Wakazi wa jiji kuu la India, Delhi wameghadhabishwa na kile wamesema
kuwepo ukungu mkubwa uliosababishwa na fataki nyingi zilizorushwa
katika sherehe za Diwali.
Mamlaka zilionya uchafuzi wa hewa
kutokana na fataki hizo kutumiwa juu ya kiwango kilichowekwa. Sherehe za
Diwali ni muhimu sana katika imani ya Kihindi na huadhimisha ushindi wa
wema dhidi ya ubaya.
Baraza la mji wa Delhi liliahidi kuweka
vifaa muhimu za kusafisha hewa wakati wa sherehe hizo. Kabla ya Diwali
kumekua na kampeini kadhaa zikiwataka raia kutofyatua fataki. Hata hivyo
wito huo haikutiliwa maanani. Urushaji wa fataki huambatana na sherehe
za Diwali na wengi huona hii kama ishara ya utajiri.
Familia na
kampuni za biashara nchini India hutumia maelfu ya dola kununua fataki
ambazo hurushwa usiku wakati wa sherehe hizo. Kwa mujibu wa Shirika la
Afya Duniani{WHO} miji 13 kati ya 20 ambayo imechafuliwa zaidi duniani
inapatikana India.
Kando na fataki, India pia huchafuliwa hewa
wakati wa msimu wa baridi ambapo jamii masikini hulazimika kuchoma
takataka kama njiya ya kupata joto hususan wakati wa usiku. Aidha kuna
desturi ya kuchoma mashamba baada ya mavuno na moto huchukua siku kadhaa
kabla ya kuzima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni