Ndege kuu za kivita za Urusi zimeonekana kwa mara
nyingine tena katika anga ya Ulaya. Taarifa hii imetolea na jeshi la
Ufaransa. Jumatano jioni, Novemba 16, ndege za kivita aina ya Tupolev 95
zilipita kwenye anga ya kaskazini mwa Ulaya na kisha karibu na pwani ya
Ireland na kuingia Ureno, zikipitajuu ya bahari ya Atlantiki kabla ya
kugeuza na kurudi nyuma.
Jeshi
la Ufaransa ambalo katika miezi ya hivi karibuni lilikuatana mara kadhaa
na ndege hizo limetuma ndege ya upelelezi ilikufuatilia ndege hizo za
Urusi. Lakini kwa sasa, ndege hizo za Urusi zinaonekana zikiwa mbali
kidogo na ardhi ya Ufaransa. Hii ni mara ya tatu tangu kuanza kwa mwaka
huu ambapo jeshi la Ufaransa linakutana na tukio hili.
Februari 17, ndege mbili aina ya Tupolev-160 zilikaribia pwani ya Ufaransa na zilionekana kwenye rada ya ndege za kivita za Ufaransa aina ya Rafale, Septemba 22 ndege hizo zilionekana kwa mara nyingine tena. Jumatano, Novemba 16, ndege tatu aina ya Tupolev 95 na ndege zingine zilionekana juu ya bahari ya Atlantiki. Ndege hizi tatu za zamani za Urusi zina uwezo wa kurusha silaha za nyuklia.
"Tutairusha ndege yetu aina ya Awacs ambayo ina piga kambi magharibi mwa Uingereza ili kuchunguza ndege hizo za Urusi, " amesema jenerali Jean-Christophe Zimmermann, Naibu Mkuu wa shughuli za ulinzi wa jeshi la anga.
Matukio haya yalikuwa yakitokea mara kwa mara wakati wa vita baridi na ndege za Urusi zilionekana kuwa hatari, wamesema marubani wa ndege za kivita za Ufaransa. Kwa sasa, jeshi la anga linafuatilia kwa karibu harakati za Urusi, lakini ndege hizo hazijaingia moja kwa moja katika anga ya Ufaransa. "Hawana nia ya kufanya mashambulizi, " amesema mmoja wa marubani wa ndege za kivita za Ufaransa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni