Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 24 Desemba 2016

Gaddafi: Kumuomboleza Gaddafi

Leo ni miaka mitano tangu kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Muammar Gaddafi ambaye alituhumiwa na nchi za Magharibi na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kwa ukatili na kukandamiza wapinzani.
Utawala wake uliangushwa kufuatia mashambulio ya ndege za kivita za nchi za Magharibi chini ya mwavuli wa shirika la kujihami la Nato.
Baada ya kuuawa kwake, maelfu ya watu walishangilia kote nchini Libya.
Lakini kadiri miaka ilivyosonga, watu wameanza kumkumbuka na kumuenzi hasa baada ya taifa la Libya kutumbukia katika misukosuko ya kisiasa na vita.
Maelfu ya watu wamekuwa wakitumia taifa hilo kujaribu kufika Ulaya, baadhi wakifariki katika bahari ya Mediterranean. Mataifa ya Ulaya pia yanalalamikia ongezeko la wahamiaji.
Katika nchi za Afrika, wakazi wa nchi ambazo Kanali Gaddafi kwa njia moja au nyingine alichangia kisiasa au kwa miradi ya ujenzi, anakumbukwa.
Mfano nchini Ghan
Karim Mohamed, 46, ambaye ni fundi wa nguo alisema Gaddafi alikuwa kama "masihi wa Afrika".
Alikuwa ameishi Libya wakati wa utawala wa Gaddafi.
"Nchini Libya, kila mtu alikuwa na furaha," anasema.
"Nchini Marekani, kuna watu wanaolala chini ya madaraja. Lakini Libya hilo halikufanyika. Hakukuwa na ubaguzi, hakukuwa na shida, hakuna lililokosekana. Kazi ilikuwa nzuri na kulikuwa na pesa pia. Maisha yangu yako yalivyo sasa kwa sababu ya Gaddafi. Alikuwa masihi wa Afrika."
Jake Wallis Simon alikutana na wanaume wengine wawili ambao pia waliunga mkono Karim.

Ndege iliyotekwa nyara Libya yatua Malta

Ndege moja ya Libya iliyoripotiwa kutekwa nyara ikiwa kwenye safari ya ndani mwa nchi imetua nchini Malta.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya shirika la ndege la serikali ya Libya, Afriqiyah, ilikuwa na abiria 118 wakati ilitekwa.
Watekaji nyara wawili waliripotiwa kutishia kuilipua ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka mji wa Sebha kusini magharibi mwa Libya ikielekea mji mkuu Tripoli kabla ya kuelekezwa nchini Malta, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Karibu watu wote waliokuwa ndani ya ndege wanaripotiwa kuondoka.
Watekaji nyara hao waliondoka ndani ya ndege hiyo na kujisalimisha.
Mmoja wao alikimbia kituo kimoja cha runinga nchini Libya kuwa yeye ni mkuu wa chama chama kinachompendelea kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi.
Meya wa mji wa Sebha nchini Libya ambapo ndege hiyo ilikuwa ikitokea anasema kuwa watekaji nyara hao wanatafuta hifadhi ya kisiasa.

Jumatatu, 19 Desemba 2016

Rais Rais Magufuli ateua mkuu mpya NIMR

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Prof Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) saa chache baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa awali Dkt. Mwele Malecela.
Taarifa kutoka ikulu imesema uteuzi wa Prof Mgaya unaanza mara moja.
Dkt Mwele Malecela, alifutwa kazi siku moja tu baada yake kutangaza kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Taarifa ya kufutwa kwake, iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa, haikueleza sababu ya kufutwa kazi kwa Dkt Malecela,
Hata hivyo, kulikuwa kumetokea habari za kukinzana kutoka kwake na wizara ya afya kuhusu kuwepo kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Alitangaza kuwepo kwa virusi hivyo nchini Tanzania siku ya Alhamisi lakini Ijumaa, baada ya habari hizo kuenea kwenye vyombo vya habari, waziri wa afya Ummy Mwalimu akatoa taarifa kukanusha habari hizo.
Dkt Mwele Malecela alikuwa ametangaza kwamba virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Kwa mujibu wake, virusi hivyo viligunduliwa wakati wa utafiti uliofanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.Kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti huo, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi vya Zika.
Hata hivyo wizara afya nchini humo, ilitoa taarifa ambapo inakanusha kuwepo kwa virusi hivyo.
"Kama nilivyoeleza mnamo Februari 2016, ugonjwa huu bado haujaingia nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa Tanzania haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika," taarifa ya wizara ya afya imesema.
Wizara hiyo inasema uchunguzi uliofanywa na NIMR ulikuwa wa kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya Zika na Chikungunya.
"Matokeo haya bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina zaidi kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani," wizara ilisema.

Asili ya Zika

Jina la virusi hivyo linatokana na msitu wa Zika, Uganda ambapo virusi hivyo vilitambuliwa kwa mara ya kwanza 1947.
Wengi wa walioambukizwa aina ya awali ya virusi walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.

Cyril Ramaphosa: Niko tayari kumrithi Jacob Zuma

Makamu wa rais nchini Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametangaza kwa mara nyingine tena kuwa yuko tayari kumrithi rais Jacob zuma kwenye uongozi wa chama cha ANC. Ndani ya mwaka mmoja, chama cha ANC kitamchagua kiongozi wake, ambaye atakiwakilisha katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019.
"Niko tayari kukitumikia chama cha ANC," alisema Cyril Ramaphosa Jumatano hii Desemba 14 kwenye redio moja nchini Afrika kusini. Hii ni mara ya pili ndani ya muda wa wiki ambapo Makamu wa rais anasema kuwa tayari kuchukua uongozi wa chama cha ANC (African National Congress).
Cyril Ramaphosa alisema kuwa anaendelea kuyasikiliza matawi mbalimbali ya chama cha ANC, akitangaza kwamba atafurahi kama atapata uungwaji mkono.Kwa kawaida Makamu wa rais anatakiwa kumrithi rais wake, lakini Cyril Ramaphosa anakwenda kwa tahadhari. Anajua kwamba kumrithi ni vigumu, kwa sababu chama cha ANC kimegawanyika kati ya wanaomuunga mkono Jacob Zuma na wale wanaompinga.
Ili kuchukua nafasi ya rais anayeshirikiana naye tangu mwaka 2012 kama kiongpzi wa chama cha ANC, Cyril Ramaphosa atapambana na mgombea mwenye ushawishi mkubwa nchini Afrika Kusini, ambaye ni Nkosazana Dlamini-Zuma, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika na mke wa zamani wa rais Zuma.
Bado hajatangaza rasmi kuwania katika uchaguzi wa urais, lakini tayari anaonekana kufanya hivyo kwa sababu anaungwa mkono na wanaounga mkono Zuma. Nkosazana Dlamini-Zuma pia anawachukulia miongoni mwa washirika wake vijana na Wanawake wa chama cha ANC pamoja na jimbo la KwaZulu-Natal ambapo anazaliwa rais Jacob Zumaya rais. Rais wa Afrika Kusini, mwenyewe anaweza pia kumuunga mkono.

Upinzani wa Gambia wamuonya Yahya Jammeh

Upinzani nchini Gambia wasema Endapo rais anayemaliza muda wake nchini humo Yahya Jammeh atakataa kuondoka Madarakani atachukuliwa kama muasi. Yahya Jammeh alirejelea kauli yake hivi karibuni baada ya kutambua ushindi wa mshindani wake Adama barrow, na kutaka kura zirudi kuhesabiwa upya.
Katikati mwa juma lililopita Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Mohamed Ibn Chambas, alisema kuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh anapaswa "kuwa tayari kukabidhi madaraka" ifikapo mwezi Januari mwakani.
Bw ibn Chambas alisema Umoja wa Mataifa hautaendelea kufumbia macho viongozi ambao hushindwa na kisha baadaye wanatumia nguvu kwa kuchukua madaraka.
"Upinzani ulishinda uchaguzi, ambao uliku halali" amesema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa wa Ban Ki-moon katika Afrika ya Magharibi.
Jumanne Desemba 13 Marais wanne kutoka Afrika Magharibi walifanya ziara katika mji mkuu wa Gambia, Banjul na kujaribu kumshawishi Yahya Jammeh kukubali kushindwa katika uchaguzi wa urais na kukabidhi madaraka, bila mafanikio.
Mihula ya miaka mitano ya Bw Jammeh itamalizika Januari 19, Mohamed Ibn Chambas amesema, huku akiongeza kuwa "atakuwa tayari kukabidhi madaraka" tarehe hiyo.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameendelea kulaani hatua ya jeshi kudhibiti Tume ya Uchaguzi na kuwafukuza wafanyakazi wote ambao kwa sasa hawawezi kwenda kazini.
Awali Ban Ki-moon alimtaka rais Jammeh kuamuru wanajeshi hao kuondoka katika tume hiyo mara moja.
Upinzani nchini Gambia umemuonya Yahya Jammeh ikiwa atakaidi kuachia ngazi, kuwa atachukuliwa kama adui wa nchi hiyo.

Papa Francis atafuta suluhisho kwa mvutano wa kisasa DRC

Papa francis anajaribu kutafuta suluhisho kwa mzozo wa kisiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwaita viongozi wa kanisa walokua wanaongoza juhudi za upatanishi kati ya serikali ya Joseph Kabila na upinzani, juu ya hatua za kuchukuliwa baada ya muda wa Kabila wa Jumatatu tarehe 19 unafika.
Mkuu wa Kanisa la Katholiki alichukua hatua hiyo baada ya viongozi wa kidini kukutana na Rais Kabila siku ya Ijuma na kiongozi wa upinzani Étienne Tshisekedi, bila ya kupata ufumbuzi.
Muungano wa upinzani wa "Ressmblemement" unampango wa kuitisha maandamano Jumatatu ambayo Wakongo wengi na Jumia ya kimataifa wanahofu yanaweza kuzusha ghasia nchini humo.
Inaripotiwa kwamba mazungumzo kati ya pande mbili yanatazamiwa kuanza tena siku ya Jumatano.
Kwa upande mwengine afisa wa juu wa Ressemblement anamhimiza Rais Joseph kabila kufikia makubaliano na kundi hilo na kuacha madaraka ili kuruhusu kipindi cha amani cha kukabiliana madaraka.
Muda rasmi wa mhula wa Kabila unamalizika jumatatu tarehe 19.
Freddy Mbuyamu Matungulu kiongozi wa kundi la Nabiso Kongo, "Kongo Yetu", anasema viongozi wa mungano wa Ressemblement wanakutana Kinshasa kuamua utaratibu wa mpito na hali ya baada ya muda wa Kabila kupita.

Wakili wa Jamii Forum anasema mteja wake anakomolewa

Wakili Benedict Ishamakaki anayemwakilisha mahakamani mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media ya nchini Tanzania, kampuni inayomiliki mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo alisema mtazamo anaouona katika kesi ya mteja wake ni kama anakomolewa.
Alipozungumza na Sauti ya Amerika-VOA inayotangaza kutoka Washington DC, mwanasheria Ishamakaki alisema ukiangalia chombo kilichomfungulia mashtaka mteja wake, katika barua kutoka kwenye chombo hicho waliandika walikuwa wanasumbuka kumuandikia barua Melo ili kupata taarifa Fulani, kwa maana hiyo kwa maoni yake mwanasheria anaona kama ni “kulipizana kisasi kwamba wewe ulikuwa unatusumbua kupata taarifa ngoja na sisi tukusumbue kupata dhamana”.
Pia aliongeza kuwa mazingira yaliyotengenezwa mahakamani siku ya Ijumaa aliposomewa mashtaka na kupelekea mteja wake kukosa dhamana kwa maoni yake anaona kama “wanachezewa mchezo Fulani”.

DR Congo imo 'hatarini

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na hatari kubwa ya kutumbukia kwenye machafuko, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetahadharishwa.
Mjumbe wa UN Maman Sidikou amesema wanajeshi 18,000 wa kulinda amani wa umoja huo ambao wamo nchini humo hawana uwezo wa kukabiliana na ghasia kama hizo iwapo zitazuka.
Maandamano yenye umwagikaji wa damu yamekuwa wakishuhudiwa mara kwa mara kufuatia hatua ya kuahirishwa kwa tarehe ya uchaguzi wa rais.
Upinzani unamtuhumu Rais Joseph Kabila kwa kujaribu kukwamilia mamlaka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake Desemba.
Watu kadha walifariki wakati wa maandamano ya kupinga serikali mwezi jana mjini Kinshasa baada ya tume ya uchaguzi kusema haingewezekana uchaguzi ufanyike Novemba.
Makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani yalishambuliwa na kuchomwa moto.
"Wadau kutoka pande zote wanaonekana kuwa tayari zaidi na kutumia ghasia kutimiza malengo yao," Bw Sidikou, mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha UN kunachojulikana kama Monusco, aliambia baraza la usalama la UN Jumanne.
Ingawa Monusco itafanya kila iwezalo kulinda raia, haina uwezo wa kukabiliana na hatari zote zilizopo."
Aliongeza: "Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeingia kipindi cha hatari kubwa kwa uthabiti wake. Kipindi kijacho kitakuwa kigumu sana, kuna uwezekano wa kufikia pahala ambapo ghasia zitazidi."
DR Congo haijawahi kuwa na rais aliyekabidhi madaraka kwa njia ya amani kwa mrithi wake tangu uhuru miaka 55 iliyopita.
Bw Kabila aliingia madarakani 2001 baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila.

Maxence Melo apewa dhamana

Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo, ambaye amekuwa akizuiliwa na maafisa wa polisi nchini Tanzania tangu Jumanne wiki iliyopita, amepewa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Masharti ya dhamana ni wadhamini wawili ambao wote walisaini bondi ya shilingi milioni 5 za Tanzania na kwamba Maxenxe hatatoka nje ya Dar es Salaam pasipo kibali cha mahakama.
Bw Melo alishtakiwa kwa makosa matatu Ijumaa.
Makosa hayo ni kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa nchini Tanzania, na kuzuia uchunguzi wa polisi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa Kimtandao.
Hakuweza kuwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana Ijumaa na alizuiliwa gereza la Keko wikendi.
Kesi itasikilizwa tena tarehe 29 Desemba.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

Taarifa za Yahoo zavuja

                                                                    

Kampuni ya mtandaoni ya Yahoo imesema Jumatano kuwa kuvuja kwa taarifa mwezi Agosti 2013 kuliweka taarifa za zaidi ya watumiaji bilioni moja kwenye hatari.
Kampuni ya mtandaoni wa Yahoo imesema Jumatano kuwa kutolewa kwa siri taarifa hapo mwezi Agosti 2013 kuliweka taarifa za zaidi ya watumiaji bilioni moja kwenye hatari. Yahoo imefafanua kuwa wizi huo wa mitandaoni ni tofauti na uliofanyika Septemba wakati kampuni hiyo ilipofichua kuwa taarifa za zaidi ya watumiaji milioni 500 zilivuja 2014.
Yahoo inaamini kuwa mtu asie na idhini Agosti 2013 aliiba taarifa zinazohusina na zaidi ya watumizi bilioni moja wa mtandao huo. Taarifa zilizoibiwa ni pamoja na majina ya watu, akaunti za barua pepe, nabari za simu, siku za kuzaliwa pamoja na mswali ya kiusalama.
Taarifa kuhusu kadi za benki inaaminika kuwa hazikuvuja. Kampuni ya Yahoo yenye makao yake Snnyville California inajiandaa kununuliwa na kampuni ya Verizon kwa dola bilioni 4.8.

Afisa wa chama cha CHADEMA hajulikani aliko

                                                                      
                                                                      Ben Saanane
Sakata la kutoweka kwa afisa wa cheo cha juu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Ben Saanane limechukua sura mpya baada ya chama hicho kutoa tamko rasmi kwamba hawajui alipo msaidizi huyo wa mwenyekiti wa taifa CHADEMA,
Kupitia mwanasheria mkuu wake Tundu Lissu, chama hicho kimeitaka serikali kupitia jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya mahali alipo Ben Saanane, msaidizi wa mwenyekiti wa taifa upande wa siasa na jamii, anayedaiwa kutoweka tangu Novemba 14 mwaka huu na mara ya mwisho kupata taarifa zake inadaiwa aliwasiliana na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Tundu Lissu amesema serikali ndio yenye ulinzi na udhibiti mkubwa wa mipaka ya nchi ambapo inao uwezo wa kufahamu kama mtu ametoka nje ya nchi au yupo ndani ya nchi hivyo wanawajibu wa kufanya kila njia ya kumpata Ben Saanane ambaye taarifa za kutoweka kwake kwa mara ya kwanza zilitolewa na ndugu zake wa karibu.
“Wakisema wamemkamata tutawauliza kwa nini wamemkamata na kumshikilia muda wote. Hatumtuhumu mtu yoyote tutauliza masuala ambayo yanahitaji kuulizwa. Huyu Ben Saanane kuna kipindi aliandikiwa barua ya kutishwa,” alisema Lissu.
Katika hatua nyingine CHADEMA pia imetaka uchunguzi wa kutosha juu ya maiti za watu zilizookotwa mto Ruvu ili kujiridhisha aina ya kifo chao licha ya kwamba taarifa za awali zilidai watu hao ni wahamiaji haramu.
Lissu alisema,” Serikali kwa maana ya jeshi la Polisi wanatakiwa kufanya inquest. Inquest ni uchunguzi wa sababu za kifo. Ilikujibu suali hiki kifo kimesababishwa na jinai au ni kifo cha kawaida."
Akanongezea kufafanua kwamba,” wale wataalamu wa uchunguzi (pathologists) lazima wafanye uchunguzi wakitaalamu kutambua huyu mtu amekufa kwa sababu gani.”
Hata hivyo Mwandishi wa VOA Dina Chahali anasema maiti za watu saba wasiojulikana ziliokotwa katika mto Ruvu mkoani pwani Desemba 11 mwaka huu.
Taarifa za awali kutoka polisi zilieleza kwamba miili hiyo inasemekana ni ya wahamiaji haramu, na tayari imezikwa. waziri mkuu Kassim Majali katika maadhimisho ya Maulid hivi karibuni pia aliagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa vifo hivyo na kutoa taarifa kamili.

Mtandao kubanwa DRC

Kampuni za mitandao katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeamrishwa kufunga mitandao ya kijamii kwanzia Jumapili hii. Hii ni kwa mujibu wa shirika la habari AFP.
Mmoja wa maafisa wa kampuni ya mtandao ameambia AFP kamba wamepokea amri hiyo kutoka kwa serikali kubana mtandao wote. Muhula wa Rais Joseph Kabila chini ya katiba unatarajiwa kumalizika Jumatatu ya wiki ijayo.
Wanaharakati wameanzisha kampeini kwenye Twitter #ByeByeKabila, kama njiya ya kumshinikiza kiongozi huyo kuachia ngazi. Chini ya katiba ya DRC Rais Kabila alistahili kumaliza muhula wake Decemba mwaka huu na kufanyike uchaguzi Mkuu.
Hata hivyo tume ya uchaguzi ilisema haikuwa tayari kuanda uchaguzi. Mazungumzo ya kitaifa ambayo yalisusiwa na vyama vikuu vya upinzani yalipendekeza uchaguzi kuahirishwa hadi mwaka 2018, ambapo Kabila ataongoza kipindi cha mpito.
Licha ya kwamba mahakama ya kuu imeridhia makubaliano hayo, hata hivyo wapinzani wamesema lazima Kabila aondoke madarakani kwanza na kuundwe utawala wa mpito bila yeye kuongoza.
Rais huyo ameahidi kwamba hatagombea mwaka 2018, lakini wapinzani wamepinga hilo. Kumekua na maandamano yaliokumbwa na ghasia na vifo kushinikiza Joseph Kabila kuheshimu katiba ya nchi na kustaafu. Katiba haimkubalii kuwania Urais tena baada ya kumaliza mihula miwili.

Binti wa rais wa zamani wa auawa

                                                                       
        Binti wa Rais wa zamani nchini Msumbiji, Armando Guebuza, Valentina Guebuza ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Maputo. Mumewe, Zofino Muiuane amekamatwa na polisi kufuatia tukio hilo lililofanyika Jumatano.
Bi Guebuza alikua na umri wa miaka 36 na imeripotiwa alipigwa risasi mara kadhaa nyumbani kwake na kufariki dunia kutokana na majeraha wakati akipelekwa hospitalini.Mumewe alikamatwa katika moja wapo ya maeneo ya burudani mjini Maputo, kwa mujibu wa gazeti moja.
Valentina Guebuza aliorodheshwa nafasi ya saba miongoni mwa wanawake chipukizi wenye ushawishi Barani Afrika na jarida la Forbes mwaka wa 2013. Alishikilia nafasi ya juu katika kampuni kadhaa za mawasiliano pamoja na biashara zinazomilikiwa na familia.
Mumewe bwana Muiuane ni mfanyibiashara na aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya sigara ya 'British American Tobacco'. Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2014 kwenye sherehe iliyohuhduriwa na wageni 1,700 akiwemo Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Mfalme wa Zwaziland Mswati wa Tatu na binti wa Rais wa Angola Isabel dos Santos. Walijaaliwa na mtoto wa kike mwaka uliopita. Armando Guebuza alistaafu kama Rais mwaka wa 2014 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Polisi waendelea kumzuilia mwasisi wa Jamii Forums

                                                                       

aarifa kutoka kwa Jamii Forums inasema Bw Melo alizuiliwa kwa kutotoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
Alitarajiwa kufikishwa kortini Jumatano lakini hilo halikufanyika.
Badala yake, polisi walifika afisi za Jamii Forums kufanya upekuzi kisha wakawahoji wafanyakazi na kuchukua maelezo ya utendaji kazi wao.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanasema Melo anashikiliwa kinyume cha sheria kwani sheria inataka mtu asishikiliwe na polisi kwa muda unaozidi saa 24 bila kuwasilishwa kortini.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilitoa taarifa Jumatano kulaani kuendelea kuwekwa kizuizini kwa Bw Melo.
"Kituo kinalitaka jeshi la polisi kuheshimu katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 1977 inayotoa haki kwa kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru," taarifa ya kituo hicho ilisema.
Kupitia taarifa, mratibu wa kitaifa wa shirika la watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania (THRDC) Bw Onesmo Olengurumwa aliwataka maafisa wa polisi kumwachilia huru mara moja Bw Melo kwa sababu "wameshindwa kumfungulia mashtaka kortini katika muda unaotakikana kisheria."
Aliitaka serikali kuhakikisha Sheria ya Makosa ya Kimtandao haitumiwi kukandamiza uhuru wa kujieleza katika mtandao nchini Tanzania.
Wakili wa Melo, Jebra Kambole anasema Ijumaa wana mpango wa kuiandikia Mahakama Kuu ombi la kuiomba iwalazimishe polisi kumpeleka Melo mahakamani hapo afunguliwe mashtaka au aachiliwe

Njia 10 za kujikinga dhidi ya virusi vya Zika

                                                                    

Katika mataifa 20, ambapo virusi hivyo vinaaminika kuchangia kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vidogo, na hasa Brazil, tahadhari imetolewa.
Ni mlipuko wa maradhi ambao unaendelea, na Dkt Anthony Fauci, ambaye ni mtaalamu wa maradhi ya kuambukiza katika Taasisi ya Taifa ya Afya Marekani.
Kuenea huku kwa kasi kwa virusi vya Zika ndiko kwa karibuni zaidi kati ya magonjwa manne ya virusi yanayoenezwa na mbu mataifa ya Magharibi katika kipindi cha miaka 20, anaandika Dkt Fauci kwenye makala katika jarida la kimatibabu lathe New England Journal of Medicine.
Mlipuko huu unafuata mlipuko wa maradhi ya kidingapopo (homa ya dengue), virusi vya Nile Magharibi, na majuzi zaidi, chikungunya. Sawa na maradhi haya, virusi vya Zika pia huenezwa na mbu.
Lakini kinyume na virusi hivyo vingine, hakuna chanjo dhidi ya Zika. Je, ni njia gani iliyopo ya kukabiliana na virusi hivi?

1. Kutumia dawa au mafuta ya kufukuza mbu

Ushauri wa kwanza kabisa ni kuepukana na mbu. Kituo cha Kudhubiti na Kuzuia Maradhi (CDC) nchini Marekani kinapendekeza watu wajipake mafuta yenye kemikali za kufukuza mbu kama vile N, N-diethyl-meta-toluamide (DEET) au picaridin.
Mafuta haya yanafaa kujipakwa mara kwa mara, kwa kufuata maagizo kwenye mikebe, au mtu anapoanza kuumwa na mbu. Mtu anafaa kujipaka baada ya kujipaka mafuta ya kukinga ngozi dhidi ya miali ya jua.
Mafuta mengi ya kufukuza mbu ni salama hata kwa kina mama waja wazito, lakini ni vyema kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kuanza kuyatumia.

2. Kuvalia mavazi ya kufunika mwili

Wataalamu pia wanakubaliana kwamba inafaa kuvalia mavazi yanayofunika mwili vyema. Mfano shati au nguo zenye kufunika mikono na pia suruali au long’i ndefu. Mavazi yanafaa kuwa mazito kuzuia mbu kufikia ngozi.
Katika baadhi ya mataifa, mavazi huwekwa dawa maalum aina ya permethrin, ambao hufukuza mbu.
Iwapo utajipaka mafuta ya kufukuza mbu, usijipake na kisha kufunika maeneo uliyojipaka kwa nguo unazovalia.

3. Kuzuia mbu kuingia nyumbani

Ikiwezekana, wataalamu wanawashauri watu walale ndani ya nyumba zilizojengwa vyema na kuwekwa kinga ya kuzuia mbu kuingia.
Usiku, lala chini ya neti zilizotibiwa.
Lakini usitahadhari usiku pekee kwani mbu aina ya Aedes aegypti, wanaoeneza virusi vya Zika, hupenda sana kuuma watu mchana.

4. Chunga mimea inayokua ndani ya nyumba

Ingawa ni muhimu kuzuia mbu kuingia, ni muhimu hata haidi kuzuia mbu kuzaana. Na mbu huhitaji maji.
Watu wanashauriwa kuchunga sana maeneo yenye maji yaliyosimama kwani huko ndiko viluwiluwi wa mbu huwa. Maeneo haya ni pamoja na mikebe, maeneo ya kuwapa mifugo na wanyama wengine lishe, jagi za kuweka maua, vibanda vya kufugia ndege na mimea ya kupandwa ndani ya nyumba.
Ni vyema pia kusafisha mifereji ya maji mara kadha kila wiki, mufunika matangi ya mali na vidimbwi la sivyo kuweka dawa ya krolini (krolini huwafukuza mbu).
Maji ambayo yametulia kwa zaidi ya siku tano yanafaa kutupwa kwa kumwagwa ardhi kavu, kwani viluwiluwi wa mbu watafariki baada ya maji kukauka. Kiasi kidogo tu cha maji kinatosha kwa viluwiluwi hao kukua kwa hivyo, ni vyema kuosha na kukausha vyema maeneo hatari.

5. Kufunika taka

Maeneo ya kutupwa taka mara nyingi huwa na maji na hutumiwa sana na mbu kuzaana.
Ili kuzuia hili, ni vyema kufunika taka, hasa katika mifuko ya plastiki.
Tairi kuukuu na vitu vingine vya ujenzi pia vinafaa kuwekwa vyema, kwani sana huhifadhi maji ambayo yanaweza kutumiwa na viluwiluwi wa mbu.

6. “Kunyunyizia dawa”

Maafisa nchini Brazil, ambako virusi vya Zika vimeenea sana, wanatafakari wazo la kunyunyizia maeneo yaliyoathiriwa na virusi hivyo dawa ya kuua mbu.Hii inachukuliwa kama njia ya dharura kabla ya michezo ya Olimpiki, ambayo itaanza mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti.
Hata hivyo, kuna utata kwani njia hii inaweza kuwa na madhara mengine kwenye mazingira na pia kuathiri afya ya wakazi.

7. Kudhibiti mbu

Serikali katika nchi kadha za Amerika Kusini tayari wameanza kampeni ya kuangamiza mbu wanaobeba virusi vya Zika kwa kutumia teknolojia.
Moja ya njia tata zinazopendekezwa ni kueneza mbu waliofanyiwa mabadiliko ya kijeneti ambao hawana uwezo wa kuzaana. Hili litapunguza idadi ya mbu na kuzuia ugonjwa huo kuenea.
Wengine wamejaribu mbinu nyingine, mfano jiji la Itapetim nchini Brazil. Maafisa mjini humo wanatumia samaki kuangamiza mbu huo.
Samaki hao hula mayai ya mbu na hivyo kuzuia kuongezeka kwa idadi ya mbu hao.

8. Vifaa ya kukabili mbu nyumbani

Maafisa wa serikali wanapojaribu kukabiliana na mbu kwa kiwango kikubwa, watu binafsi manyumbani pia wanatumia njia mbalimbali kukabili mbu.
Wanatumia vifaa mbalimbali vya kuwawinga na kuwaua mbu. Mfano ni kutumia kifaa kinachoiga mwili na kutoa hewani ya kaboni dayoksaidi pamoja na joto, ili mbu waingie ndani wakidhani ni binadamu.
Mitambo mingine ya kunyunyiza dawa ya kuua mbu pia inatumiwa, lakini inapingwa na baadhi ya watu kwani inaathiri pia nyuki, vipepeo na wadudu wengine.

9. Kukwepa kusafiri

Wale wanaoishi maeneo ambayo hayajaathirika na virusi hivyo, wanajizuia kusafiri.
CDC imewashauri wanawake waja wazito nchini Marekani kuahirisha ziara zao Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean kadiri wawezavyo.
Kituo hicho kimewashauri wanawake wanaopanga kusafiri maeneo hayo kutafuta ushauri wa madaktari kwanza.
Shirika la Afya Duniani (WHO), hata hivyo, halijaunga mkono ushauri huo wa CDC.
“Kwa kutumia ushahidi uliopo, WHO haipendekezi vikwazo vya usafiri au biashara kuhusiana na virusi vya Zika. Lakini kama tahadhari, mataifa mbalimbali yanaweza kutoa mapendekezo mbalimbali ya kiafya na kuhusu usafiri kwa raia wake, kwa kuzingatia utathmini,” WHO imesema.

0. Kuzuia kuenea

Mtu anapoambukizwa, hatua zaidi zinafaa kuchukuliwa kuzuia kuumwa tena na mbu wiki ya kwanza baada ya kuugua, CDC inasema.
Hii ni kwa sababu virusi vya Zika vinaweza kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine kupitia damu baada ya kuumwa na mbu.
Ingawa hatari ya kuenezwa kwa virusi hivi kupitia kujamiiana haijathibitishwa kisayansi, baadhi wanapendekeza watu watumie mipira ya kondomu hadi wiki mbili baada ya kupona.
Aidha, watu wachukue tahadhari kuepusha kuambukizwa virusi hivyo kupitia mate na majimaji ya mwili.

Virusi vya Zika vyagunduliwa nchini Tanzania

                                                                        

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.
Kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti huo, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi vya Zika.
Dkt Mwele Malecela ameambia BBC kwamba kwa sasa serikali inaangazia kuzuia wajawazito wasiumwe na mbu ambao wanaaminika kueneza virusi hivyo.
"Bado tunajaribu kuangalia ni aina gani ya virusi vya Zika. Lakini hiyo ni dhahiri, tukizingatia kwamba mbu wanaoambukiza Zika wako nchini kwetu na mazingira yaliyoko nchini kwetu hayatofautiani sana na yale ya Amerika ya Kusini na nchi kama Thailand ambako ugonjwa huo unapatikana," amesema Bi Malecela.
                                                                         

"Ugunduzi huu tumeupata kwa watu na tutaendelea kufanya kazi kuangalia kama tutaupata kwa mbu ambao utatuhakikishia basi kwamba ugonjwa huo ina maana umekuwepo nchini ni vile tu ulikuwa haujaonekana."
"Heri nusu shari kuliko shari kamili, kulielewa jambo na kujua kwamba lipo nchini na kujua kwamba wajawazito wanaweza kuzaa watoto wenye matatizo haya kutatuwezesha kuzuia ugonjwa huyu. Tutahakikisha nguvu zetu za kupambana na mbu wanaoeneza virusi hivi zinaongezeka."
Virusi vya Zika zimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa wakiwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo katika mataifa ya Amerika Kusini na sana Brazil.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania, Dkt Malecela, alipokuwa akitangaza matokeo ya utafiti huo mjini Dar es Salaam alisema uchunguzi wao ulionesha kati ya watoto 80 waliozaliwa wakiwa na matatizo ya kimaumbile, asilimia 43.8 walikuwa na virusi vya Zika.
Mapema mwaka huu, serikali ya Tanzania iliwaagiza madaktari wote kuwa macho kuhusu hatari ya virusi hivyo mlipuko ulipotokea nchini Brazil.
Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya mapenzi.
Haijabainika iwapo aina ya virusi vya Zika vilivyopatikana Tanzania ni vile ambavyo vimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Amerika Kusini.
Virusi vya aina hiyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika katika visiwa vya Cape Verde mwezi Mei mwaka huu.
Jina la virusi hivyo linatokana na msitu wa Zika, Uganda ambapo virusi hivyo vilitambuliwa kwa mara ya kwanza 1947.
Wengi wa walioambukizwa aina ya awali ya virusi walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.
Lakini kwa aina ya sasa, ambayo mlipuko wake ulianza mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Brazil, dalili zake zimekuwa kali na virusi hivyo vinaaminika kusababisha kudumaa kwa ubongo na kasoro nyingine mwilini.
  • 1947: Wanasayansi wanaotafiti kuhusu homa ya manjano msitu wa Zika, Uganda wagundua virusi hivyo kwenye tumbili.
  • 1948: Virusi hivyo vyapatikana kutoka kwenye mbu aina ya Aedes africanus msitu wa Zika
  • 1952: Visa vya kwanza vya binadamu kuambukizwa virusi vya Zika vyaripotiwa Uganda na Tanzania
  • 1960-80: Virusi vya Zika vyapatikana kwenye mbu na tumbili maeneo ya kati Afrika
  • 1960-80: Virusi vya Zika vyapatikana maeneo yenye misitu na mvua nyingi Asia, ikiwemo India, Indonesia, Malaysia na Pakistan
  • 2007: Virusi vya Zika vyaenea nje ya Afrika na Asia, kwanza katika visiwa vya Yap kwenye bahari ya pasifiki
  • 2012: Watafiti wagundua aina mbili tofauti za virusi vya Zika, virusi vyenye asili Afrika na vingine vyenye asili Asia
  • Machi 2, 2015: Brazil yaripoti visa vya watu kuugua kutokana na maambukizi ya virusi vya Zika
  • Julai 17: Brazil yaripoti visa vya watoto kuzaliwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo
  • Okt. 30: Visa vya watoto kuzaliwa an vichwa vidogo Brazil vyaongezeka
  • Novemba 2015-Januari 2016: Visa vya Zika vyaripotiwa Suriname, Panama, El Salvador,
  • Mexico, Guatemala, Paraguay, Venezuela, French Guiana, Martinique, Puerto Rico,
  • Guyana, Ecuador, Barbados, Bolivia, Jamhuri ya Dominika, Nicaragua, Curacao,
  • Na Jamaica
  • Feb. 2, 2016: Kisa cha kwanza cha Zika kuenezwa Marekani charipotiwa, kikidaiwa kutokana sana na ngono badala ya kuumbwa na mbu.
  • Mei 20: WHO yatangaza kupatikana kwa virusi vya Zika kwa mara ya kwanza Afrika kipindi cha sasa cha mlipuko, katika visiwa vya Cape Verde. Virusi hivyo ni vya aina sawa na virusi vilivyosababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil.
  • Agosti 3, 2016: Wataalamu Marekani watangaza kuanza kwa majaribio ya chanjo dhidi ya Zika.

Jumatatu, 12 Desemba 2016

Jammeh akataa kuachia madaraka



Rais Yahya Jammeh aliyeiongoza Gambia kwa kiasi miaka 22  ametangaza ijumaa usiku kwamba hakubaliani tena  na  matokeo yaliyompa ushindi mpinzani wake Adama Barrow na  kutaka uchaguzi mpya ufanyike.Jammeh ametoa onyo kali akiwataka wagambia wabakie majumbani mwao na kutothubutu kuingia mitaani kuandamana.Inaarifiwa wanajeshi walionekana wakiweka vizuizi vya magunia ya mchanga katika maeneo muhimu kote kwenye mji mkuu Banjul hali ambayo inatajwa kusababisha hali ya wasiwasi kote katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo linaelekea kutumbukia katika mgogoro mpya Wa kisiasa.
Uchunguzi uliofanyika kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa Desemba Mosi yameonesha kutokea kwa dosari zisizokubalika upande wa tume ya uchaguzi alisema Jammeh katika hotuba yake iliyooneshwa kupitia Televisheni ya Taifa na kuonegeza kwamba hatokubali tena kuachia madaraka  kwa mgombea wa upinzani Adama Barrow.Zaidi rais huyo alisema'' kama nilivyokuyakubali matokeo ya uchaguzi kwa nia nzuri naamini kwamba tume huru ya uchaguzi ilikuwa huru na ya kweli na ya kutegemewa,Natangaza kwamba sikubaliani na matokeo kwa hali yoyote.
Jeshi limetawanywa katika mji mkuu  huku Marekani ikilitaka jeshi hilo kuendelea kuheshimu uatawala wa sheria na matokeo ya urais.Tayari upinzani umejibu hatua ya rais Jammeh kwa kumkosoa na kusema kupitia mitandao ya kijamii kwamba anakwenda kinyume na demokrasia lakini pia upinzani umewataka wananchi wagambia wabakie watulivu.Matokea ya hadi sasa yanaonesha Adama Barrow alishinda kwa asilimia 43.29 ya kura wakati Jammeh akipata asilimia 39.64 na idadi jumla ya waliojitokeza kupiga kura ni asilimia.Marekani kupitia balozi wake mjini Banjul imetowa mwito wa Utulivu na kulitaka jeshi liendelee kuheshimu utawala wa kisheria na matokeo ya uchaguzi wa rais.
Desemba 2 rais Jammeh alitoa hotuba iliyovuta hisia kubwa miongoni mwa wananchi wa Gambia baada ya kukubali kushindwa na kuahidi kumpokea madaraka mpinzani wake kwa njia ya amani tangazo ambalo lilizusha vifijo na nderemo katika nchi hiyo.
Lakini sasa Jammeh amegeuza msimamo na kusema kwamba uchaguzi wa Desemba Mosi ulikuwa ndio uchaguzi uliokabiliwa na udanganyifu mkubwa kabisa kuliko chaguzi zote katika historia ya Gambia.Nchi jirani ya Senegal imetoa tamko la kulaani kinachoendelea Gambia huku nchi hiyo ikilitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kulijadili suala hilo na pia kumtolea mwito Jammeh kuyakubali matokeo na kupisha kipindi cha mpito kwa njia ya amani na kuyakabidhi madaraka.

Jumatano, 30 Novemba 2016

Njama za mauaji alizoepuka Fidel Castro

                      Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith.
Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.
Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa ,kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.
Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.
Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika
Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.
Mipango yote hiyo ilitupiliwa mbali.
Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi kuugundua,ripoti hiyo ilisema.
Mmoja ya wapenzi wa Castro wa zamani ,Marita Lorenz alisajiliwa.
Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka katika kinywaji cha Castro.Lakini Castro aligundua jaribio hilo na anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.
''Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza kuniua,"Bbi Lorenzo alisema Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na gazeti la New York daily.
Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea kuvuta sigara yake.''Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na uhakika juu yangu.Alinikumbatia na tukafanya mapenzi''.
Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini Panama.
Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.
Watu wanne ikiwemo mtoro mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.
Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya Castro ambaye pia anajulikana '' The Beared'' aonekana kama chombo cha kukejeliwa badala ya kumuua.
Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.
Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.
Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.
''Nimevaa fulana ya kawaida'',alisema.
Miongo kadhaa awali mwaka 1975, tume ya bunge la seneti nchini Marekani ilifichua maelezo ya njama nane dhidi ya maisha ya Castro kwa kutumia vifaa ambavyo tume hiyo inasema ''vinachosha akili''.
Njama moja iliopangwa na ambayo karibu ifaulu mara mbili ilikuwa ile ya kutuma dawa za sumu Cuba na kuwapeleka watu kumuua kiongozi huyo.
Ulikuwa wakati kama huo ambapo rais Kennedy, ambaye aliruhusu uvamizi wa kumuondoa madarakani rais Castro mwaka 1961 aliuawa, ambapo ajenti wa CIA alikuwa anatoa kalamu yenye sumu ilio na sindano kwa ajenti mmoja wa Cuba ili kumuua kiongozi huyo.

Mkurugenzi wa CIA amuonya Trump

                    Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani CIA amemuonya rais mteule wa Marekani Donald Trump kwamba kusitisha makubaliano ya mpango wa nyuklia na Iran itakuwa ''hatari na upuuzi''.
Katika mahojiano na BBC ,John Brennan pia alimshauri rais huyo mpya kuwa na tahadhari kuhusu ahadi mpya za Urusi akiilaumu Moscow kwa mateso yanayoendelea nchini Syria.
Katika kampeni yake ,bw Trump alitishia kufutilia mbali mpango wa mnyuklia nchini Iran mbali na kuashiria kufanya kazi kwa karibu na Urusi.
                    Bw Brenan atajiuzulu mnamo mwezi Januari baada ya kuhudumia shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne.
Katika mahojiano ya kwanza na vyombo vya habari vya Uingereza ,Brennan alitaja maswala kadhaa ambapo alisema kuwa utawala mpya unafaa kuzingatia kwa busara na heshima, ikiwemo lugha inayotumiwa kuhusu ugaidi, uhusiano na Urusi, mpango wa kinyuklia wa Iran na vile siri za shirika hilo hutekelezwa

Makampuni ya kigeni yalalamikia kodi

                         Baadhi ya makumpuni makubwa ya kigeni yaliyowekeza nchini Tanzania huenda yakafikiria kupunguza au kusitisha shughuli zake kwa sababu ya masharti magumu yanayowekwa dhidi ya makampuni hayo, ikiwemo kodi kubwa.
Kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanywa na shirika la habari la Reuters pamoja na wakurugenzi wakuu wa makapuni ya kigeni yaliyowekeza nchini Tanzania, kiasi ya makampuni sita yanafikiria mipango mipya kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini, mawasiliano ya simu au usafirishaji kwa kutumia meli. Hiyo yote inatokana na juhudi zinazofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuubadili uchumi wa nchi hiyo.
Makampuni matatu yamesema huenda yakapunguza shughuli zake za uwekezaji kwenye taifa hilo la Afrika  Mashariki, huku makampuni mengine mawili yakisema yanafikiria kutanua zaidi shughuli zake katika nchi jirani na kampuni moja imesema inaandaa mchakato wa kujiondoa kabisa nchini Tanzania. Makampuni hayo yaliombwa kutotajwa majina kwa sababu ya umuhimu wa suala hili na kwa sababu mipango yao hiyo bado haijatangazwa hadharani.
Kampuni moja bado haijatoa msimamo wake jinsi ya kukabiliana na mageuzi hayo ya serikali ya Tanzania, huku makampuni matano yakisema kuwa mipango yao haikuathirika na mageuzi hayo, ikiwemo miradi miwili mikubwa, ule wa kiwanda cha kusindika gesi asilia-LNG wenye thamani ya Dola bilioni 30 na mradi wa kiwanda cha mbolea wenye thamani ya Dola bilioni 3.
                                    Tanzania na uwekezaji wa kigeni
Tanzania inategemea zaidi uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, kuliko nchi nyingine za ukanda huo, kutokana na ukubwa wa uchumi wake. Mwaka uliopita nchi hiyo ilipokea zaidi ya Dola bilioni 1.5, kwenye uchumi ambao thamani yake ilikuwa chini ya Dola bilioni 45. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na Benki ya Dunia.
Rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye amepewa jina la utani ''Tingatinga'' kutokana na miradi yake ya miundombinu na aina ya uongozi wake, alizindua mchakato wa mageuzi yake ya kiuchumi, baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo mwaka uliopita, akiahidi kuubadilisha uchumi wa nchi hiyo, kuondoa urasimu na rushwa pamoja na kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi.
Mwaka huu serikali ya Magufuli iliongeza kodi katika utumaji wa fedha kwa kutumia simu za mkononi, mabenki, huduma za utalii na zile za usafirishaji wa mizigo. Kodi ya mapato kwa mwaka wa fedha 2014/2015 jumla ilikuwa Shilingi za Tanzania trillioni 9.8 ambazo ni sawa na Dola bilioni 4.5. Kwa mwaka wa fedha 2016/2017, serikali ina lengo la kukusanya kodi ya mapato zaidi ya trilioni 15.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Adolf Mkenda, amesema wameyasikia malalamiko yanayotolewa na milango iko wazi, lakini wanahakikisha kuwa kila mtu analipa kodi anayopaswa kulipa kwa kuzingatia haki. Amesema lazima kuwepo na mageuzi mapya ambayo ni magumu, ili kuufanya uchumi kuwa imara.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Richard Kayombo amesema ongezeko la kodi ya mapato lilihitajika kwa ajili ya kulipia miundombinu mipya nchini humo. Makampuni makubwa ya kigeni ambayo yamewekeza nchini Tanzania ni pamoja na yale ya nishati, uhandisi, mawasiliano ya simu, madini, na usafirishaji kwa kutumia meli.

Majivu ya Fidel Castro kusafirishwa Santiago

                                                                           

            Mwili wa Fidel Castro aliyefariki akiwa na umri wa miaka 90, Ijumaa wiki jana, ulichomwa moto kulingana na matakwa yake. Majivu yake yatapitishwa katika miji kadhaa nchini humo kwa siku tatu kwanzia leo, kabla ya kufikishwa mji wa Santiago ambako ndiko atazikwa siku ya Jumapili.
Mji wa Santiago unaojulikana kama chimbuko la ukomunisti wa Cuba, ndiko mapinduzi yaliyoongozwa na marehemu Castro yalianzia mnamo mwaka 1953 na akachukua urais mwaka 1959.  Hapo jana mamia ya maelfu ya waombolezaji walifika kumpa heshima za mwisho jijini Havana.
Rais wa Bolivia ni miongoni mwa waliohudhuria misa hiyo na alisema: "Fidel hajafa kwa sababu wanaopigania uhuru hawafariki. Huyo ni Fidel. Hajafa kwa kuwa mawazo hayafi hasa mawazo yanayoleta ukombozi. Fidel hajafa kwa kuwa mapigano hayajaisha hasa mapigano dhidi ya utengano. Fidel ni kama yuko hai kuliko zamani akiendeleza vita kuokoa makazi yetu ya pamoja".
Mazishi yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa wakiwemo marais Nicolas Maduro wa Venezuela, Daniel Ortega wa Nicaragua, Evo Morales wa Bolivia na Rafael Correa wa Equador, kando na wakuu wa nchi za Amerika ya kusini na mfalme wa zamani wa Uhispania Juan Carlos.
Uhusiano wa Cuba na Marekani
                                                                            



Fidel Castro alitawala Cuba kwa miaka 47, hadi alipojiuzulu mwaka 2006 kufuatia hali yake ya kiafya, na kumkabidhi nduguye Raul Castro. Tangu wakati huo hajajitokeza hadharani japo inaaminika alikuwa na wasiwasi na uhusiano ulioimarishwa mwaka 2014 kati ya nchi yake na hasimu wao wa jadi Marekani. Haijabainika ikiwa uhusiano huo utaendelea kuimarika baada ya Januari rais mteule wa Marekani Donald Trump atakapochukua rasmi urais.
Akitoa hotuba ya rambirambi jijini Havana, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema "Cuba haikutafuta madini ya dhahabu, almasi au mafuta barani Afrika. Wacuba walitaka uhuru na mwisho wa unyanyasaji wa bara la Afrika kutumiwa kama kiwanja cha kuchezewa na nchi kubwakubwa huku watu wakiteseka".
Fidel Castro alipendwa na wengi duniani hasa Amerika ya kusini na Afrika, kwa kusimama dhidi ya Marekani, huku akizindua mipango ya elimu bure na huduma za afya bila malipo kando na kuwatuma madakitari wao katika mataifa mengine duniani kutoa misaada ya kiafya.
Lakini wengine walimshutumu kuwa kiongozi wa kiimla aliyevuruga uchumi kutokana na sera zake za usosholisti na kuwanyima wacuba haki za kibinadamu mfano uhuru wa kujieleza.

Jumamosi, 26 Novemba 2016

Timu ya Trump yagawanyika

Mgawanyiko katika timu ya mpito ya Rais-mteule Donald Trump kuhusu nani ateuliwe kuwa waziri wa mambo ya nje umeanza kutoka hadharani, na kusababisha nafasi hiyo kubaki wazi mpaka tofauti ndani ya timu hiyo zipatiwe ufumbuzi.
Makundi yanayopingana katika timu hiyo ya mpito yamegawanyika baina ya mgombea urais Mrepublican mwaka 2012 Mitt Romney na meya wa zamani wa jiji la New York Rudolph Giuliani.
Katika ujumbe wa Twitter Alhamisi, mshauri wa Trump, Kellyanne Conway alieleza hisia za upande unaompinga Romney. Conway alisema amepata "rundo" la maoni yenye wasiwasi ambayo yanahoji utiifu wa Romney ambaye alimshambulia sana Trump wakati wa kampeni za urais.
Wale wanaompinga Giuliani kama waziri wa mambo ya nje wanadai kuwa uhusiano wake mkubwa na makampuni ya nje huenda ukasababisha mvutano mkubwa katika vikao vya kumthibitisha katika baraza la seneti. Wanahoji pia endapo mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 ana nguvu za kuweza kuwa anasafiri sana nje ya nchi kama kazi hiyo inavyohitaji.
Rais huyo mteule, ambaye amejizolea sasa sifa ya kugeuza misimamo yake, amewasifu wote Romney na Giuliani. Trump inasemekana aliwaambia wasaidizi wake kwamba Romney "anafanana" na nafasi hiyo lakini pia amekuwa akimsifu Giuliani pia.
Wengine ambao wanasemekana kufikiriwa katika nafasi hiyo ni pamoja jenerali mstaafu na mkurugenzi wa zamani wa CIA David Petraeus na Seneta Bob Corker wa Tennessee.

Mpiga picha Hamilton afariki

                     Mpiga picha Muingereza,mwenye utata David Hamilton, anayejulikana kwa kupiga picha za uchi za wana mitindo vijana, amepatikana amefariki nyumba kwake mjini Paris.
Taarifa za vyombo vya habari za Ufaransa zinasema dawa zilipatikana kandao ya maiti yake lakini kilichosababisha kifo chake bado hakija bainika.
Hadi kifo chake mpiga picha huyo mwenye umri wa miaka thamanini na tatu alikuwa akiendesha shughuli zake mjini Paris.
Alijizolea umaarufu wake miaka ya sitini. Hivi karibuni Hamilton,alituhumiwa kwa ubakaji na mwanahabari mmoja na kumekuwa na madai sawa na hayo kutoka kwa watu tofauti wanaoshughulika na kampuni za mamode hasa watoto.
Mapema wiki hii,Bwana huyo hata hivyo alitoa taarifa kukanusha vikali madai hayo na kutishia kuchukulia hatua za kisheria vyombo vya habari wanaoendeleza uvumi huo dhidi yake.

Moto mkali wawaka Israel,

              Takriban watu elfu 60 wameyakimbia makaazi yao  wakati ambapo polisi na vikosi vya wazimamoto wanapelekwa kwa wingi katika mji wa Haifa ambako inahofiwa kwamba moto huo mkali unaweza kuendelea kutokana na hali ya ukame inayoandamana  na upepo.  Watu kadhaa wamelazwa hospitali kutokana na madhara ya kuvuta moshi lakini hakuna taarifa zinazoashiria kuwa kuna watu walio katika hali mahututi.  Mamia ya nyumba za watu ziliharibiwa katika mkasa huo, Israel hapo jana ililazimika kuwaita maafisa wa jeshi wa akiba kuja kuungana na polisi wa nchi hiyo pamoja na wazima moto.  Vile vile maafisa hao waliitumia ndege maalum ya kupambana na moto mchango uliotolewa na jamii ya kimataifa.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Israel Micky Rosenfeld amesema shughuli za kuwahamisha watu zilifanyika jana usiku katika mji mdogo ulio karibu na jiji la Jerusalem baada ya nyumba kadhaa katika mji huo kushika moto.  Hadi kufikia sasa watu 12 wamekamatwa na wanatuhumiwa kuhusika na moto huo.  Viongozi wa Israel wanahisi kwamba moto huo umeanzishwa kwa
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaumu vitendo vya uchochezi moingoni mwa Wapalestina kuwa ndio chanzo cha mashambulio hayo.  Moto huo ulianza siku tatu zilizopita katika eneo la jamii ya Neve Shalom karibu na mji wa Jerusalem eneo ambalo jamii za Kiarabu na Kiyahudi zinaishi pamoja.  Baadae moto ulizuka upande wa kaskazini katika eneo la Zichron Yaakov na kwengineko karibu na mji wa Jerusalem kabla ya moto mkubwa kuanza katika mji wa Haifa.  Nchi kadhaa zikiwemo Urusi, Ufaransa, Cyprus, Uturuki,Croatia,Ugiriki na Italia zimetuma misaada yao ya kupambana na moto huo.  katika hatua isiyo ya kawaida Wapalestina pia wamejiunga na wazima moto wa Israeli kusaidia kuuzima moto huo.
                   Maafa haya ni mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2010 wakati Israel ilikumbwa na moto mkubwa uliowahi kutokea katika historia, moto huo ulisababisha vifo vya watu 42 na wazima moto waliweza kuuzima baada ya siku nne pale ndege maalum ya kuzima moto ilipofika kutoka Marekani na kutokea wakati huo Israel imeimarisha vifaa na jeshi lake la kupambana na moto, imenunua ndege maalum za kuzima moto ambazo zina uwezo wa kumwaga maji mengi katika eneo husika.

,Fidel Castro amefariki dunia

                                                                     

Kiongozi mashuhuri ,mwanamapinduzi , aliekuwa  Rais  wa  Cuba,Fidel  Castro  amefariki  dunia  akiwa  na  umri  wa miaka 90.Taarifa juu ya kifo cha mwanamapinduzi  huyo ilitolewa, na ndugu  yake,  Rais Raul  Castro kwenye  televisheni  ya  serikali alisema: " Wapendwa  watu wa Cuba,  marafiki wa Amerika yetu na  dunia  nzima, nikiwa  na majonzi mazito,  nawapa  taarifa ,kwamba  kamanda  mkuu wa mapinduzi  ya Cuba,Fidel Castro Ruz  amefariki  dunia."
Fidel  Castro  aliiongoza  Cuba, baada  ya kuyafanikisha mapinduzi yaliyoung'oa  utawala  wa  dikteta  Fulgencio  Batista  mnamo mwaka  wa 1959. Hatua alizochukua ikiwa pamoja  na  kuleta mageuzi katika sera  ya  ardhi  na  kutaifisha viwanda na  makampuni , zilisababisha uadui  kati yake  na  Marekani.
Marekani  ilijibu kwa kuiwekea  Cuba  vikwazo vya  kibiashara.  Hata  hivyo  Cuba
ilipata misaada  mikubwa  kutoka Umoja  wa kisoviet na hivyo  kuwa tegemezi wakati  wote.  Kisiwa cha Cuba kiliingia katika kipindi kigumu sana cha matatizo ya kiuchumi  baada ya Umoja  wa kisoviet kusambaratika mnamo mwaka wa 1990 .Hata hivyo mfumo wake wa kikomunisti uliweza kukihimili kipindi hicho hadi hivi karibuni ambapo Cuba na Marekani zilirejesha uhusiano wa kibalozi baina yao.
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro amemsifu Fidel Castro kwa uongozi wake. Nae kiongozi wa zamani wa urusi Mikhael Gorbachev amemsifu Castro kwa kuiimarisha Cuba.

Jumamosi, 19 Novemba 2016

Ndege za kivita za Urusi zaonekana kwenye anga ya pwani ya Ufaransa

                     Ndege kuu za kivita za Urusi zimeonekana kwa mara nyingine tena katika anga ya Ulaya. Taarifa hii imetolea na jeshi la Ufaransa. Jumatano jioni, Novemba 16, ndege za kivita aina ya Tupolev 95 zilipita kwenye anga ya kaskazini mwa Ulaya na kisha karibu na pwani ya Ireland na kuingia Ureno, zikipitajuu ya bahari ya Atlantiki kabla ya kugeuza na kurudi nyuma.
Jeshi la Ufaransa ambalo katika miezi ya hivi karibuni lilikuatana mara kadhaa na ndege hizo limetuma ndege ya upelelezi ilikufuatilia ndege hizo za Urusi. Lakini kwa sasa, ndege hizo za Urusi zinaonekana zikiwa mbali kidogo na ardhi ya Ufaransa. Hii ni mara ya tatu tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo jeshi la Ufaransa linakutana na tukio hili.
Februari 17, ndege mbili aina ya Tupolev-160 zilikaribia pwani ya Ufaransa na zilionekana kwenye rada ya ndege za kivita za Ufaransa aina ya Rafale, Septemba 22 ndege hizo zilionekana kwa mara nyingine tena. Jumatano, Novemba 16, ndege tatu aina ya Tupolev 95 na ndege zingine zilionekana juu ya bahari ya Atlantiki. Ndege hizi tatu za zamani za Urusi zina uwezo wa kurusha silaha za nyuklia.
"Tutairusha ndege yetu aina ya Awacs ambayo ina piga kambi magharibi mwa Uingereza ili kuchunguza ndege hizo za Urusi, " amesema jenerali Jean-Christophe Zimmermann, Naibu Mkuu wa shughuli za ulinzi wa jeshi la anga.
Matukio haya yalikuwa yakitokea mara kwa mara wakati wa vita baridi na ndege za Urusi zilionekana kuwa hatari, wamesema marubani wa ndege za kivita za Ufaransa. Kwa sasa, jeshi la anga linafuatilia kwa karibu harakati za Urusi, lakini ndege hizo hazijaingia moja kwa moja katika anga ya Ufaransa. "Hawana nia ya kufanya mashambulizi, "  amesema mmoja wa marubani wa ndege za kivita za Ufaransa.

Mwili wa msichana kuhifadhiwa

                   Msichana ambaye alitaka mwili wake ugandishwe na kuhifadhiwa kwa matumaini kwamba anaweza kurejeshewa uhai wakati mmoja siku za usoni, alipata ushindi wa kihistoria saa chache baada ya kufariki dunia.
Msichana huyo alitaka mwili wake uhifadhiwe kwenye friji maalum baada ya kufa kwa matumaini kwamba anaweza kurejeshewa uhai, na hata ikiwezekana aponywe, baadaye. Mamake alimuunga mkono lakini babake alikuwa anapinga wazo hilo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 14 alikuwa anaugua aina nadra sana ya saratani.
Jaji katika mahakama ya Uingereza aliamuru kuwa mama yake ndiye angekuwa na usemi wa mwisho kuhusu mwili wake.
Mwili wa msichana huyo, aliyefariki mwezi Oktoba, sasa umesafirishwa kwa ndege hadi Marekani kuhifadhiwa.
Msichana huyo alikuwa anaishi London na alitumia mtandao wa intaneti kusoma zaidi kuhusu teknolojia ya kuhifadhi miili ya cryonics miezi ya mwisho ya uhai wake.

Matumaini siku za usoni

                 Cryonics ni teknolojia inayotumia kuuhifadhi mwili kwa kuugandisha kwa matumaini kwamba huenda ikawezekana kuufufua au kupata tiba siku za usoni.
Msichana huyo alimwandikia jaji na kumwambia kwamba alitaka "kuishi muda mrefu" na hakutana "kuzikwa ardhini".
Aliandika: "Nafikiri kuhifadhiwa kwa teknolojia ya cryonic kutanipatia fursa ya kutibiwa na kuamshwa - hata kama ni baada ya miaka mia moja."
Jaji Justice Peter Jackson, alimtembelea msichana huyo hospitalini na anasema aliguswa sana na ujasiri ambao msichana huyo alikuwa nao katika kukabiliana na maradhi aliyokuwa anaugua.
                    Kwenye uamuzi wake, alisema, uamuzi huo haukuwa kuhusu usahihi au kutofaa kwa cyronics bali mzozo kati ya wazazi wa msichana huyo kuhusu hatima ya mwili wa binti yao.

Mwili kugandishwa

                     Cryonic ni shughuli ambayo imekuwa na utata mwingi na hakuna ajuaye iwapo inawezekana kufufua miili iliyogandishwa kufikia sasa.
Kuna vifaa Marekani na Urusi ambapo miili inaweza kuhifadhiwa kwenye madini ya naitorjeni kwenye baridi kali (chini ya nyozijoto -130C) - lakini huduma hiyo haipo Uingereza.
Gharama ya kugandisha mwili kwa muda usiojulikana inakadiriwa kuwa takriban £37,000.

Barua ya msichana kwa jaji

                   "Nimetakiwa kueleza ni kwa nini nataka jambo hili lisilo la kawaida lifanyike.
"Nina miaka 14 pekee na sitaki kufariki dunia lakini najua nitafariki dunia.
"Nafikiri kuhifadhiwa kwa njia hii ya cyronic kutanipa fursa ya kutibiwa na kuamshwa - hata kama ni miaka mia moja ijayo.
"Sitaki kuzikwa ardhini.
"Ninataka kuishi na niishi muda mrefu na nafikiri siku za usoni huenda kukapatikana tiba ya saratani ninayougua na kuniamsha.
"Ninataka kupata fursa hii.
"Hayo ndiyo mapenzi yangu.

                          Wazazi wa msichana huyo walitalakiana na msichana huyo hakuwa amekutana na babake kwa miaka sita kabla yake kuanza kuugua.
Mamake aliunga mkono mapenzi yake ya kutaka mwili wake uhifadhiwe kwa kugandishwa lakini babake alikuwa anapinga.
Babake alisema: "Hata kama itawezekana afufuliwe na atibiwe tuseme miaka 200 ijayo, huenda hatapata jamaa yeyote anayemjua na huenda asikumbuke mambo mengi. Atakuwa katika hali ya masikitiko ikizingatiwa kwamba ana miaka 14 na atakuwa Marekani."
Ingawa baadaye alibadili msimamo wake na kusema anaheshimu uamuzi wa bintiye, alitaka kuuona mwili wa bintiye baada ya kifo chake, jambo ambalo msichana huyo alikuwa amekataa.
Jaji alisema ombi la msichana huyo lilikuwa la kipekee kuwahi kuwasilishwa England na Wales, na labda kwingineko.

Kuhitajika kwa sheria

              Jaji Jackson alisema kesi hiyo ni mfano wa matatizo mapya yanayoletwa na sayansi kwa wanasheria.
Msichana huyo alifariki Oktoba akifahamu kwamba mwili wake ungegandishwa, lakini jaji alisema kulikuwa na matatizo siku aliyofariki.
Wahudumu wa hospitali na wakuu wao walieleza wasiwasi kuhusu jinsi mwili wake uliandaliwa kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Hilo lilifanywa na kundi la watu wa kujitolea Uingereza kabla ya mwili huo kupelekwa Marekani.
Amedokeza kwamba mawaziri wanafaa kutafakari uwezekano wa kutoa kanuni na sheria za kusimamia uhifadhi wa miili kwa kutumia teknolojia ya cyronic siku za usoni.

Madonsela ashinda tuzo ya Forbes

                                                               

                    Aliyekuwa mlinzi wa maslahi ya umma nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela ametawazwa kuwa mtu mashuhuri zaidi wa Forbes wa mwaka 2016.
Bi Madonsela aliwashinda marais watatu wa Afrika, raia mwenzake wa Afrika Kusini na watu wan chi ya Rwanda katika kushinda tuzo hiyo.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake Ameenah Gurib wa Mauritania walikuwa wameteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Mwingine ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Michiel le Roux ambaye ni mwanzilishi wa benki ya Capitec.
                      Bi Madonsela, aliyetangazwa mshindi kwenye hafla iliyoandaliwa Nairobi Alhamisi jioni, amejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini. Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa miaka sita.
Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani.
Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011.
Aliwahi kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga mkono alipofanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia tajiri ya Gupta.
Alimchunguza pia Rais Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla.
Bi Madonsela ni mama wa watoto wawili.
Alikuwa wakili na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa harakati za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Huu ni mwaka wa sita kwa tuzo hiyo ya Forbes kwa mtu mashuhuri zaidi Afrika kutoleewa.

Washindi wa awali ni:

  • 2011 - Sanusi Lamido Sanusi, aliyekuwa wakati huo Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria.
  • 2012 - James Mwangi, CEO wa Benki ya Equity, Kenya
  • 2013 - Akinwumi Adesina, aliyekuwa wakati huo Waziri wa Kilimo Nigeria.
  • 2014 - Aliko Dangote, mwenyekiti wa CEO wa kampuni ya Dangote Group, Nigeria.
  • 2015 - Mohammed Dewji, CEO wa kampuni ya MeTL Group, Tanzania

Alhamisi, 17 Novemba 2016

Rais Dr John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016

:Rais Dr John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge katika mkutano wake wa 5 mjini Dodoma
                                                           

ICC yaziomba nchi za Afrika kutojivua uanachama

                                                                                 


                           Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ya ICC imezitolea wito nchi za Afrika kutojiondoa kutoka mahakama hiyo.Wito umetolewa wakati wa kuanza kwa mkutano wa kila mwaka wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma
Nchi kadhaa za Afrika katika siku za hivi karibuni zimetangaza zinajiondoa kutoka mahakama ya ICC. Kwanza ilikuwa Burundi, kisha Afrika Kusini na Gambia ikafuata mkondo. Siku ya Jumatatu, wiki hii, Gambia iliifahamisha rasmi Umoja wa Mataifa azma yake ya kujiondoa.
Rais wa ICC Sidiki Kaba, mwanasiasa wa Senegal amewaomba viongozi wa Afrika kutojiondoa ICC akisema katika ulimwengu uliozongwa na ghasia zinazosababishwa na itikadi kali kuna haja ya dharura ya kulinda misingi na haki ya kila mtu.
                                                                       

Kaba amekiri kuwa mahakama ya ICC iliyoanzishwa mwaka 2000 kushughulikia kesi mbaya zaidi za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu inapitia wakati mgumu na kuongeza kuna uchunguzi ulioendeshwa na mahakama hiyo ambao haukuwa wa haki lakini amewahakikishia viongozi kuwa wamesikilizwa.
Viongozi wa Afrika wameishutumu mahakama hiyo kwa kuwaandama na kutoendesha shughuli zake kwa usawa na haki. Kenya, Namibia na Uganda zimedokeza zina nia ya kujiondoa kutoka mkataba wa Roma. Kamishna wa tume ya kutetea haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema licha ya wenye nguvu kutaka kujiondoa kutoka ICC, waathiriwa kwingineko wanaililia mahakama hiyo kuwasaidia.   
                                                                         
    
                                  l Hussein amesema kwa kujiondoa kutoka mkataba wa Roma, viongozi huenda wakajipa kinga lakini kwa gharama ya kuwanyima watu wao ulinzi wa kipekee na kuonya mtindo mpya wa kutaka kujitenga wimbi ambalo limeighubika dunia kwa sasa kutapelekea mashambulizi zaidi dhidi ya mahakama hiyo.
                                                                             

Kati ya kesi kumi zinazoendeshwa na ICC, tisa ni kuhusu nchi za Afrika na iliyosalia inaihusu Georgia. Hapo jana mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda alisema kuna sababu ya kuanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Marekani kwa uhalifu wa kivita walioufanya Afghanistan.
Urusi imetangaza rasmi inaondoa saini yake katika mkataba wa Roma ikisema mahakama ya ICC imeshindwa kutimiza matumaini ya Jumuiya ya kimataifa, haiko huru na ina mapendeleo. Mwaka 2000, Urusi ilitia saini mkataba huo wa Roma lakini haikuidhinisha rasmi mkataba huo.
                                                                           


Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini agizo la kujiondoa kutoka kwa mkataba wa Roma baada ya nchi hiyo kutofurahishwa na jinsi ICC inavyochunguza kesi ya vita kati ya Urusi na Georgia vya mwaka 2008. Mkataba wa Roma una nchi wanachama 120.

Kuuawa kwa Osama Bin Laden

                                                                       

                 Mwaka 2001, mwezi Desemba katika milima ya Tora Bora baada ya mapambano ya siku kumi na moja toka tarehe 6 hadi 17 na mabomu kadhaa kudondoshwa katika milima hiyo hatimaye askari wa miguu walianza zoezi la kuikagua milima hiyo kuangalia kama kuna masalia yoyote muhimu yanayoweza kuwapa fununu ya kuielewa vita waliyoianzisha kati yao Majeshi ya Marekani na Wanamgambo wa Taliban.
Katika mchakato huo wa ukaguzi wanajeshi wa marekani walifanikiwa kumuokota kijana mmoja wa umri wa mika 21 akiwa hai. Baada ya kumuokota wanajeshi kadhaa wakampakia katika chopa ya kivita na kurudi nae katika kambi ya kijeshi ya Bagram Air Base iliyo nchini Afghanistan.
Baada ya kufika katika kambi ya Bagram wanajeshi wakaanza kumuhoji kijana huyo ajieleze yeye ni nani na alikuwa anafanya nini katika milima ya Tora Bora.
Baada ya kujitambulisha kijana huyo akawaeleza kuwa alikuwa anawinda katika milima hiyo ya Tora Bora na kwa bahati mbaya akajikuta ameingia kwenye eneo ambalo hakujua kuwa kulikuwa na mapigano ya kijeshi.
                   Maafisa wote wa kijeshi hawakuamini maelezo haya na waliendelea kumuhoji kwa siku kadhaa lakini yule kijana alishikilia maelezo yake yale yale kuwa alikuwa anawinda milimani.
Baada ya kutokuwepo kwa mafanikio yoyote ya kumuhoji kijana huyu Maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi katika kituo cha Bagram wakawasiliana na maafisa wa CIA waliopo nchini Afghanistan na kuwaeleza juu ya tukio hilo. Maafisa hao wakawashauri kuwa kijana huyo wakabidhiwe wao ili wamuhoji wao kwa kina.
                    Siku tatu baadae kijana huyo akakabidhiwa kwa maafisa wa CIA na wao wiki moja baadae wakamsafirisha kutoka Afghanistan mpaka kwenye jela za siri (Black Sites) za CIA zilizopo ulaya katika nchi ya Romania na baadae akaamishiwa jela za siri nchini Poland.
Baada ya kijana huyo kufikishwa huko mahojiano yakaendelea na akaendelea kushikilia msimamo wake kuwa alikuwa anawinda kwenye milima ya Tora Bora. CIA ikaamua kupanua wigo wake zaidi ili wamtambue. Wakachukua alama zake za vidole na kuziingiza katika mfumo wa alama za vidole wa nchi karibia zote za kiarabu lakini wakapata matokeo sifuri, hakukuwa na taarifa zozote zinazoshabihiana alama za vidole za kijana huyo.
Hii ilikuwa na maana nyingi lakini maana moja kubwa ni kwamba kijana huyu hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu katika maisha yake, alikuwa ni 'raia mwema'!
CIA wakaanza kuhisi labda kijana huyu kweli hakuwa na hatia yoyote. Lakini kabla hawajalipa nafasi wazo hilo kukua kwenye vichwa vyao, wakaakua wafanye kitu cha kubahatisha, wakaingiza alama za vidole za kijana huyo katika mfumo wa kiusalama wa nchini kwao marekani na matokea ambayo waliyapata hakuna ambaye aliweza kuamini.
                       Kumbukumbu za mifumo ya kiusalama ya nchi za marekani zilionyesha kuwa mtu mwenye alama hizo za vidole zinafanana kabisa na mtu ambaye alijaribu kuingia nchini marekani siku ya tarehe 3 Agosti 2001 katika uwanja wa ndege wa Orlando, Florida akitokea Dubai.
Maafisa wa uhamiaji wa uwanja wa ndege wakamkataa kuingia nchini marekani kutokana na sababu kadhaa. Kwanza kijana huyo alikuwa na fedha dola 2,800 pekee na hii iliwapa shida maafisa wa uhamiaji kuelewa angewezaje kuishi nchini marekani? Pili kijana huyu alikuwa amekata tiketi ta kwenda pekee (one way ticket).
                        Sababu hizi mbili zilipelekea maafisa wa uhamiaji wa uwanja wa ndege kuhisi kijana huyu alikuwa na mpango wa kuwa muhamiaji haramu kwani dalili hizo zilionesha kuwa hakuwa na mpango wa kurudi tena kwao. Hivyo basi maafisa hao wa uhamiaji wa uwanja wa ndege wa Orlando wakamkataa kijana huyo juingia nchini marekani na wakamrudisha alikotokea.
                          Maafisa wa CIA walishitushwa na jambo hili na wakawasiliana na vyombo vingine vya usalama nchini Marekani na pasipo kupoteza muda maafisa kutoka shirika la upelelezi la FBI wakafika katika uwanja wa ndege wa Orlando, Florida ili wapate taarifa zaidi kuhusu nini hasa kilitokea siku ya Agosti 3 2001 siku ambayo kijana huyo alikataliwa kuingia nchini marekani.
Baada ya FBI kufika uwanja wa ndege waliomba kuzungumza na maafisa uhamiaji waliokuwepo siku ya tarehe 3 Agosti pia waliomba wapatiwe mikanda ya video ya kamera za ulinzi za uwanja wa ndege.
Baada ya kuangalia mikanda hiyo ya video, FBI waligundua jambo kubwa zaidi ambalo hawakulitegemea kabisa. Kamera za ulinzi zilizo nje ya uwanja zilirekodi gari inayomilikiwa na Mohamed Atta likiwa limepaki nje ya uwanja wa ndege.
Kwa wasiomfahamu Mohammed Atta ndiye alikuwa mtekaji kiongozi wa watu walioteka ndege za kimarekani na kwenda kuzigongesha katika magorofa ya WTC siku ya tarehe 11, Septemba 2001. Pia ndiye aliyeendesha moja wapo ya ndege hizo zilizotekwa.
                      Kwahiyo FBI wakang'amua kuwa siku hiyo Mohammed Atta alifika uwanja wa ndege kumpokea kijana huyo lakini kwa bahati mbaya maafisa uhamiaji walimkataa asiingie Marekani.
Hii ilikuwa na maana kwamba kama kijana huyu asingelitiliwa shaka na maafisa wa uhamiaji basi alitakiwa kuwa mojawapo ya washiriki walioteka ndege na kuzilipua katika majengo ya WTC siku ya Septemba 11, 2001.
Taarifa hizi ziliishitua FBI na pasipo kuchelewa wakawataarifu maafisa wa CIA katika jela ya siri nchini Poland ambako kijana huyu alikuwa anashikiliwa, na baada ya maafisa hawa kupata taarifa hii mara moja wakawasiliana na Makao Makuu ya CIA Langley, Virginia nchini Marekani.
Mara baada ya taarifa hizi kufika Makao Makuu ya CIA, Mkurugenzi wa CIA Bw. Leon Panetta akaamuru kijana huyo awekwe 'mahali salama' kwa ajili ya 'mahojiano' zaidi.
Ndege ikaandaliwa na safari ya kuelekea gereza la Guantanamo Bay ikaanza.
Jina halisi la kijana huyu anaitwa Mohammed al-Qahtani kipindi anakatwa alikuwa na umri wa miaka 21 na kwa sasa ana miaka 36 na ni mfungwa namba 63 (ISN 10063) katika gereza la Guantanamo Bay.
                            NDANI YA GUANTANAMO: 'MAHOJIANO' ZAIDI
                       Baada ya kijana al-qahtani kufikishwa katika gereza Guantanamo ambapo aliwekwa selo katika jengo lililoitwa Camp Delta 'mahojiano' zaidi yakaendelea. Licha ya mambo yote ambayo vyombo vya usalama viligundua juu yake lakini kijana yule aliendelea Kushikilia msimamo wake kuwa alikuwa anawinda kwenye milima ya Tora Bora.
Ilifikia hatua mpaka Katibu mkuu kiongozi wa makamu wa rais wa kipindi hicho Bw. David Addington pamoja na mshauri wa ikulu Bw. Alberto Gonzales walifika binafsi katika jengo la Camp Delta ndani ya gereza la Guantanamo mahsusi kwaajili ya kuongea na kijana al-qatani ili aeleze ukweli lakini kijana huyo akashikilia msimamo kuwa yeye ni muwindaji.
Ndipo hapa ilipofikia hatua hii Waziri wa Ulinzi wa Marekani wa wakati huo akaidhinisha 'Mbinu za Mahojiano Zilizoboreshwa' (Enhanced Interrogation Techniques) zitumike kumuhoji kijana huyo.
Mbinu hizi zilizoboreshwa zilikuwa zinajumuisha kwa mfano kutesa mfungwa kwa kumnyima pumzi kimateso kwa kumiminia maji (waterboarding), mikao ya msongo (stress positions), kumnyima usingizi n.k.
            Uamuzi huu ulikuja kuleta mushkeli na watu wa haki za binadamu miaka iliyofuata.
Baada ya maafisa waliokuwa wanamuhoji kupewa idhini ya kutumia 'mbinu zilizoboreshwa' inasemekana kwamba kijana al-Qahtani ndiye mmoja wa wafungwa wa Guantanamo waliovunja rekodi kwa kuhojiwa muda mrefu zaidi kwa 'mbinu zilizo boreshwa'. Inasemekana kijana al-Qahtani alihojiwa kwa siku 48 mfululizo!
Baada ya 'mahojiano ya kina' yaliyochukua siku 48 kwa kutumia 'mbinu zilizoboreshwa' hatimae al-Qahtani akafunguka na kueleza ukweli.
Kwanza akakiri kuwa jina lake ni Mohammed al-Qahtani na ni raia wa Saudi Arabia.
Pia akakiri kuwa ni yeye ndiye aliyekataliwa kuingia nchini Marekani siku ya Tarehe 3, Agosti 2001 na akaeleza kuwa alipewa maagizo na mtu anayeitwa Khalid Sheikh Mohammed ili aje marekani kwaajili ya kazi maalumu. Pia alieleza kuwa aliwahi kupatiwa mafunzo maalumu ya utendaji wa kishushushu na mawasiliano ya usiri (Operational training in Covert Communications) na aliyempatia mafunzo hayo alijulikana kama Abu Ahmed al-Kuwait.
Baada ya kupewa maelezo haya ilikuwa ni hatua kubwa kiasi kwa CIA lakini bado kulikuwa na mambo kadhaa hayakuwa sawia.
Kwa upande Khalid Sheikh Mohammed (KSM) mtu ambaye kijana huyu alimtaja kuwa ndiye alyemuagiza aje Marekani, mtu huyu alikuwa anafahamika vizuri na CIA. Walimfahamu kuwa ndiye moja wa Lutenati wa ngazi za juu wa kikundi cha Al Qaeda na ndiye 'mchora ramani' wa mashambulizi ya septemba 11, 2001.
                        Lakini mtu wa pili (Abu Ahmed al-Kuwait) aliyetajwa na huyu kijana kuwa ndiye aliyempatia mafunzo kijana juu ya ushushushu na mawasiliano ya siri, mtu huyu CIA walikuwa hawamfahamu. Ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kulisikia jina hilo.
Hivyo basi kipaumbele kikawekwa kwamba kijana huyu 'ahojiwe' zaidi ili atoe taarifa zitakazofanikisha kumpata KSM (Khalid Sheikh Mohammed) 'mchora ramani' wa mashambulizi ya Septemba 11. Mahojiano kwa kutumia mbinu zilizobordshwa yakaendelea.
Kwa msaada wa maelezo waliyoyapata kutoka kwa kijana al-Qahtani maafisa wa CIA kwa kushirikiana na maafisa wa ISI (Inter-Service Intelligence - Idara kuu ya masuala ya usalama na ushushushu nchini Pakistani) walifanya oparesheni maalumu ya kumkamata KSM (Khalid Sheikh Mohammed) baada ya kumuwinda kwa muda mrefu sana na hatimae siku ya Machi 1, 2003 walifanikiwa kumkamata KSM akiwa hai katika katika jimbo la Ralwapindi nchini Pakistani.
Baada ya kukamatwa tu na taarifa hiyo kufika makao makuu ya CIA Langley, Mkurugenzi mkuu Bw. Panetta akaamuru KSM awekwe 'mahali salama' mara moja. Na pasipo kupoteza muda siku hiyo hiyo CIA wakampandisha ndege KSM na kumpeleka gereza la Guantanamo. Na baada ya KSM kupokelewa Guantanamo alipewa selo kwenye jengo mojawapo la Guantanamo linaloitwa Camp Echo na akatambulika kama mfungwa namba ISN 10024.
                     Kesho yake 'mahojiano ya kina' yakaanza kwa kutumia 'mbinu zilizoboreshwa'.
Haikuchukua siku nyingi za 'mahojiano' KSM akaanza kufunguka na kusema ukweli. Kwanza akakiri kuwa yeye ndiye 'mchora ramani' wa shambulizi la Septemba 11, na ni moja ya malutenati wanaotegemewa na Al Qaeda katika kueneza propaganda za kikundi hicho. Akakiri kuhusika kutafuta vijana watakaotekeleza shambulizi hilo, akakiri kusaidia baadhi yao kupata mafunzo ya urubani na akakiri kusaidia kuwaingiza marekani vijana hao.
Maafisa wa jeshi na CIA walimbana zaidi KSM aeleze ni namna gani wanaweza kuwapata viongozi wa ngazi za juu wa Al-Qaeda na hasa hasa kiongozi mkuu lakini jibu la KSM liliwashangaza kila mtu. KSM akawaeleza kuwa hata yeye afahamu kiongozi mkuu yuko wapi au anapatikanaje.
Mwanzoni walihisi anawadanganya lakini baada ya 'kumbana' zaidi wakagundua kuwa anamaanisha kuwa hajui 'kiongozi mkuu' yuko wapi wala namna ya kumpata.
KSM akawaeleza kuwa kiongozi mkuu, Osama Bin Laden aliacha kutumia simu toka mwaka 1998 maada ya mawasiliano yake ya simu ya satelaiti kudukuliwa na CIA na kuponea chupu chupu kuuwawa na wanajeshi wa kimarekani.
Akawaeleza kuwa tangu hapo aliacha kutumia na mawasiliano ya simu na mawasiliano yote mengine ya kisasa na kwa upande wa mawasiliano akawa muumini wa falsafa ambayo imekuja kutumiwa na karibia maafisa wote wa ngazi za juu wa vikundi vya wapiganaji katika mashariki ya kati, kwamba; "If you live like you are in the 'past', the 'future' will never find you"! (Ukiishi kama upo kwenye nyakati za zamani, usasa hautakukamata kamwe).
Kwa hiyo mawasiliano yote yalikuwa yanafanyika kwa mdomo kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu au kwa barua za kuandika kwa mkono.
                          CIA wakambana zaidi aeleze je yeye alikuwa anapataje maagizo kutoka kwa kiongozi mkuu na akawajibu kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa anaaminika kwa asilimia mia moja na kingozi mkuu na ndiye aliyekuwa 'mpambe' wa karibu wa Bin Laden na kwamba kwa miaka kadhaa wapiganaji wa Al-Qaeda wala malutenati wa ngazi za juu walikuwa hawajawahi kumuona Bin Laden wala hawajui alipo na maagizo yote waliyapata kwa mdomo kutoka kwa mtu mmoja pekee aliyeitwa Abu Ahmed al-Kuwait.
Maafisa wote wa jeshi na CIA waliduwaa. Hii ilikuwa ni mara ya pili wanasikia jina hili. Mara ya kwanza walilisikia kutoka kwa kijana al-Qahtani kuwa alipatiwa mafunzo ya ushushushu na Abuu Ahmed al-Qahtani na sasa wanaelezwa na KSM ambaye ni lutenati wa ngazi za juu kabisa wa Al Qaeda kuwa hajawahi kumuona kiongozi mkuu kwa miaka kadhaa na maagizo yote yalikuwa yanaletwa kwake na mtu anayeitwa Abu Ahmed al-Kuwait.
Kitu kilichowasahangza zaidi CIA ni kwamba walikuwa wanawafahamu viongozi na malutenati wote wa ngazi za juu wa Al Qaeda lakini jina hili lilikuwa jipya kwao. Hawakuwahi kumsikia Abu Ahmed al-Kuwait.
                          Wakiwa bado wapo kwenye mshangao wapigani wa kikurdi kutoka nchini Iraq wakawasiliana na serikali ya marekani kuwaeleza kuwa wamemkamata Hasaan Ghul moja ya mawakala wa Al Qaeda anayetegemewa nchini Iraq.
CIA wakampakia Hassan Ghul kwenye ndege na kumpeleka kwenye jela za siri nchini Romania.
Baada ya 'kumuhoji' kwa siku kadhaa Hassan Ghul akawaeleza kuwa maagizo yote kuhusu mashambulizi na mipango mingine anayapata kutoka kwa kiongozi mkuu Osama Bin Laden kupitia kwa mtu anayemfahamu kwa jina la Abu Ahmed al-Kuwait.
Mshangao wa CIA ukageuka kuwa kitendawili. Huyu Abu Ahmed al-Kuwait ni nani na wanawezaje kumpata?
Mkurugenzi Mkuu wa CIA akaamuru kuwa kumtambua na kumkamata Abu Ahmed al-Kuwait kiwe kipaumbele namba moja..
Baada ya mchakato wa muda mrefu hatimae mwaka 2007 CIA walifanikiwa kumtambua Abu Ahmed al-Kuwait ni nani! Wakafanikiwa kupata jina lake halisi (Ibrahim Saeed Ahmed) na kwamba mwanzoni alikuwa ni mwanafunzi wa KSM kabla hajapanda ngazi kuwa mpambe wa Bin Laden.
Baada ya kumfahamu kwa kiasi CIA wakaanzisha mpango maalum wa kumchunguza ili wapate taarifa zaidi juu yake. Ili waweze kumpata kirahisi CIA wakafanya zoezi maalum la kuwatambua ndugu zake mbali mbali waliokuwa wanaishi kwenye nchi tofauti tofauti za kiarabu.
Baada ya kuwatambua ndugu hao CIA wakafanya kazi ya kudukua mawasiliano ya simu ya ndugu zake na katika kitu kimojawapo ambacho walikigundua ni kwamba ndugu zake hao walikuwa na desturi ya kuwasiliana na namba za simu tofauti tofauti lakini zote zikiwa ni za Pakistan. Hii ilipelekea CIA kuhisi kwamba namba hizi ni za al-Kuwait lakini alikuwa anazibadilisha mara kwa mara ili kuepuka kugundulika.
                       Kwahiyo walichofanya CIA ni kusubiri siku ambayo ndugu yoyote wa al-Kuwait akipiga simu yoyote kwenda nchi ya Pakistan basi wataifuatilia namba hiyo ili wafahamu ni nani aliyekuwa anaongea naye.
Siku hiyo haikukawia sana kwani mwaka 2010 ndugu mmoja wapo alipiga simu kwenda Pakistan katika mji wa Pashwar. Kwa kutumia Wapalestina waliokuwa wanafanya kazi kwaajili ya CIA waliifuatilia simu hiyo mjini Pashwar na kuthibitisha kuwa aliyekuwa anaongea na simu hiyo alikuwa ni Abu Ahmed al-Kuwait. Baada ya al-Kuwait kumaliza kuongea na simu aliingia ndani ya gari na kuondoka na wapelelezi hao wakamfutilia kwa makini wajue anakoelea.
Pasipo kujua kuwa anafuatiliwa al-Kuwait aliendeshe gari mpaka mji wa Abbottabad. Na alipofika Abbottabad akaingia kwenye Jumba moja la kifahari. Jumba hili lilikuwa na muonekano na ulinzi uliotia shaka. Na hii ikapelekea CIA kuamini kuwa ndani ya jumba hilo hakuwa al-Kuwait pekee anayeishi bali kuna uwezekano mtu wa hadhi ya juu zaidi alikuwa anaishi humo ndani. Pengine labda kiongozi mkuu wa Al Qaeda, Osama bin Laden labda alikuwa ni mkazi humo ndani.
Waziristan Haveli
                                                                    

                     Baada ya CIA kugundua nyumba hii na kuitilia mashaka kuwa kuna uwezekano inamuhifadhi kiongozi wa hadhi ya juu wa Al Qaeda pengine labda Osama bin laden mwenyewe, hivyo wakaingiza wapelelezi katika mji wa Abbottabad ambao walinunua nyumba mjini hapo kama raia mwingine wa kawaida. Baada ya wapelelezi hao kufanikiwa kufanya mkazi mjini Abbottabad wakaanza kazi ya kukusanya taarifa juu ya jumba hilo na wakazi wake.
Wapelelezi hao ambao walikuwa ni raia wa Pakistan wanaofanya kazi kwa niaba ya CIA wakaanza kuwadodosa majirani na wakafanikiwa kupata taarifa za kutosha kiasi.
Kwanza majirani waliwaeleza kuwa jumba hilo linamilikiwa na mtu wanayemfahamu kama Arshad Khan (Abu Ahmed al-Kuwait) ambaye anaishi na kaka yake pamoja na familia zao. Majirani wakaeleza kuwa Arshad amewaeleza kuwa kuwa yeye ni msimamizi wa biashara za Hoteli za familia yao zilizopo Dubai. Pia majirani walimueleza kuwa Arshad (al-Kuwait) alikuwa ni 'mtu wa watu' na alikuwa anahudhuria karibia kila msiba mtaani kwao.
Pia walielezwa kuwa licha ya kuwa na uwezo wa kifedha huwa anapenda kufanya manunuzi ya mahitaji yake ya nyumbani hapo hapo mtaani na mara kwa mara hutoka na watoto wake kwenda kuwanunulia mikate kwenye duka la uokaji (bakery) mtaani hapo.
Pia majirani waliwaeleza kuwa wamezoea kuliita jumba hilo Waziristan Haveli (Waziristan Mansion (Kasri la Waziristan)) kwani waliamini kuwa wakazi wa jumba hilo wanatokea Waziristan.
Baada ya CIA kupata taarifa hizi kutoka kwa wapelelezi waliojipenyeza mtaani hapo wakaamua wapanue wigo zaidi kwa kuwahusisha kitengo Maalumu cha Taifa la Marekani chini ya wizara ya ulinzi (DOD) kinachohusika na kukusanya taarifa na Ushushushu wa kijiografia (National Geospatial-Inttelligence Agency - NGA) ili wafahamu nukta baada ya nukta ya jumba hilo.
Kwa kutumia picha za satelaiti na kukusanya picha kwa kutumia ndege inayojiendesha yenyewe (drone) NGA walipata taarifa zote muhimu kuhusu jumba hilo kuziwasilisha CIA.
Taarifa yao ilieleza kuwa jumba hilo lililoitwa Waziristan Haveli lipo umbali wa takribani kilomita moja na nusu kutoka kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Abbottabad cha jeshi la Pakistan. Mtaani ambao jumba hili lilikuwepo ulikuwa na makazi ya wastaafu wengi wa jeshi la Pakistan.
Jumba hili lilichukua eneo kubwa zaidi kuliko nyumba nyingene za jirani kwani jumba lilijengwa kwenye eneo la ardhi lenye ukubwa la takribani mita za mraba 3,500.
Jumba hili lilizungukwa na ukuta wenye urefu wa futi 12 lakini ndani yake ukiingia unakutana na eneo la wazi tupu alafu anakuta ukuta mwingine wenye urefu wa futi 18. Kuta zoto hizi juu yake zilikuwa na waya za miba miba na umeme.
Pia jumba hili lilikuwa na ghorofa tatu na katika balkoni ya gorofa ya tatu ilikuwa na ukuta wake wa kuikinga wenye urefu wa futi 7. Pia kulikuwa na kamera za ulinzi katika kila kona ya jumba hili.
Pamoja na hayo pia NGA waligundua kuwa ndani ya jumba hilo kulikuwa na bustani kubwa iliyopandwa mboga mboga, pia kulikuwa na kuku zaidi ya 100, sungura pamoja na ng'ombe mmoja.
Pia jumba hili lilikuwa na mdirisha madogo na machache kiasi kwamba ukiliangalia haraka haraka unaweza kudhani halina madirisha kabisa.
                      Pia idara ya ushushushu wa kijiografia ya Marekani NGA ilifanikiwa kukusanya taarifa za wakazi wa jumba hilo ambapo walifanikiwa kung'amua kuwa Kasri hilo lilikuwa na wakazi wapata 22 wanaoishi ndani yake wengi wao wakiwa ni watoto. Pa waling'amua kuwa kulikuwa na takribani wakazi watani ambao kamwe walikuwa hawatoki nje ya jumba hilo.
Baada ya NGA kuwasilisha taarifa yao kwa CIA kuhusu vile walivyovibaini kuhusu jumba hili, Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Leon Panetta alizidi kushawishika kuwa Kasri hili lilikuwa linamuhifadhi kiongozi wa hadhi ya juu wa Al Qaeda na pengine ni Bin Laden mwenyewe anaishi humo.
Hivyo basi akaamuru ufanyike uthibitisho wa mwisho kuhakiki kama ni kweli kile anachokihisi.
CHANJO FEKI
                       Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Pattena alitaka kwanza kuhakiki kama hisia zao ni za kweli kuwa Bin Laden anaishi kwenye Kasri hilo. Hivyo basi maafisa wa CIA wakaja na mpango kuwa wafanye uhakiki wa uwepo wa familia yake na kama familia yake ipo kwenye jumba hilo basi hapana shaka Bin Laden atakuwepo ndani ya hilo Kasri.
Kwahiyo maafisa hao wakaemweleza mkurugenzi wao wanachotakiwa ni kupata sampuli za vinasaba (DNA) za watoto wanaoishi ndani ya jumba hilo.
Kwahiyo mkakati ukawekwa kwamba ifanyike chanjo feki ili wapate fursa ya kuingia kwenye jumba hilo kuwahudumia watoto na wakifanikiwa kuingia watatumia mbinu kadhaa kuchukua sampuli za vinasaba za watoto eidha kwa kubakiza damu kiduchu za hao watoto kwenye sindano ya kutolea chanjo au mbinu nyinginezo.
Ili kufanikisha azma hii CIA walimuendea Daktari Bingwa aliyeitwa Shakil Alfridi ambaye alikuwa ndiye daktari mkuu katika maeneo ya Khyber mpakani na Afghanistan.
CIA wakafanikiwa kumshawishi daktari Hugo ashiriki kwenye mpango huo wa kutoa chanjo hiyo feki.
Baada ya kufanikiwa kumshawishi Dk. Shakil matangazo yakawekwa kuhusu mpango wa kutoa chanjo katika eneo hilo kwa mwezi February na Mwezi April 2011. Ili kuwapiga chenga serikali ya mji wa Abbattobbad wasihusike kwenye zoezi hilo Dk. Shakil alieleza kuwa amepata ruzuku kutoka mashirika ya kimataifa ili atoe chanjo hiyo bure na chanjo hiyo ni ya kuwakinga watoto dhidi ya Hepatitis B.
                       Hivyo basi alifanya zoezi lake kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na watu wa serekali za mitaa na manesi ambao walijumuika nae kutoa chanjo hiyo walipata posho iliyoshiba.
Ili kuepuka watu kuanza kuuliza maswali na kuwa na wasiwasi, alianza kutoa chanjo hiyo katika mitaa wanayoishi masikini kama vile mitaa ya Nawa Sher. Alifanya hivyo kwa mwezi February na aliporejea tena alitoa chanjo hiyo katika mtaa wanaoishi watu matajiri katika mji wa Abbattobad yaani mtaa wa Tabil ambapo ndipo kulikuwa na hilo jumba linalotiliwa mashaka.
Ilipofika zamu ya kutoa chanjo kwa watoto waliopo ndani ya hilo jumba walikaribishwa kwa ukarimu na Dk. Shakil mwenyewe akabaki nje getini na akamruhusu nesi aliyeitwa Bakhto aingie ndani ya kasri atoe 'chanjo' kwa watoto.
'Chanjo' ikatolewa, zoezi likaisha Dk. Shakil na manesi wake wakarejea Khyber na kukabidhi sampuli walizozipata kwa CIA.
                        Sampuli zikasafirishwa mpaka marekani, zikafanyiwa uchambuzi wa DNA kisha ikalinganishwa na DNA ya dada yake Osama Bin Laden aliyefariki dunia mwaka 2010 jijini Boston nchini Marekani kwa uvimbe kichwani.
Baada ya sampuli hizo za DNA kupimwa na kulinganishwa, majibu yakapelekwa mezani kwa Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Pattena. Baada ya Pattena kuyaona majibu hayo akatabasamu mpaka ufizi wa mwisho, akainua simu ya mezani na kupiga ikulu ya Marekani na kuomba kuongea na Rais Obama.
Mara baada ya kuunganishwa na Rais Obama, Pattena akampa taarifa Rais, taarifa iliyosubiriwa muda mrefu na kwa shauku kubwa, kwa kifupi akamueleza Rais kwa furaha "we got him.!" ("Tumempata.!")
OPARESHENI NEPTUNE SPEAR
                         Baada ya kupatikana uhakika kuwa Osama Bin Laden anaishi ndani jumba hilo lililopo Abbottabad, CIA wakafanya kikao maalum na Jemedali Msaidizi (Vice Admiral) William H. McRaven ambaye ni kamanda wa kitengo maalum kinachosimamia oparesheni maalum zinazofanywa na majeshi yote ya marekani ( Joint Special Operations Command - JSOC) ambapo katika kikao hicho CIA walimpa taarifa wa kila wanachokifahamu kuhusu makazi hayo waliyoyagundua.
Baada ya kupewa taarifa hiyo, Admiral McRaven akapendekeza kuwa wanaweza wakatuma kikosi cha makomando kufanya uvamizi kwenye jumba hilo lakini akawa na wasiwasi inaweza kuleta mushkeli na jeshi la Pakistan ambalo lipo kilomita moja na nusu tu kutoka makazi ya siri ya Bin Laden.
Baada ya majadiliano ya kina Admiral McRaven akawaagiza maafisa kadhaa kutoka Jeshi la Wanamaji (U.S. NAVY) kitengo cha Maandalizi ya ya Mapigano/vita Maalum ( Special Warfare Development Group - DEVGRU) kwamba waweke ofisi ya muda makao makuu ya CIA Langley na washirikiano kuandaa mpango maalumu utaoenda kupendekezwa kwa Rais juu ya kushugjulikia makazi yaliyoaminika kumficha Osama Bin Laden.
Baada ya miezi miwili ambayo DEVGRU waliitumia kuaandaa mpango kwa kushirikiana na CIA hatimaye wakawasilisha mapendekezo yao kwa Mkurugenzi wa CIA Bw. Pattena na kwa waziri wa ulinzi Bw. Robert Gates.
                         Kisha Rais Obama akaitisha kikao maalum cha Baraza/kamati ya usalama ya Taifa ili kujadili suala hilo.
Baada ya majadiliano marefu kwenye kikao hicho ilionekana kuwa Rais Obama alipendelea zaidi pendekezo la kulipua makazi hayo kwa bomu kutoka angani. Lakini maswali yakaibuka je ni vipi kama kuna handaki kwenye jumba hilo na Osama labda huwa anakaa chini ya hilo handaki. Katika upelelezi wao wote CIA hawakuweza kung'amua kama kulikuwa na handaki katika jumba hilo ama la.
Kwa kuzingatia hivyo basi (uwepo wa handaki) kama wataamua kulipua makazi hayo kwa bomu basi itawabidi watumie bomu lenye uzito usiopungua Kg. 910 ili liweze kusambaratisha kabisa makazi hayo pamoja na handaki kama lipo.
                         Lakini pendekezo hili nalo likawa na changamoto zake kwani kama litatumika bomu lenye nguvu kubwa hivyo, kulikuwa na nyumba kadhaa za majirani ambazo zitakuwa ndani ya kipenyo cha mlipuko (blast radius). Pia kama makazi hayo yangelipuliwa kwa bomu kusingekuwa na ushahidi wowote wa kujiridhisha kuwa Osama ameuawa kwenye shambulio hilo.
Baada ya kubainishwa kwa changamoto hizi katika kikao kilichofuata cha kamati ya Usalama wa Taifa, Obama akasitisha mpango huo wa kulipua makazi kwa bomu usitekelezwe.
Chaguo la pili lilikuwa kwa makomando wa kikosi cha Wanamaji (Navy) SEALs, wavamie makazi hayo kwa kutumia helikopta maalum zinazoruka bila kutoa kelele na sio rahisi kuonekana na Rada ya adui. Chaguo hili lilikuwa ni zuri lakini lilikuwa na changamoto moja kubwa. Kumbuka makazi haya yapo karibu kabisa na kituo cha Kijeshi cha Pakistani, itakuwaje kama wakishtukiwa kabla hawajamaliza kutekeleza oparesheni?
                         Baadhi ya watu waliokuwepo kwenye kikao akiwemo waziri wa ulinzi Bwa. Robert Gates akapendekeza kuwa labda wawashirikishe watu wa kitengo maalumu cha ushushushu cha Pakistan (ISI). Wazo hili likapingwa vikali na Rais Obama kuwa hawaamini hata chembe Wapakistani na endapo wakiwaeleza kuhusu oparesheni hiyo basi siku hiyo hiyo Osama ataamishiwa sehemu nyingine.
Obama akapendekeza kuwa kama ikitokea makomando wao wamekamatwa kabla hawajamaliza oparesheni yao basi Admiral McRaven atatakiwa ajiandae kumpigia simu Mkuu wa Majeshi Pakistani Ashfaq Parvez Kayani kumshawishi kuwaachia makomando hao wa Marekani.
Lakini pia Obama akamuagiza Admiral McRaven awaandae makomando wake kwa mapambano ya kijeshi kama ikitokea wamepewa upinzani na wanajeshi wa Pakistan na hawataki kuwaruhusu waondoke.
                        Watu wote waliohudhuria kiako hicho cha kamati ya usalama wakakubaliana na mpango huo wa kuvamia makazi ya Bin Laden kwa kutumia helikopta isipokuwa Makamu wa Rais Joe Biden pekee aliupinga mpanga huo kwa asilimia zote.
Licha ya Makamu wa Rais kuupinga mpango huo, siku ya tarehe 19 April kamati ya Usalama wa Taifa ilipokutana tena Rais Obama akatoa idhini ya awali kukubali oparesheni hiyo itekelezwe. Na ikapewa jina Oparesheni Neptune Spear.
Kesho yake McRaven pamoja na kikosi chake cha SEALs wakaondoka marekani kuelekea Afghanistan ambapo walitumia takribani wiki mbili kufanya mazoezi kuhusu oparesheni waliyoenda kuifanya.
                        Kikosi hiki kilifikia katika kambi ya Bagram nchini Afghanistan na hapo palitengenezwa mfano wa nyumba kama ile inayosadikiwa kumuhifadhi bin laden na kikosi cha SEALs wakafanya wazoezi ya kutosha jinsi watakavyotekeleza zoezi hilo.
Ilipowadia siku ya tarehe 29, Rais Obama alimpigia simu Kamanda McRaven kumuuliza juu ya maendeleo ya maandalizi. Pia akamuuliza kama alikuwa na angalau ya chembe ya shaka kuhusu kufanikiwa kwa oparesheni hiyo na kama alikuwa na shaka yoyote basi oparesheni hiyo itahairishwa. McRaven akamjibu kuwa vijana wake wako tayari kwa kutekeleza Oparesheni.
Obama akawapa idhini ya mwisho kuwa amewaruhusu kufanya oparesheni hiyo siku itakayofuata yaani tarehe 30 April.
                       Kesho yake Obama akataarifiwa kuwa oparesheni imehairishwa kwa muda wa siku moja kutokana na hali ya hewa kutokuwa rafiki na badala yake itafanyika kesho yake tarehe 1.
Jioni ya siku hiyo Obama akampigia simu tena McRaven kumtakia kilala kheri yeye na makomando wake wa SEALs na akwashukuru kwa kujitoa kwao kwa ajili ya Taifa lao.
Siku ya tarehe 1 May ilipowadia wajumbe wa kamati ya usalama wa taifa walikusanyika katika chumba maalumu cha ikulu ya marekani (situation room) kufuatilia oparesheni hiyo kupitia kwenye runinga iliyokuwa inaonyesha picha za moja kwa moja zilizokuwa zinachukuliwa ndege ya kujiendesha (drone) iliyokuwa inafuatilia tukio zima la oparesheni hiyo.
Usiku wa manane Makomando wa SEALs wapatao 79 waliruka na helikopta za kijeshi kutokea kambi ya kijeshi ya Bagram mpaka eneo la mpakani Jalalabad. Walipofika hapo wakagawana. Makomando wapatao 24 pamoja na mbwa aina ya Belgia Malinois aliyeitwa Cairo waliingia kwenye helikopta mbili aina ya Black Hawk ambazo zimeboreshwa kuzuia kuonekana na Rada ya adui na kutotoa sauti.
Makomando waliosalia waliingia kwenye chopa kubwa za kijeshi aina ya Chinook.
Makomando ambao walipanda kwenye chopa za kivita aina ya Black Hawk hawa ndio walipewa jukumu la kuvamia makazi ya Bin Laden. Makomando wengine ambao walipanda kwenye chopa kubwa za kivita aina ya Chinook hawa watakaa maili kadhaa kutoka eneo la tukio kama tahadhali ikitokea wenzao wakahitaji msaada zaidi.
                     Baada ya kujigawanya hivi safari ya kuelekea kwenye makazi ya siri ya Bin Laden ikaanza.
Baada ya kuyafikia makazi ya Bin Laden Chopa moja ilitua eneo la mbele ya jengo na nyingine ilitua nyuma kwa juu na makomando wakashuka kwa spidi ya haraka kwa kutumia kamba.
Chopa ambayo ilitua mbele ya jengo, rubani aliiweka chini kwa makosa kidogo na kusababisha mkia wa helikopta kugonga uzio wa ukuta wa nyumba na almanusuura ipinduke chini juu lakini kwa ustadi akaiweka sawa na makomando wakashuka salama ingawa helikopta tayari ilikuwa imeharibika.
Baada ya makomando wote kufanikiwa kuingia ndani ya uzio wakaanza kuisogelea mlango mkubwa wa nyumba. Pembeni ya nyumba kubwa kulikuwa na vyumba vichache vimejengwa kwa ajili ya wageni na ndani yake walitokea wanaume wawili waliokuwa na bunduki aina ya AK-47 na kuwafyatulia risasi makomando wa SEALs.
Kabla watu hao hawajaleta madhara yoyote makonmando wa SEALs waliwadondosha chini kwa risasi mbili kila mmoja. Watu hawa wawili walikuja kutambulika baadae kuwa ni Abu Ahmed al-Kuwait pamoja na kaka yake aliyeitwa Abrar.
                     Kisha makomando wakaingia ndani ya nyumba. Na baada ya kuingia ndani kuna kijana akaonekana akikimbia kupandisha ngazi kwenda ghorofa ya juu. Naye akadondoshwa chini kwa risasi. Kijana huyu naye alikuja kutambulika kama mtoto mkubwa wa kiume wa Osama Bin Laden.
Baada ya kijana huyo kupigwa risasi mlango wa chumba kilichopo ghorofa ya juu ulionekana kufunguliwa na mtu akachungulia. Pia naye akafyatuliwa risasi kadhaa zikamkosa lakini moja ikampata ubavuni. Mtu huyo aligeuka haraka na kurudi ndani chumbani lakini kabla hajaufunga mlango wa chumba vizuri komando wa SEALs alifanikiwa kuruka na kubiringika mpaka ndani ya chumba hicho.
Katika kujitahidi kujificha mtu huyo (Bin Laden) alimnyakua mwanamke mmoja aliyekuwepo humo chumbani (mkewe Mdogo) na kumsukumia kwa komando wa SEALs lakini komando alifanikiwa kumkwepa mwanamke huyo na akafanikiwa kufyatua risasi iliyompata Osama kwenye paji la uso.
Papo hapo komando mwingine naye alikuwa ameshaingia chumbani naye akafyatua risasi iliyompata Osama kifuani. Bin laden akadondoka chini na komando mmoja akamfyatulia risasi nyingine kifuani akiwa hapo hapo chini. Pale pale roho ya Osama Bin Laden ikaach mwili.
Komando mmoja akatoa simu ya mawimbi ya kijeshi na kuwasiliana na kamanda McRaven aliyekuwa amebaki kwenye kambi ya Bagram. Baada ya kupokea tu simu komando akamueleza kamanda wake kwa kifupi tu "Geranimo".
                                                                          

                     Kamanda wake nae akaitafsiri taarifa hii kwa watu waliopo Ikulu marekani pamoja na Rais Obama wakifuatilia Kupitia Satelaiti, kamanda McRaven akawaeleza "For God and for the country, Geranimo Geranimo Geranimo" kisha akamalizia "Geranimo EKIA" (EKIA - Enemy Killed In Action (Aduai ameuawa kwenye mapambano)). Geranimo ndio lilikuwa jina la fumbo (code name) la kumtambua Osama Bin Laden katika oparesheni hii.
Seneta Hillary Clinton kipindi akiwa kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani naye siku alikuwepo Ikulu ndani ya situation room anaeleza kuwa mara baada ya Rais Obama kusikia taarifa hii kwa msisimko na hisia kubwa akaongea maneno machache tu, "we got him" ("tumempata/tumemmaliza").
Baada ya kutoa taarifa hiyo kuwa wamefanikiwa kumuua Bin Laden, makomndo wa SEALs wakawakusanya wanawake na watoto wote waliowakuta ndani ya nyumba hiyo na eakawafunga kwa pingu za plastiki na kuwaacha hapo hapo. Kisha wakaubeba mwili wa Bin Laden na kuupakia kwenye Chopa.
                   Lakini kabla ya kuondoka wakailipua ile chopa iliyopata itilafu kwani isingeweza kuruka tena na hawakutaka watu wajue teknolojia yao ya siri inayotumika kwenye chopa hizo.
Zoezi lote hili lilipangwa kutumia dakika 40, lakini kutoka na umahiri wa hali ya juu wa makomando wa SEALs liliisha ndani ya dakika 30 pekee. Risasi 16 tu ndizo zilifyatuliwa na watu 5 waliuwawa (Osama, mtoto wake wa kiume, Abu Ahmed al-Kuwait, Abrar (kaka wa al-kuwait), na mke wa Abrar).
Baadaya ya hapo wakaruka mpaka kambi ya Bagram kisha mwili wa Bin laden ukapakiwa tena kwenye chopa na kupelekwa kwenye manowari ya kivita ya NAVY iliyoko baharini. Huko sampuli za DNA zikachukuliwa na mwili ukapigwa picha. Baada ya hapo mwili ukavilingishwa shuka jeupe alafu ukatumbukizwa kwenye mfuko mkubwa na imara, vikawekwa na vyuma vizito ndani yake, mfuko ukafungwa, ukatumbukizwa baharini. Huo ukawa mwisho wa Bin laden Duniani.
                                                      HOTUBA YA UTHIBITISHO
                 Jioni ya siku hiyo Rais wa marekani Barack Obama alitoa hotuba ambayo itakumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo. Alisema;
"Habari za jioni, usiku huu napenda kuwataarifu Wamarekani na Ulimwengu wote kuwa Marekani imeendesha oparesheni iliyofanikiwa kumuua Osama Bin Laden kiongozi wa Al Qaeda na Gaidi anayehusika na vifo vya maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia......"
Ulimwengu ulisimama kwa sekunde kadhaa na wengine hawakuamini masikio yao na mpaka sasa wapo wasio amini na kumeibuka nadharia nyingi mno. Lakini hiki nilichokisimulia ndicho wanachoamini CIA na serikali ya Marekani, kuwa siku ya Tarehe 1 mwezi May mwaka 2011; "Geranimo E.K.I.A..... Adui aliuwawa katika mapambano."