Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Clinton na Trump warushiana vijembe katika hafla

                              Wagombea urais wa Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump hawakujizuia kutoleana maneno katika hafla ya chakula cha jioni ya kila mwaka kwa ajili ya kutoa misaada mjini New York, wakati wa kutoa hotuba zao ambazo ni utamaduni wa kutoa vichekesho kwa kila mmoja anayegombea urais, nchini Marekani lakini walijikuta wakishambuliana.
Katika mlo huo wa jioni wa kumbu kumbu ya Alfred E.Smith ambao huandaliwa na taasisi ya hisani ya Catholic Charity wagombea hao wawili walikaa meza moja na kutoa maneno ya kuchekesha katika hotuba zao siku moja baada ya mdahalo uliokuwa na ushindani mkali na maneno makali dhidi ya kila mmoja kuwahi kutokea katika historia ya Marekani.
Trump ambaye alianza kuzungumza katika usiku huo alichukua nafasi hiyo kufanya utani juu ya jambo ambalo limezungumzwa sana katika uchaguzi wa mwaka huu kuhusu tabia na mwenendo wake.
Clinton nae kwa upande wake alianza hotuba yake kwa kutoa utani juu ya hali ya afya yake ya hivi karibuni na fedha anazolipwa.

'Diwali' yalaumiwa mjini Delhi

                          Wakazi wa jiji kuu la India, Delhi wameghadhabishwa na kile wamesema kuwepo ukungu mkubwa uliosababishwa na fataki nyingi zilizorushwa katika sherehe za Diwali.
Mamlaka zilionya uchafuzi wa hewa kutokana na fataki hizo kutumiwa juu ya kiwango kilichowekwa. Sherehe za Diwali ni muhimu sana katika imani ya Kihindi na huadhimisha ushindi wa wema dhidi ya ubaya.
Baraza la mji wa Delhi liliahidi kuweka vifaa muhimu za kusafisha hewa wakati wa sherehe hizo. Kabla ya Diwali kumekua na kampeini kadhaa zikiwataka raia kutofyatua fataki. Hata hivyo wito huo haikutiliwa maanani. Urushaji wa fataki huambatana na sherehe za Diwali na wengi huona hii kama ishara ya utajiri.
Familia na kampuni za biashara nchini India hutumia maelfu ya dola kununua fataki ambazo hurushwa usiku wakati wa sherehe hizo. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani{WHO} miji 13 kati ya 20 ambayo imechafuliwa zaidi duniani inapatikana India.
Kando na fataki, India pia huchafuliwa hewa wakati wa msimu wa baridi ambapo jamii masikini hulazimika kuchoma takataka kama njiya ya kupata joto hususan wakati wa usiku. Aidha kuna desturi ya kuchoma mashamba baada ya mavuno na moto huchukua siku kadhaa kabla ya kuzima

Mtoto kutoka Ghana alipata umaarufu mitandaoni

                                                               

      Mtoto mmoja wa kiume ambaye picha yake ilipata umaarufu kwenye mitandao huenda ikasababisha kijiji kizima kupata elimu.
Jake amekuwa mmoja wa wanafunzi maarufu zaidfi nchini Afrika Kusini tangua watu waanze kusambaza picha yake huku wakiifanyia utani picha hiyo
Hata hivyo Jake anaishi umbali wa kilomita kadha kaskazini, katika kijiji kimoja kilicho mashariki mwa Ghana bila ya kufahamu umaarufu alioupata.
Ukweli ni kwamba hadi siku ya Jumatano hata mtu ambaye aliipiga picha hiyo hakuwa na habari kuwa imepata umaarufu.
Mpiga picha Carlos Cortes alisafiri kwenda nchini Ghana mwaka 2015 na kufanya makala kuhusu Solomon Adufah, ambaye ni msanii aliyekuwa akirejea nyumbani kutoka Marekani.
Picha ya Jake ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka minne, ni kati ya mamia ya picha zilizopigwa wakaati Adufah alikuwa akiwafunza watoto sanaa.
Lakini picha hiyo ya Jade ilianza kusambaa mitandaoni baada ya Adufah kuituma kwa akaunti yake ya mtandao wa Instagram.
Wakati aligundua kuwa picha hiyo imeanza kupata umaarufu hakujua cha kufanya.
Hapo ndipo sasa Adufah ambaye ameishi Marekani tangu umri wa miaka 16 alianzisha mchango akiwa na matumaini kuwa Jake atasababisha watu kudhamini elimu yake na ya watoto wengine kijijini.
Ndani ya saa 24 kampeni hiyo ilichangisha dola 2000. Adufa anasema kwa pesa hizo zitatatumiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa watoto wa eneo hilo.

Papa Francis kuhudhuria maadhimisho ya mageuzi ya Kiluteri Sweden

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amekoselewa na wakatoliki wahafidhina kufuatia uamuzi wake wa kuhudhuria maadhimisho ya Jubilei ya miaka 500 ya mageuzi ya Kiluteri yaliyoanzishwa na Martin Luther yatakayofanyika nchini Sweden. Martin Luther raia wa Ujerumani alianzisha mageuzi hayo mnamo mwaka 1517 mara baada ya kuandika tasnifu 95 akilikosoa kanisa katoliki la Roma kwa vitendo vya rushwa. Papa Francis anautembelea mji wa Lund kusini mwa Sweden ambako shirikisho la kiluteri la kidunia lilianzishwa mnamo mwaka 1947 na atafanya ibada ya pamoja na waluteri ili kuzindua maadhimisho hayo yatakayoendelea hadi mwakani. Ziara ya kiongozi huyo inaonekana kuungwa mkono na waluteri licha ya ukosoaji kutoka kwa wakatoliki wahafidhina.

Watoto milioni 300 duniani wanavuta hewa chafu sana

         Katika utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa, karibu watoto milioni 300 wanaishi kwa kuvuta hewa chafu ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa ya kimwili ikiwemo kuharibu ubongo wao. Kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF yaliyotolewa leo Jumatatu, karibu mtoto mmoja kati ya watoto saba duniani kote anaishi kwa kuvuta hewa ya nje iliyo chafu mara sita zaidi ya miongozo ya kimataifa, na kusema kwamba uchafuzi wa hewa ni chanzo kikuu katika vifo vya watoto. UNICEF imechapisha utafiti wake wiki moja kabla ya kufanyika mazungumzo ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa yanayohusu mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yatanyika nchini Morocco katikati ya mwezi Novemba. Kwa mujibu wa UNICEF uchafuzi wa hewa unasababisha vifo vya watoto laki sita walio chini ya umri wa miaka mitano kila mwaka na kutishia maisha na mustakabali wa mamilioni ya watoto, amesema mkurugenzi wa shirika hilo Anthony Lake.

Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Burundi ina mipango ya kujiondoa mahakama ya ICC

Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo amesema nchi hiyo ina mipango ya kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama ya kimataifa ya kushughulikia kesi za uhalifu ya ICC, miezi sita baada ya mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda kusema watachunguza ghasia zilizuka nchini humo zilizosababisha vifo vya mamia ya watu. Sindimwo amesema wameiandikia mahakama hiyo ya ICC kueleza nia yao ya kujiondoa kutoka mkataba wa Roma kwani wamegundua ni muhimu kujiondoa ICC ili Burundi iwe huru. Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilitumbukia katika mzozo mwaka jana baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea muhula wa tatu madarakani kinyume na katiba.

Rais wa Colombia ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel

                                                          

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2016 licha ya kuvunjika kwa mkataba wake wa kusitisha vita na waasi wa Farc nchini humo.
Rais Santos aligongwa vichwa vya habari baada ya kufanikiwa kupata makubaliano ya amani na waasi hao jambo ambalo lilifikisha kikomo vita vilivyodumu kwa karibu miaka hamsini.
Mkataba huo ulitiwa saini na Bw Santos na kiongozi wa waasi hao kamanda Rodrigo Londono, anayejulikana vyema kwa jina Timochenko mjini Cartagena tarehe 27 Septemba.
"Colombia inasherehekea, ulimwengu unasherehekea kwa sasa kuna vita vimemalizika duniani," alisema wakati huo.
"Tutatimiza malengo yote, tutazidi nguvu changamoto zote na kugeuza nchi hii kuwa taifa ambalo tumekuwa tukitaka liwe, taifa la amani."
Watu 260,000 waliuawa kwenye vita hivyo na wengine milioni sita kuachwa bila makao.
Mapatano hayo na kundi la waasi la Farc yalikataliwa na raia katika kura ya maoni iliyoandaliwa Oktoba 2.
Wakosoaji wanasema kuwa mkataba huo wa amani unawapa waasi wa Farc fursa ya kukwepa haki kwa makosa waliyofanya.
Lakini rais Santos kwa upande wake anasema kuwa hayo ndiyo mapatano bora zaidi yanayoweza kufanywa kwa niaba ya Colombia.
Baadhi ya wanachama wa FARC, pamoja na maafisa wa kijeshi na polisi walipangiwa kufikishwa mbele ya mahakama maalumu kujibu mashtaka kwa makosa ambayo wametekeleza katika vita nchini humo chini ya mkataba huo.
Kundi la Farc, ambalo lilianza kama wanamgambo wa Chama cha Kikomunisti mwaka 1964, linatarajiwa kuacha vita na kuingia katika siasa za amani.