Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limemchagua sheikh Abubakar Zubeir bin Ally kuwa mufti wa Tanzania, kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma.
Uchaguzi huo umefanyika baada ya kifo
cha aliyekuwa mufti wa Tanzania. Sheikh Issa bin Shaaban Simba aliyefariki juni
15 mwaka huu kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam,kwa ugonjwa wa
kisukari na presha.
Sheikh Abubakar Zubeir alichaguliwa baada
ya kuwashinda masheikh wengine watatu waliojitokeza kushindania nafasi hiyo.
Mwanazuoni
huyo ndiye aliyekaimu wadhifa huo kwa miezi mitatu baada ya kifo cha mufti Simba,
alichaguliwa kwenye mkutano wa dharura uliojumuisha wadhamini wa baraza hilo,
maulamaa, masheikh wenyeviti wa mikoa na wilaya waliojumuika katika ukumbi wa
hotel ya African dreams uliopo area D mjini Dodoma.
Katika hotuba yake ya shukrani, Sheikh
mkuu, mufti Abubakar alishukuru kamati ya
Bakwata pamoja na wajumbe wote wa mkutano huo, alisema atafanya kazi
yake kwa uandilifu na kuwaunganisha waislamu ambao wanaonekana kukata tamaa
katika nchi yao wenyewe.
“Nawashukuru kwa ushirikiano
mlioniomnyesha na nInaahidi kuyasimamia yote mliyoyasema wakati nilipokaimishwa
nafazi hii kule Bagamoyo na kubwa kufanyakazi na taasisi zote za dini zilizopo
hapa nchini na nje ya nchi kwa mslahi ya waislam.Lakini pia niliahidi huko nyuma
juu ya kuifanyia marekebisho katiba yetu ya Bakwata namuomba Mwenyezi MUNGU aniwezeshe
nianikishe hilo kwa faida ya waislam wote na yeyote mwenye mawazo mema kw ajili
ya kuboresha hali ya waislam nchini,milango iko wazi namkaribisha kwa ushauri mzuri” alisema
mufti. Aliwaomba waislam wote nchini kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu
wa octoba 25 mwaka huu na kumtaka kila mmoja kumchagua kiongozi atakayeona anamfaa
kwa ajili ya maendeleo ya eneo lake na taifa kwa ujumla.
Alikuwa naibu
mufti wa Tanzania katika kipindii cha uongozi wa sheikh mkuu isa bin Shabani Simba
na baadaye kuwa naibu kadhi nkuu wa Tanzania baada ya cheo cha unaibu mifti kufutwa
kwenye katiba ya bakwata.
Sheikh Abubakar ni zao la masheikh wakubwa
nchini kama akina sheikh Hassani hin Ameer aliyeupokea uhuru wa Tanganyika mwka
1961,uwanja wa taifa Dar es Salaam,sheikh Abdallah Farsy wa Mombasa, sheikh
Mohamed Ramia wa Bagamoyo sheikh Mohamed bin Ayoub wa Tanga, mufti sheikh mkuu Hemed
bin Jumaa bin Hemed.
Na kuahidini kuwa nitafanya wema,
uadilifu na heshima ya nchi yetu ili wote tumwabudu Allah (S.W) kwa amani na
usalama “alisema
mufti wa Jamuhuri ya muungano wa
Tanzania sheikh abubakar zubeir bin ally.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni