Papa Francis anatarajia kurahisisha
taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki waliooana kutoa talaka
na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika kanisa hilo .
Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo .Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama .
Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kupokea komunio.
Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa wanandoa , lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni