Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 26 Desemba 2015

Yesu alizaliwa siku ya tarehe 25 disemba?

                                                                     

                 Angalia mazoea yanayoambatana na krismasi nini mti wa kijani kibichi (mti krimas) siku hizi ya plastiki, ukumbi,mapambo, pamba, mzee mwenye ndevu nyeupe na kofia yenye kishungi na mstari mweupe na suti nyekundu,taa(disco lights) maua ya plastiki,kigogo cha mti kinachoonekana kiini chake,mnyama pori mwenye pembe kama mti na tololi yana maana yeyote na kuzaliwa kwa Yesu?
Yote haya hayana uhusiano naye lakini yana mambo mengi ya kufanya kwenye matamasha ya kipangani. Lini hasa Yesu alizaliwa? Alizaliwa siku ya tarehe 25 disemba?                                 
                               

                  Ukichunguza kwa umakini maandiko, kwa vyovyote, kwa uhakika inaonyesha kuwa tarehe 25 disemba haiwezi kuwa siku ya kuzaliwa Yesu. Hizi ni sababu.
                  Kwanza tunaona kuwa  wachungaji walikuwa kondeni  wanachunga mifugo yao wakati Yesu anazaliwa (Luka 2:7-8) wachungaji hawakwenda kondeni wakati wa mwezi wa kumi na mbili (disemmba),Kulingana na sherehe katika kitabu cha"The complete book of American holydays "mwandishi anasema...
" kulingana na maelezo ya Luka inaonekana Yesu anaweza kuwa alizaliwa kiangazi au mwanzoni mwa kipindi cha mchipuko (falls) . Kwa kuwa disemba kuna baridi kali  na mvua katika Yudea ni wazi wachungaji wangetafuta hifadhi ya mifugo yao wakati  wa usiku. ( Uk. 309)
Pia the enterpreater’s One-volume commentary anasema kuwa aya hiyo
inapinga kuzaliwa ( kwa Yesu) disemba 25  kuwa hali ya hewa haikuruhusu” wachungaji kuchunga mifugo yao wakati wa usiku .
Pili wazazi wa Yesu walikwenda Bethlehem kujisajili katika sensa ya Warumi (Luka 2:1-4)sensa kama hizo hazikufanyika wakati wa baridi ambapo joto lilishuka chini ya kiwango cha kuganda  na njia zilikuwa katika hali mbaya, sensa kwenye hali ya hewa kama hiyo ilikuwa ni sawa na kujishambulia.
              Ilikuwa vigumu kuwaingiza wapangani katika ukristu ukweli muhimu unaotakiwa kuelea vizuri kichwani mwako ni kuwa kuifanya siku ya tarehe 25 Disemba ilikuwa ni makubaliano na wapagani (William Warsh. The story of Santa Klaus 1970 uk.62)
Kama Yesu hakuzaliwa tarehe 25 Disemba, biblia inaonyesha lini?

Lini alizaliwa?
                   Maandiko ya kibiblia yana onyesha wakati wa majira ya mchipuo (falls) ya mwaka kuwa ndiyo uwezekano zaidi wa Yesu kuzaliwa kipindi hicho ukiegemea kwenye hoja ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji.
Elizabeti (mama yake Yohana Mbatizaji. ) alikuwa na ujauzito wa miezi sita wakati taarifa ya Yesu ilipotolewa (Luka 1:24-36)tunaweza kukadiria  wakati wa mwaka Yesu aliozalilwa kama tunaweza kuja wakati aliozaliwa Yohana . baba yake Yohana, Zakaria alikuwa kuhani akihudumu katika hekalu la Jerusalemu wakati wa abiya (Luka 1:5)Historia inaonyesha kuwa hii ilifanyika mwezi wa sita (juni 13 -19) kwa mwaka huo.The campannion bible, 1974, appendix 179. Uk 200)
Wakati huu wa huduma ya hekalu ndipo Zakaria alipo pata habari kuwa yeye na mkewe Elizabeti watapata mwana.
(Luka 1:8-13) baada ya kumaliza zamu yake akarudi nyumbani Elizabeth akapata ujauzito (Luka 1:23-24)
Kadiria kuwa tukio la Yohana lilitokea karibu na mwishoni mwa mwezi wa sita jumlisha miezi tisa inatupeleka mwishoni mwa mwezi wa tatu ambapo ndipo uwezekano mkubwa ndipo alipozaliwa Yohana  jumlisha miezi sita (tofauti ya umri wa kati ya Yohana na Yesu (1:35-36)
Inatupeleka mpaka mwishoni mwa Septemba hapa ndipo pana uwezekano mkubwa wa kuzaliwa Yesu .                                                 
          
                    Ingawa ni vigmu kuipata kwa mara ya kwanza yeyote aliyesherehekea Disemba  kama siku ya kuzaliwa Yesu wanahistoria wanakubaliana kuwa hiyo ililkuwa wakati wa karne ya nne. Hii inashangaza ni tarehe iliyo chelewa krismas hailusherehekewa Roma, mjimkuu wa himaya ya Warumi mpaka miaka 300 baadaye, baada ya kifo cha Yesu. Haina asili katika mafundisho wala matendo ya Wakristu wa mwanzo.


Jumapili, 13 Desemba 2015

Rider Seventeeny

                                                         



Rider Seventeeny
Jina Peter Paschal Joseph
Kuzaliwa Arusha
Mwanamziki
Mtindo bongo flavor
Mwaka alioanza 2004
                    Alizaliwa hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha na kuanza masomo katika shule ya Msingi Kaloleni baada ya  mwaka mmoja wazaszi wake wakahamia Tanga ambako ni nyumba iliko mizizi ya ukoo wake. Hapo akaanza tena darasa la kwanza katika shule ya msingi St.Martin ambayo sasa inaitwa Magila wilayani Muheza  mkoani Tanga huo ulikuwa mwaka 2000.
Hakukaa sana Tanga baba yake alipata uhamisho wa kazi na kuelekea Dar  es salaam hapo hakuwa na hiari isipokuwa kukusanya virago vyake na kumfuata baba yake, kwa mara nyingine  tena akajikuta anaanza darasa la kwanza katika shule ya msingi Vingunguti A iliyopo wilaya ya Ilala huo ulikuwa mwaka 2001.
                            

 Kama kawaida ya vipaji vyote huanza kujitokeza umri mdogo akiwa shuleni akajikuta anapenda muziki na kutamani kuwa mwanamuziki mkubwa albam ya Dully sykes uluyokkwenda kwa jina la historia ya kweli  ilikuwa na wimbo uliobeba jina la historia ya kweli. Kulikuwa na wimbo uliobeba jina la Salome huo ndio uliompagawisha Rider kwa kiwango cha kutosha kumfanya aukariri mashairi yake pamoja na nyimbo zingine ikiemo Monalisa.
Taratibu alijifunza kuimba na kufunga nyimbo pamoja na kuigiza akishirikiana na baadhi ya wanafunzi wenzake waliokuwa  na vipawa vinavyofanana.
                   Mwaka 2004 walianzisha kundi waliloliita Son cost, Rider akiwa kiongozi akishirikiana na Yasco Taller pamoja na Bang'ala wa masoko.  Kundi liliendeshwa Kiugumu ugumu mpaka mwaka 2008  wlipofanikiwa kutoa wimbo ulioitwa Acha bifu waliorekodiwa  katika studio za Pamoja Records kwa Nas B na kinanda kama solo artist. Studio zilikuwa kinondoni mkwajuni hapa walitoa nyimba mbili.
Acha bifu ulionya wasanii wanajamii kuacha mivutano isiyo na tija wala maana yoyote nyimbo  hizo hazikufanikiwa kuchezwa redioni. Mwaka 2009 ulikuwa mwaka mgumu kwa kila manakundi. Wawili wliokuwa wana soma walijikita zaidi katika  masomo na mmoja alikuwa anafanyakazi na kukosa muda wa kufanya muziki kikamilifu. Hivyo kundi likafa kifo cha kawaida.
                            
Akiwa anasoma Secondary ya Msongola hakuacha sanaa imponyoke akageukia sanaa ya maigizo na kujikita katika uchezaji wa filam. Akafanikiwa kupata nafasi katika kundi la Alwatani Theatre Group lililo kuwa na maskani yake ilala likiongozwa na Haji Dilunga.
Akishiriki katika filamu ya Bunge la wachawi namba moja, Bunge la wachawi namba mbili, Popobawa na Zindiko alipopata nafasi ya kuingiza na Ahmed Ulotu (Mzee Chilo). Bada ya kumaliza kidato cha nne akarudi kwenye muziki. Akaanzisha kundi linaloitwa La Ukoo Entertainment.
Kundi lilianza kama masihara, sasa limekuwa kubwa likIshirikisha wasanii wa fani mbalimbali toka kona tofauti tofauti, wazo lilianzaia shuke utekelezapo wake ulipoanza hakukuwa na kusimama hata baada ya kumaliza shule wanebaki na La Ukoo Entertainment kundi likiwa na wachoraji, waigizaji Graphic Designers, vinyozi, wacheza mpira wote pamja wanaitwa La Ukoo. Si kwa maana ya watu wa asili ya sehemu moja la hasha isipokuwa Ukoo katika burudani ndipo wote wanajumuika chini ya  mwamvuli mmoja La Ukoo.
Kwa sapoti ya marafiki na La Ukoo akanza ktoa T-shirt zenye nemo ya la ukoo Entertainment. Milango iko wazi na kundi linapokea yeyote mwenye kipaji cha sanaa anayependa kujiunga 2012 alifanikiwa kutoa wimbo Nimedata akiwa amemshirikisha jay maswagger kutoka kundi la republic. Millionare lililokuwa chini ya  marehemu Sharo Millionere mwongozaji akiwa Dr. Babak na Big Josh imetengenezwa katika Studio za Kany  Records chini ya producer Man Lee” hii pia haijapata kuchezwa redioni ila inapatikana youtube kwa jina   rider 17 ft.Jay Maswagger
                                 
                    kama kawaida changamoto haikosekani popote hapa zinamkabili pia Rider kwenye kazi yake ameonyesha kipaji akabuni wazo , na kulifanyIa kazi lakini ukosefu  wa pesa ni changamoto kubwa na nzito kwake, kuikabili, pia msimamizi wa kazi zake pamoja na wadhamini bado hajawapata hivyo kumuwia vigumu kurekodi na kuzifanyia promo kazi zake zichezwe katika vituo vya radio na tv ziweze kuwafikia watu  kwenda Studio kwa miguu ni changamoto nyingine inayomkabili. Pia wapo watu wanaoshindwa kuthubutu kufanyia kazi mawazo yao. Hawa wanatumia midomo na nguvu zao kumkatisha tamaa ya kutimiza ndoto zake.Hivyo  yeyote mwenye kutaka kusukuma harakati hizi kwa michango ya hali na mali na mawazo mazuri milango iko wazi na anakaribishwa.Yote kwa yote hachoki anakaza mkwiji na kusonga mbele sasa anajiandaa kurekodi wimbo mpya na kutoa video yake wapenzi na mashabiki wake watapata kazi zake kupitia mitandao ya kijamii kueni mkao wa kula.

Ijumaa, 11 Desemba 2015

Ethiopia Inakabiliwa na Ukame

Ethiopia inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 50, huku shirika la Save the Children likitoa wito  wa  haraka wa  msaada wa chakula.
Shirika hilo limesema msaada huo utakuwa ni suluhisho la mda tu, na viongozi wa dunia wanaokutana mjini Paris lazima wachukuea hatua juu ya  mabadiliko ya hali ya hewa.
Serikali ya Ethiopia inasema watu millioni 10 na laki moja  watakabiliwa na upungufu wa mkubwa wa chakula mwaka 2016, na  zaidi ya   nusu ya hao ni watoto.
Kadhalika kuna watoto takriban laki 4 walio katika hatari ya kukumbwa na  utapia mlo mkubwa, hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa ukuwaji na matatizo ya akili.
John Graham, mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Ethiopia, amesema mzozo wa mwaka huu ni matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Ukame mbaya unahusishwa  na mfumo wa hali ya hewa ujulikanao kama El Nino umeharibu misimu miwili mikuu ya mvua nchini humo mwaka huu na kutokana na hilo mavuno yajayo hayatarajiwi kuja hadi mwezi Juni mwakani.
Idara ya Umoja wa Mataifa ya  Chakula na Kilimo (FAO) inakadiria kuwa takriban aslimia 80 ya Waethiopia wanafanya kazi katika sekta ya kilimo, na wengi wao ni wakulima wa wadogo wadogo ambao wanategemea mvua  kwa kilimo.
Hiyo ndio sababu taifa hilo linakumbwa na mizozo ya chakula mara kwa mara na wakulima wanakosa njia na elimu ya kukabiliana na changamoto za hali ya hewa.
Shirika la Save the Children linaomba  msaada wa  takriban dola  millioni 100 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa lakini limesema mwaka huu majibu yamekuwa  ya pole pole mno.

Rais Magufuli atangaza baraza la mawaziri Tanzania

Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake jipya la mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lenye wizara 18 lakini litakuwa na mawaziri 

Katika mtiririko huo kuna baadhi ya wizara zitakuwa na waziri pekee bila ya kuwa na naibu waziri ambapo lengo kuu ni kutimiza ahadi ya kuwa na baraza dogo lenye kasi ya ufanyaji kazi  na kupunguza gharama za matumizi ya serikali yasiyo ya lazima.
Rais magufuli alisema baraza lake la mawaziri halitakuwa na semina elekezi na fedha zilizotengwa shilingi bilioni mbili kwa shughuli hiyo zitaelekezwa katika ufanyaji kazi mwingine wa kuboresha maendeleo ya wananchi kama vile madawati au kwenye utoaji wa elimu bure.
Wizara ya mambo ya njena EAC/Kimataifa
- Augustino Mahiga, Naibu Waziri - Dk. Suzan Kolimba
Wazara wa Utamaduni, Sanaa na michezo
Waziri-Nape Nnauye
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri -Sospeter Muhongo na Naibu Waziri-Medard Kalemani
Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri -Jenista Mhagama
Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala
mawaziri wawili - Simbachawene na Kairuki
Ofisi ya Makamu wa Rais/Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba Naibu waziri Luhaga Mpina.
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri ni Charles Kitwanga
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi
Waziri wake ni Wiliam Lukuvi Naibu Angelina Mabula.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Husein Mwinyi
Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri - Harrison Mwakyembe
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi
Waziri- Mwigulu Nchemba Naibu Waziri- William Tate Ole Nashon
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Waziri - Charles Mwijage
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalimu Naibu - Dk Hamis kigwangalla
Wizara ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi
Waziri - bado hajapatikana - Naibu Waziri -Stela manyanya
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri - bado hajapatikana na Naibu Waziri - Injinia Ramo Makani
Waziri wa Fedha na Mipango
Waziri - bado hajapatikana, Naibu Waziri - Dk. Ashantu Kijachi
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri - bado hajapatikana, Naibu Waziri -Edwin Ngonyani

Jumapili, 6 Desemba 2015

Alvin “ Secco “ Patterson

Alvin Patterson


Alvin “ Secco “ Patterson
Jina kamili Fransisco Willie
Pia anajulllukana kama
 Alvin “ Secco “ Patterson,Secco Pep ,Willie Pep
Alizaliwa (1930-12-30)
Asili – Kingston Jamaica
Mtindo – Reggae
Mpigaji wa percurssion
Vyombo anavyopiga –percussion /bongo drum , conga, tambourine, cowbell, nk.
Mwaka aliofanya kazi 1969 mpaka sasa
Alioshirikiana nao
Bob Marley & The Wailers,The Wailers
Alvin “ Secco “ Patterson
             Alizaliwa tarehe 30 Desemba 1930, Havana (Cuba) ni mpiga percussion alikuwa mwanakundi wa The Wailers band
Alvin  alikuwa ni mpiga percussion katika Bob Marley and The Wailers na ni mmoja kati ya marafiki wa karibu sana wa Bob Marley. Ingawa anajulikana kama “Secco”alizaliwa akaitwa Fransisco Willie, Havana Cuba na baba mwenye asili ya Jamaica na mama Mpanama akiitwa Cellestina Hardin. Alichagua jina la Alvin Patterson kama jina la kisanaa na alipata jina la “Secco” kama kifupisho cha jina lake la Fransisco alihamia Jamaica na wazazi wake waliishi Westmorland, ambako wazazi wake walikuwa wanajishughulisha na kilimo baadaye akahamia Kingston na mama yake baada ya wazazi wake kuachana, kama kijana Patterson alitafuta kazi katika mgodi wa madini ya bauxite
              Mwaka 1957 Patterson aliamua kuhamia Marekani kutafuta kazi yenye kipato zaidi. Akiwa katika safari yake ajali mbaya ilitokea ya treni ilitokea 1st September.   Mara moja Patterson alirudi kisiwani kuwatafuta ndugu zake aliohofia wanaweza kuwemo kati ya watu 200 waliofariki au 700 waliojeruhiwa. Na wazo lake la kuondoka likafutika ma akarudi jumla Kingston katika mgodi wa bauxite.
              Ilikuwa kipindi hiki ndipo Patterson kwa mara ya kwanza alipo kutana na Bob Marley  akiwa na miaka kumi na tano, mdogo kwa Patterson tofauti ya miaka kumi na tano na waliishi wote  eneo moja katika makazi  duni ya  watu masikini Trech town. Marley alimwona Patterson sababu ya umaarufu wake wa mchezo wa cricket, alikuwa na uwezo mkubwa wa kuucheza na akaanza kumfuatilia Patterson mara kwa mara, akitafuta ujuzi wa criket na pia akivutiwa na muonekano wa Alvin Patterson
Wakazama katika urafiki na Marley na wakabaki hivyo mpaka mwisho wa maisha ya Marley. Patterson alimtia moyo Marley  wakati anaanza kujaribu kuimba muziki,akiwa Patterson mwenyewe alipata uzoefu katika muziki wa kupiga percussion kwa mwanamuziki maarufu wa Calypso akiitwa Lord Flea na wapiaji wengine  namna ya kupiga combo za kikalypso. Na alikuwa ni Patterson kwanza aliyelichukua kundi la The Wailers. Likiwahusisha Marley, pamoja na Peter Tosh na Bunny Wailer kulipeleka studio za Coxsson  dodd kwa mara yao ya kwanza july 1963.  Makubaliano yalifikiwa na The Wailers  wakatoa muziki uliotikisa “simmer down” wimbo uliomtambulisha Marley
                    Wakati wailers ikijitanua katika muziki Jamaica,Patterson aliendelea kifanyakazi katika mgodi wa bauxite, mwaka 1966 wakati Marley akifanyakazi Marekani, Patterson alijeruhiwa katika ajali iliyotokea katika mgodi, wakati bomba la gasi iliyopita chini ya sakafu ya canteen ilipopasuka, ikasababisha mlipuko ulioacha wafanyakazi wengi kujeruhiwa vibaya. Patterson alitupwa nje ya jengo na akapoteza viatu katika tukio hilo wakati  Marley aliporudi kisiwani wiki kadhaa baadaye , alimshawishi Patterson  kuachana na kazi ya mgodini na aanze kujikita katika muziki matokeo yake Patterson akaanza kuchangia percussion katika nyimbo zilizofuata za The Wailers mchango wake wa kwanza unaojuikana ulikuwa juni 1967walipotoa “ lyrical satirycal” na this train” ziliachiwa na the wailers zikihusisha wail n soul M label. Wakati ushiriki wa Patterson katika Original Wailers (ikiwahusisha Tosh na Bunny) ulikuwa mdogo, lakini mchango wake ulizidi kuongezrka. Wakati Original Wailers walipokwenda  ziara yao ya kwanza (pekee)uingereza  mwaka 1973. Patterson alishiriki kama mtu wa kipekee kwenye ubunifu wa kiasili(root)
                   Wakati ushirikiano wa Marley, Tosh na Bunny ulipoisha Paterson akawa kiini cha kuihuisha bendi upya kwa maelezo ya Marley na akashiriki kila rekodi na  maonesho yote ya jukwaani ambayo Marley alifanya kwa maisha yake yote, Patterson akazama katika muziki na rekodi walizofanya  akibuni na kufanya muziki   uonekane wa kiasili.
Chupa ya maziwa katika “jamming” na muitikio wake sauti ya percussion katika “crazy baldhead” ni miongoni mwa mifano bora kabisa ya mitindo yake ya kufanya. Kitu rahisi kwa ubora wa juu. Ingawa hakutajwa Patterson anaaminika aliandika baadhi ya nyimbo za marley ukijumlisha na “work”.
                     
Wakati wote wa maisha ya marlley Patterson alikuwa karibu yake. Mwaka 1976,Patterson alikuwa anafanya mazoezi na Marley akiwa barabara ya 56 Hope (road) ambapo mtu mwenye bunduki alimjeruhi Marley, pia walikuwepo mkewe Marley na meneja Don Taylor. Septemba 1980 Patterson alikuwa na Marley wakati alipopatwa shambulio la ugonjwa  wakati anafanya mazoezi ya mbio (jigging) centra park na akabaki na Marley wakati  wote wa matibabu yake ya kansa new York, marekani mpaka katika kliniki ya Dr Jose Issels.
Rottach-Egern, Ujerumani.
Kufuatia kifo cha Marley, Patterson aliendelea music na The Wailers band . mwaka 1990 Patterson alipata shambulio la ubongo, (haemorrhage) akiwa ziarani Brazil shambulio lililokaribia kupoteza maisha yake alipopata nafuu akaachana na muziki wa jukwaani isipokuwa anaonekana tu katika matamasha mbalimbali yanayomuhusisha Marley . Patterson sasa anaishi kingston.