Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 3 Novemba 2016

Kiongozi wa IS asema hakuna kusalimu amri

Wakati vikosi vya Iraq vikizidi kuusogelea mji wa Mosul, kiongozi wa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS Abu Bakr al-Baghdadi amewatumia ujumbe wa sauti wapiganaji wake akiwataka kutosalimu amri dhidi ya majeshi ya serikali. Kiongozi huyo amesikika akisema "hakuna kusalimu amri" na kuwaambia wapiganaji kwamba ni heshima kuilinda ardhi hiyo kuliko kusalimu amri kwa aibu. Huo ni ujumbe wa kwanza kutolewa na kiongozi katika kipindi cha mwaka mmoja na kumekuwa na tetesi juu ya afya na harakati za kiongozi huyo lakini hajulikani alipo. Mwezi Juni mwaka 2014, alijitokeza hadharani mjini Mosul na kutangaza Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria. Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani na unaovinga mkono vikosi vya Iraq, unakadiria kuwepo kiasi ya wapiganaji 3000 hadi 5000 wa IS ndani ya mji wa Mosul.

Hakuna maoni: