Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 3 Novemba 2016

Wikileaks yachapisha barua pepe mpya kuhusu Clinton

Mtandao wa Wikileaks umechapisha barua pepe mpya kutoka kwa mkuu wa timu ya kampeni ya Hillary Clinton, John Podesta. Barua pepe hizo zinaonyesha wizara ya mambo ya nje ikimueleza Clinton juu ya ripoti inayohusu taarifa za matumizi ya barua pepe binafsi. Katika taarifa zilizoko ndani ya barua pepe za Clinton, kunaonekana kuwepo na uratibu wa karibu kati ya wizara na timu ya kampeni ya Hillary Clinton na zinapendekeza kwamba huenda afisa wa serikali alimdokeza Bi. Clinton kuwa taarifa zake za matumizi ya barua pepe binafsi ziko karibu kujulikana. Timu ya kampeni ya Clinton inaishutumu Wikileaks kwa kutumia taarifa zilizodukuliwa na Urusi katika jitihada za kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo. Wagombea wote wawili Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrats wameendelea kutupiana vijembe katika kampeni za lala salama kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Hakuna maoni: