Maafisa wa usalama wa Marekani wameanzisha uchunguzi wa haki za
kiraia baada ya kanisa moja la watu weusi katika jimbo la kusini la
Mississipi baada ya kuchomwa moto na kuandikwa kwa rangi alama ya
“Mpigie kura Trump” .
Kanisa hilo la kihistoria lililojengwa miaka 111 iliyopita la
Hopewell Missionary huko Greenville Mississipi liliharibika sana
kutokana na maji mengi ya kuzima moto na moshi hapo Jumanne usiku.
Meya wa Greenville Errick Simmons alisema kwamba wanalichukulia tukio
hilo kama uhalifu wa chuki kwasababu ya ujumbe wa kisiasa ambao
wanaamini ulikuwa na lengo la kusababisha kitisho kwsa waumini wapiga
kura.
Anasema kitendo hicho ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya haki ya wananchi kuabudu kwa uhuru.
Meya huyo alisema kwamba Idara ya upelelezi wa jinai , FBI na idara
ya upelelezi ya jimbo la Mississipi wanasaidia katika uchunguzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni