Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Watoto milioni 300 duniani wanavuta hewa chafu sana

         Katika utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa, karibu watoto milioni 300 wanaishi kwa kuvuta hewa chafu ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa ya kimwili ikiwemo kuharibu ubongo wao. Kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF yaliyotolewa leo Jumatatu, karibu mtoto mmoja kati ya watoto saba duniani kote anaishi kwa kuvuta hewa ya nje iliyo chafu mara sita zaidi ya miongozo ya kimataifa, na kusema kwamba uchafuzi wa hewa ni chanzo kikuu katika vifo vya watoto. UNICEF imechapisha utafiti wake wiki moja kabla ya kufanyika mazungumzo ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa yanayohusu mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yatanyika nchini Morocco katikati ya mwezi Novemba. Kwa mujibu wa UNICEF uchafuzi wa hewa unasababisha vifo vya watoto laki sita walio chini ya umri wa miaka mitano kila mwaka na kutishia maisha na mustakabali wa mamilioni ya watoto, amesema mkurugenzi wa shirika hilo Anthony Lake.

Hakuna maoni: