Tafuta katika Blogu Hii
Jumatatu, 2 Januari 2017
Trump na Ngueso kuijadili Libya
Rais Denis Sassou Ngueso wa Jamhuri ya Kongo atakutana na rais mteule wa
Marekani, Donald Trump, kuujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini
Libya, pamoja na masuala mengine yanayolihusu bara la Afrika. Msemaji
wa Nguesso, Thierry Moungalla, amethibitisha taarifa hiyo kupitia
mtandao wa Twitter. Wawakilishi wa Trump, anayetarajiwa kuanza rasmi
majukumu yake Januari 20, hawakuwa tayari kuthibitisha mara moja juu ya
kuwepo kwa mkutano huo. Libya imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa
kufuatia pande mbili za kiserikali nchini humo kuhasimiana huku makundi
mengine yaliyo na silaha nayo pia yakipambana kuwania madaraka. Mapema
mwezi huu, Umoja wa Mataifa ulielezea juu ya mgogoro wa kibinadamu
nchini Libya, ambao unazidi kuyafanya mapambano dhidi ya wahamiaji
haramu kuwa magumu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni