Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 21 Septemba 2015

Sudan yatoa wito dhidi ya Israel

Sudan yatoa wito wa kusimama kidete dhidi ya Israel
Serikali ya Sudan imeutaka ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kusimama kidete mkabala na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjidul Aqswa. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imetoa taarifa kuhusiana na uvamizi na hujuma za Israel na mashambulio ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Masjidul Aqswa na waumini wa Kipalestina wanaotekeleza ibada katika msikiti huo na kuonyesha kuchukizwa mno na hatua hizo za Wazayuni. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan  imeutaka ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kuitisha mkutano wa dharura kwa ajili ya kutafuta njia za lazima za kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika msikiti wa al-Aqswa na kusimama kidete mkabala na jinai hizo za kinyama. Taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Sudan imebainisha kwamba, kusimama kidete na kuweko umoja katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu ni jambo la lazima kwa ajili ya kuhitimisha uvamizi na hujuma za Israel na kuzuia kubomolewa msikiti huo mtakatifu. Masjidul Aqswa ni eneo la tatu kwa utukufu kwa Waislamu baada ya Masjidul Haram mjini Makka na Masjidun Nabawi mjini Madina huko Saudi Arabia. Katika miaka ya hivi karibuni, Israel imeshadidisha njama na hujuma zake dhidi ya eneo hilo takatifu.

Hakuna maoni: