswali Masjidun- Nabawiy (Msikiti wa Mfalme) na wanaume kuzuru kaburi la Mtume

                 Makka
     Kufanya Twawwaaf kuzunguka kaaba mara 7 kuswali mara 2 Maqaam Ibrahim Sayi

Swafaa na Marwah
    Kuanzia kilima cha Swafaa kwenda kilima cha Marwah mara saba. Wakimaliza Umrah watabakia Makka na kuswali katika Masjidul- Haraam

Mina
    Asubuhi wanaondoka Makka kuelekea Mina

Siku ya Arafah
         Wanaondoka katika mina asubuhi kuelekea Alafah na kubali hadi jua linapozama. Ni siku ya kutekeleza faradhi kubwa miongoni mwa taratibu za hija. Siku ya kuomba dua sana. Na ndivyo siku aliyosimama Mtume Muhammad (S,W) katika milima ya Arafah na kutoa hotuba yake ya mwisho.
          Hapa wataswali swala ya Adhuhuri na Alasiri janian wa Qwaswran (kujumuisha na kufupisha rakaa mbilimbili) watasiliza hotuba (watakaukuwa karibu na Masjidun- Namirah). Wasiokuwepo huko siku hiyo watafunga Swawm ya Arafah. Jua likizama wanaelekea Muzdalifah.

Muzdalifah- Mina- Makka
         Watafika Muzdalifah usiku na wataswali magharibi na Ishaa  ‘Jam’an kwa Quaswran ( kujumuisha na kufupisha Rakaa talu magharibi kawaida na kufupisha Rakaa mbili Ishaa) Watabaki Muzdalifa usiku mzima kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuokota vijiwe vya kurusha katika Jamaraat.
        Asubuhi- Yawmun- Nahr (siku ya kuchinja). Kwa mahujaji, na kwa wasiokuwepo huko ni siku ya iyd wataelekea kutekeleza vitendo vifuatavyo vya faradhi za Hija.
Kurusha vijiwe katika Jamraat, kutufu Twaaful – Ifaadh, kunyoa nywele na kuchinja ( vyovyote watakavyotanguliza katika vitendo hivi inajuzu) kurusha mawe katika Jamaraat.

Ayyaamut – Tashriya
     (Siku ya kwanza na ya pili ya Thashriya) Watarudi Mina na kwaajili ya kurusha mawe katika Jamaraat.                                    Ni siku ya kula na kunywa na kumkumbuka Mwenyezi Mungu.

Siku ya mwisho ya Tashriya
     Wanaopenda kubakia Mina watabakia kisha watarudi Makka na ikiwa safari imewadia watafanya Twawwaaful – Wida-a (Twawwaaf ya kuaga).

Hakuna maoni: