Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 23 Machi 2018

Lucy na Seretse Khama

                                                                          

Wakati mwanamfalme wa Kiafrika na karani mmoja mwanamwali Mzungu wa maisha ya wastani kutoka kwa wamiliki wa bima wa Lloyd, walipoamua kuoana mnamo mwaka 1948, ilichochea hisia mbalimbali nchini Uingereza na Afrika.
Seretse Khama alikutana na Ruth Williams alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Oxford na wakaanza kuchumbiana.
Baada ya masomo yake, alitarajiwa kwenda nyumbani hadi katika taifa lake lililokuwa koloni ya Uingereza wakati huo ikijulikana kama Bechuanaland ambayo sasa ni Botswana, na kuoa mmoja wa watu wa kabila lake, lakini mapenzi yake kwa Williams ya libadilisha kila kitu.
Familia yake ilipinga ndoa hiyo na Khama akalazimika kukatalia mbali fursa ya kuwa mfalme.
Serikali ya Uingereza iliingilia kati na kujaribu kupinga ndoa hiyo haua iliyomfanya Khama kufukuzwa kutoka nchi yake.
Askofu wa London, William Wand, angeruhusu tu harusi inayofanyika kanisani ikiwa tu utawala nchini Uingereza ungeruhusu ndoa hiyo kufanyika. Hilo halikufanyika.
Wapenzi hao wawili walilazimika kuoana baadaye katika ofisi ya mwanasheria mkuu iliyoko Kensington huko London mnamo Septemba mwaka 1948.
Waziri mkuu wa Afrika Kusini wakati huo Daniel Malan, alitaja ndoa yao kama "iliyojaa kichefuchefu" huku mwanafunzi mmoja aitwaye Julius Nyerere, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, akasema "ni mojawepo ya hadithi nzuri sana za mapenzi duniani",
Mmoja wa walioshuhudia alizungumza na dadake Ruth Williams, ambaye alisema harusi hiyo ilikuwa "mapenzi yaliyoshinda chuki".
Wawili hao walipata uungwaji mkubwa huku maandamano yakizidi huko Bechuanaland, kushinikiza kutambuliwa kwa ndoa hiyo ambapo baadaye walikubaliwa kurejea nchini humo mnamo mwaka 1956 baada ya watu wa kabila la Bamangwato, lake Bw Khama, walipoamua kutuma barua kwa njia ya telegram hadi kwa Malkia Elizabeth wa II.

Kufanikisha uhuru

Seretse Khama aliamua kukatalia mbali utawala wa kabila lake na akaamua kuwa mkulima na mfugaji huko Serowe. Baadaye alikibuni chama cha Bechuanaland Democratic Party na akashinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 1965.
Akiwa Waziri mkuu wa Bechuanaland (Botswana) alifanikisha nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1966 na akawa Rais wa kwanza wa Botswana.
Ruth Williams Khama, alifahamika kama Lady Khama baada ya uhuru na alihudumu kama mkewe Rais wa Botswana kuanzia mwaka 1966 hadi 1980.
Walijaliwa watoto wanne: Wa kwanza Jacqueline aliyezaliwa Bechuanaland mwaka 1950; Ian aliyezaliwa England mwaka 1953, na pacha Anthony na Tshekedi waliozaliwa Bechuanaland waliozaliwa 1958.
Ian Khama ndiye Rais wa sasa wa Botswana na alianza kuongoza mwaka 2008.
Ian na Tshekedi ni wanasiasa nchini humo.

Mmiliki wa facebook aomba radhi kwa kashfa

Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica,ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa. Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.
Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.
AmesemaThe CEO said: "Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu,na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia,mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook,mwisho wa siku nina wajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu."Amesema Zuckerberg.
Nini ambazo Zuckerberg ameahidi kukifanya?
Katika kufuatilia matatizo ya sasa nay a zamani amesema atafanya mambo yafuatayo
Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko yam waka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.
Kufanyia uchunguzi kazi za program za kimitandao zinazotiliwa shaka
Kupiga marufuku mwanzilishi wa program yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zita pafanya Facebook kuwa mahala salama.

Alhamisi, 19 Januari 2017

Makamu wa rais

                                                                         

Makamu wa rais nchini Gambia Isatou Njie-Saidy amejiuzulu saa chache kabla ya muda wake wa kuongoza kutimia ,AFP imenukuu duru za familia yake.
Waziri wa mazingiura na elimu ya juu pia alijiuzulu,ikiwa ni msururu wa mawazuri kumtoroka bw Jammeh kufuWakati huohuo wakili wa rais Yahya Jammeh ametorokea nchini Senegal baada ya kumuandikia barua rais Jammeh akimtaka kuachilia mamlaka gazeti la Nigeria Primium times limesema.
Edu Gomez alisema kuwa amemfanyia kazi Jammeh chini ya shinikizo chungu nzima .
atia hatua yake ya kukataa kujiuzulu baGazeti hilo pia limenukuu barua hiyo ikisema: Siku ya Jumanne tarehe 17 mwezi Januari 2017, mwanangu na mimi tulifanya uamuzi muhimu kutafuta hifadhi katika taifa jirani la Senegal.Hatua hii tuliona ni muhimu kutokana hofu inayoendelea kutanda na wasiwasi kila wakati.
BBC hatahivyo haijapata uthibitisho huru wa ripoti hiyo.
Bw Gomez alimwakilisha Jammeh katika harakati za kufutilia mbali ushindi wa kiongozi wa upinzani Adama Barrow katika uchaguzi wa tarehe mosi Disemba.
ada ya zaidi ya miongo miwili afisini
                                                                     

Uganda yakanusha tuhuma za Kinshasa kuhusu kundi la M23

Serikali ya Kampala yakanusha tuhuma kuhusu kundi la waasi wa zamani wa M23 Mashariki mwa DR Congo
Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo alifahamisha kutiwa wasiwasi na uwepo wa waasi wa zamani wa kundi la M23 Mashariki mwa nchini.
Kwa upande wake serikali ya Kampala immekanusha uwepo wa waasi hao katika ardhi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Serikali ya Kinshasa ilifahamisha wanamgambo wapatao 150 wa kundi la M23 walingia mashariki mwa Jamhuri ya kşdemokrasia ya Congo.

Putin,Merkel na Hollande,Wafanya mazungumzo

Rais wa Urusi Vladimir Putin,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande wamefanya mazungumzo ya simu

Rais wa Urusi Vladimir Putin,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande wamefanya mazungumzo ya simu kuhusu utatuzi wa masuala ya Ukraine.
Viongozi hawa watatu wamejadili jinsi ya kuisaidia nchi ya Ukraine kutatua matatizo yake.
Mkutano pia uligusia kuendeleza kwa makubaliano waliofanya na nchi hiyo mnamo Oktoba mwaka jana mjini Berlin.
 Kwa mujibu wa habari Mgogoro kati ya serikali ya Ukraine na kundi la Pro Russian Separatist lazima utatuliwe kwani unazidi kusababisha maafa.
Mpaka sasa watu takriban 9750 wamepoteza maisha kutokana na mgogoro huu.

Joto laongezeka zaidi duniani

Kwa kipindi cha miezi kumi na mbili,Hali ya joto duniani imefikia kiwango cha juu zaidi kilichowahi kutokea kwa miaka mitatu mfululizo.
Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa na kusaidiwa na shirika la uchunguzi wa masuala ya anga ( NASA), umebaini kuwa wastani wa joto kabla ya mapinduzi ya viwanda ilikuwa ni kipimo cha celsius 1.1.
Madhara yanayotokana na hali hii ni pamoja na ukame huko nchini India, na kuyeyuka kwa kiwango kikubwa cha barafu katika ukanda wa Arctic.
Wataalamu wametaja sababu za kuongezeka kwa joto duniani kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kama vile shughuli za viwanda zinazochangia kiasi kikubwa cha gesi chafu na hali ya matukio ya asili maarufu kama El Nino yanayosafirisha joto kutoka katika bahari ya pasifiki.
Huu ni mmoja kati ya miaka 16 ya joto zaidi kuwahi kutokea, hali hii imetokea tena karne hii.

Mtu wa mwisha o kutembea kwenye Mwezi, afariki dunia

                                                                   

Mwana anga wa Marekani Gene Cernan, aliyekuwa binadamu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, amefariki dunia akiwa na miaka 82.
Shirika la anga za juu la Marekani Nasa limesema limehuzunishwa sana kumpoteza mwana anga huyo mstaafu.
Cernan alikuwa mmoja wa watu watatu pekee waliowahi kwenda Mwezini mara tatu na ndiye binadamu aliyeukanyaga Mwezi mara ya mwisho kabisa, mwaka 1972.
Maneno yake ya mwisho aliyoyasema kabla ya kuondoka kwenye Mwezi yalikuwa: "Tunaondoka jinsi tulivyokuja na, Mungu akitujalia, tutarejea na amani na matumaini kwa binadamu wote."
Alikuwa kamanda wa chombo cha anga za juu cha Apollo 17 wakati huo.
Ni watu 12 pekee waliowahi kutembea kwenye Mwezi, na kati yao ni sita pekee ambao bado wako hai.
Kupitia taarifa, familia ya Cernan imesema alifariki dunia Jumatatu baada ya kupata matatizo ya kiafya.