Polisi nchini Kenya Jumanne waliwakamata watu watatu waliogundulika
wakiwa na bomu la kienyeji walipoingia kwenye eneo la maduka ya
kifahari.Kwa mujibu wa idara ya polisi ya Kenya bomu hilo liliteguliwa kwa usalama na kulidhibiti lisilipuke.
Mkuu wa polisi, bwana Robinson Mboloi ambaye
anaongoza kituo cha polisi cha Kasarani katika mji mkuu Nairobi akisema
kuwa wamewatia mbaroni wanaume watatu ambao waligundulika kuwa na bomu
hilo la kienyeji na kitufe cha kulilipua. Eneo la maduka ambalo wanaume
hao walikamatwa ni la Garden City Mall.
Bwana Mboloi alisema maafisa wa kitengo kinachoshughulika na milipuko walitegua bomu hilo na eneo hilo la maduka liko salama.
Eneo hilo la maduka ambalo liko mjini Nairobi lilifunguliwa mapema
mwaka huu, na kuelezewa kuwa kituo kikubwa cha maduka ya kifahari katika
Afrika mashariki.
Kenya imekumbwa na mlolongo wa mashambulizi yaliyofanywa na waasi
wenye uhusiano na kundi la wanamgambo wa kisomali la Al-shabaab ambao
miaka miwili iliyopita walishambulia eneo la maduka la kifahari la
Westgate Mall.
Katika shambulizi hilo wanamgambo hao wa kiislamu
walivamia na kuua watu takriban 67 na wafanyakazi katika siku nne za
ghasia wakidai ni majibu kwa jeshi la Kenya kuwepo nchini Somalia.
Wanaume watatu waliokamatwa Jumanne wameripotiwa kuwa wote ni
wakenya na walisimamishwa wakiwa pamoja na maafisa usalama kwenye eneo
la ukaguzi la kuingia kwenye kituo cha maduka.
Mboloi alisema kitufe cha kutegua bomu kilionekana wakati wa ukaguzi
na shukran kwa kazi nzuri ya wana usalama. Na kuongezea watachunguzwa
ili kufahamu mahusiano yao na ugaidi wa kundi la Al-shabaab.
Tangu mashambulizi ya Westgate, kundi la Al-shabaab limeendelea
kuishambulia Kenya ndani ya ardhi yake huku shambulizi kubwa zaidi
likiwa ni lile la mwezi April mwaka huu wakati washambuliaji wanne wa
kujitoa mhanga walipowaua watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa
kilichopo kaskazini mashariki mwa Kenya, wengi wao wakiwa wanafunzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni