Tafuta katika Blogu Hii
Jumatatu, 31 Oktoba 2016
Papa Francis kuhudhuria maadhimisho ya mageuzi ya Kiluteri Sweden
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amekoselewa na
wakatoliki wahafidhina kufuatia uamuzi wake wa kuhudhuria maadhimisho ya
Jubilei ya miaka 500 ya mageuzi ya Kiluteri yaliyoanzishwa na Martin
Luther yatakayofanyika nchini Sweden. Martin Luther raia wa Ujerumani
alianzisha mageuzi hayo mnamo mwaka 1517 mara baada ya kuandika tasnifu
95 akilikosoa kanisa katoliki la Roma kwa vitendo vya rushwa. Papa
Francis anautembelea mji wa Lund kusini mwa Sweden ambako shirikisho la
kiluteri la kidunia lilianzishwa mnamo mwaka 1947 na atafanya ibada ya
pamoja na waluteri ili kuzindua maadhimisho hayo yatakayoendelea hadi
mwakani. Ziara ya kiongozi huyo inaonekana kuungwa mkono na waluteri
licha ya ukosoaji kutoka kwa wakatoliki wahafidhina.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni