I
dadi ya watu waliojitokeza katika baadhi ya vituo ni ndogo, tofauti na
uchaguzi wa awali Oktoba 25, mwaka jana. Baadhi ya mitaa imeonekana
kutulia huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika baadhi ya maeneo.Mgombea
urais wa chama cha ADC Hamad Rashid amepiga kura yake kituo cha
Tondooni Wawi wilaya ya Chake-Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Amesema:
"Nina imani ya kuwa Rais, nikikosa nitakuwa Makamu wa Rais".
Mgombea
urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed
Shein amezungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo
cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja.
Mwanzo amezungumzia hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi huo.
Kuhusu amani na utulivu, amesema anaamini kutakuwa na utulivu visiwani.
Kumbuka, Chama cha Wananchi (CUF) kilitangaza kwamba
hakitashiriki uchaguzi wa marudio unaoendelea leo. Chama hicho
kinaamini kilishinda uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na
mgombea wake Maalim Seif Hamad anafaa kutangazwa mshindi.
Tume ya uchaguzi Zanzibar hata hivyo ilitangazwa kwamba
hakuna aliyejiondoa rasmi kutoka kwa uchaguzi wa leo.
Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja.Katika vituo vingi, wapiga kura hajawafika. Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na maafisa wa usalama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni