Serikali ya China imetangaza kwamba itapiga marufuku biashara ya
pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwisho wa
mwaka 2017.
Baraza la mawaziri la China katika taarifa yake hapo Ijuma, limeeleza
kwamba “ili kulinda vyema ndovu na njia bora ya kupambana na biashara
haramu China itasitisha hatua baada ya hatua viwanda na uuzaji wa pembe
kwa ajili ya biashara, ifikapo mwisho wa 2017.”
China imekua
ikikabiliwa na shinikizo kutoka Jumuia ya Kiamtaifa kukomesha utumiaji
wa bidhaa za pembe. Na mwezi Machi baada ya mkutano kati ya marais
Barack Obama na Xi Jinping, serikali ya Bejing ilieleza kwamba itapanua
marufuku ya pembe na bidhaa za pembe zlizoagiziwa kutoka nje kabla ya
1975.
"Haya ni mabadiliko makubwa kwa ndovu wa afrika", alisema Aili Kang,
mkurugenzi wa kitengo cha Asia cha Tasisi ya kulinda Wanyamapori iliyoko
New York. “Nina fahari kubwa kwa nchi yangu kuonesha uwongozi ambao
utasaidia kuhakikisha kwamba ndovu wana uwezo hivi sasa ya kunusurika na
kutotoweka duniani.”
Shirika la habari la China Xinhua linaeleza kwamba marufuku hiyo
itasababisha kufungwa kwa viwanda 34 na vituo 143 vya bishara
vilivyoidhinishwa.
Biahsra ya peme ilipigwa marufuku 1989 na mkataba wa kimataifa
chiniya shirika la CITES. China ndio soko kuu la duniani la biashara ya
pembe za ndovu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni