Takriban watu elfu 60 wameyakimbia makaazi yao wakati ambapo polisi
na vikosi vya wazimamoto wanapelekwa kwa wingi katika mji wa Haifa
ambako inahofiwa kwamba moto huo mkali unaweza kuendelea kutokana na
hali ya ukame inayoandamana na upepo. Watu kadhaa wamelazwa hospitali
kutokana na madhara ya kuvuta moshi lakini hakuna taarifa zinazoashiria
kuwa kuna watu walio katika hali mahututi. Mamia ya nyumba za watu
ziliharibiwa katika mkasa huo, Israel hapo jana ililazimika kuwaita
maafisa wa jeshi wa akiba kuja kuungana na polisi wa nchi hiyo pamoja na
wazima moto. Vile vile maafisa hao waliitumia ndege maalum ya
kupambana na moto mchango uliotolewa na jamii ya kimataifa.
Msemaji
wa jeshi la polisi nchini Israel Micky Rosenfeld amesema shughuli za
kuwahamisha watu zilifanyika jana usiku katika mji mdogo ulio karibu na
jiji la Jerusalem baada ya nyumba kadhaa katika mji huo kushika moto.
Hadi kufikia sasa watu 12 wamekamatwa na wanatuhumiwa kuhusika na moto
huo. Viongozi wa Israel wanahisi kwamba moto huo umeanzishwa kwa
Waziri
mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaumu vitendo vya uchochezi
moingoni mwa Wapalestina kuwa ndio chanzo cha mashambulio hayo. Moto
huo ulianza siku tatu zilizopita katika eneo la jamii ya Neve Shalom
karibu na mji wa Jerusalem eneo ambalo jamii za Kiarabu na Kiyahudi
zinaishi pamoja. Baadae moto ulizuka upande wa kaskazini katika eneo la
Zichron Yaakov na kwengineko karibu na mji wa Jerusalem kabla ya moto
mkubwa kuanza katika mji wa Haifa. Nchi kadhaa zikiwemo Urusi,
Ufaransa, Cyprus, Uturuki,Croatia,Ugiriki na Italia zimetuma misaada yao
ya kupambana na moto huo. katika hatua isiyo ya kawaida Wapalestina
pia wamejiunga na wazima moto wa Israeli kusaidia kuuzima moto huo.
Maafa
haya ni mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2010 wakati Israel
ilikumbwa na moto mkubwa uliowahi kutokea katika historia, moto huo
ulisababisha vifo vya watu 42 na wazima moto waliweza kuuzima baada ya
siku nne pale ndege maalum ya kuzima moto ilipofika kutoka Marekani na
kutokea wakati huo Israel imeimarisha vifaa na jeshi lake la kupambana
na moto, imenunua ndege maalum za kuzima moto ambazo zina uwezo wa
kumwaga maji mengi katika eneo husika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni