Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 21 Septemba 2015

Kuzidi hofu ya madhara ya jinai za Saudia nchini Yemen

  Wasiwasi wa taasisi za kimataifa na za nchini Yemen kuhusu jinai za ukoo wa Aal Saud nchini humo umeongezeka mno hivi sasa huku Saudia na kundi lake la nchi zinazotenda jinai, zikizidisha ukatili wao dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Yemen. Jeremy Hopkins, mjumbe wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Yemen ametoa tamko kuhusu kuongezeka jinai na uvunjaji wa haki za wananchi wa Yemen na kuharibiwa miundombinu ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu, na kusema kuwa, ana wasiwasi mkubwa wa kutofika shehena ya misaada ya kibinadamu kwa watu 11 elfu waliokwama huko kusini mwa mji mkuu wa Sana’a, kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Saudia. Jeremy Hopkins ameongeza kuwa, kitendo cha wanajeshi wa Saudia cha kushambulia shehena za misaada ya kibinadamu na maeneo ya kusafishia maji nchini Yemen kinasikitisha sana na kimewasababishia matatizo makubwa wakazi wa eneo hilo. Wizara ya Afya ya Yemen jana Jumamosi ilitoa taarifa na kusema kuwa hospitali za mji mkuu Sana’a hazina uwezo tena wa kupokea majeruhi na zimekumbwa na uhaba mkubwa wa madawa, mafuta na mahitaji mengine ya lazima. Wizara ya Afya ya Yemen imezitaka taasisi za kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuwaokoa wagonjwa na majeruhi wa mashambulio ya anga ya Saudia. Muhammad al Masouri, Katibu Mkuu wa taasisi ya masuala ya kisheria ya “al Bayt al Qanuni” ya Yemen amesema kuwa, hivi sasa haiyumkiniki tena kuzalisha maji safi nchini humo kutokana na kukatika umeme na kuharibiwa mabomba ya mafuta. Ametahadharisha kuwa, wananchi milioni 27 wa Yemen wanakabiliwa na hatari kutoka kila upande. Wanajeshi wa utawala wa ukoo wa Aal Saud jana Jumamosi pia waliendelea kufanya jinai kwenye maeneo ya makazi ya raia katika mikoa ya Sana’a, Sa’ada, Taez, al Baydha na al Hudaydah nchini Yemen na kuua makumi ya wananchi wasio na hatia kujeruhi wengine 100. Vile vile ndege vamizi za Saudia na genge lake zimeshambulia mara 20 majengo ya Wizara ya Vijana, Wizara ya Mambo ya Ndani na kituo cha polisi huko Sana’a. Amma cha kusikitisha zaidi ni kuona kuwa jinai hizo za Saudi Arabia zinafanyika mbele ya macho ya jamii ya kimataifa na mashirika yanayojigamba kuwa ni watetezi wa haki za binadamu na utawala wa sheria, ulimwenguni. Kimya cha mashirika hayo kimezidi kuwa kikubwa katika hali ambayo, shirika la habari la al Ahd la nchini Yemen limeripoti kuwa, Saudi Arabia inatumia pia makombora yenye gesi ya sumu dhidi ya wananchi wa Yemen. Kwa mujibu wa shirika hilo, gesi hizo za sumu zilizoenea kwenye makazi ya raia na mashamba ya kilimo, zimepelekea kuzuka magonjwa ya ajabu nchini Yemen. Houthis 

Hakuna maoni: